Dayalisisi (Figo)
Chemo & Mionzi (Kansa)
Gharama kubwa za haya matibabu, imesababisha kuchukua uhai wa ndugu zetu wengi mno!!
Bado wapo wengine wengi wapo vitandani sasa wanaugulia.
Bado wapo wengine wanatembea wakiamini ni wazima, lakini bila kujua tayari wanayo haya maradhi.
Siku zinavyozidi kwenda, ongezeko la waathirika wa maradhi haya linakuwa kwa kasi kubwa mno!!
Huku vifo vingi vikitokea kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama, na kutofika vituo vya afya mapema na kwa wakati sahihi!!
Tutaendelea kupoteza kundi kubwa sana la wapendwa wetu💔
kama hazitafanyika jitihada kubwa kupunguza gharama za matibabu na kuongeza elimu (Awareness) kuhusu afya zetu (Lifestyle), Checkup mara kwa mara!!
Kata ya Idukilo wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga. Iko jirani na Maganzo Magharibi ya Mwigumbi.
Wananchi wamemkataa Diwani fake wa ccm aliejiweka madarakani 2025…
Tangu wakati huo wananchi hawamtaki.
RPC Shinyanga amepeleka Oparesheni hapo, mamia ya watu wamepigwa na kuumizwa wengine zaidi ya 150 wana kesi mahakani Kishapu..
Uonevu huu haukubaliki.
Nimeelekeza Mawakili wa chama waingilie kati na chama ngazi ya kanda wafanye mkutano Idukilo kuzungumza na wananchi.
RPC Shinyanga sio wajibu wako kisheria kulazimishia wananchi Kiongozi wasiemtaka ambae hawajamchagua.
Klabu ya Kagera Sugar imeungana na Geita Gold FC kurejea Ligi kuu ya soka ya NBC Tanzania bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kengold FC katika uwanja wa Kaitaba, Kagera na kufikisha pointi 68 ambazo haziwezi kifikiwa na Mbeya Kwanza na Polisi Tanzania waliopo nafasi ya tatu na nne mtawalia zikiwa zimesalia mechi mbili Ligi kutamatika.
Kocha Juma Kaseja amewarejesha Wanankurukumbi Ligi kuu wakifikisha jumla ya alama 68 baada ya kushinda mechi 21, sare 6 na vichapo viwili kwenye michezo 28 ikiwa ni msimu mmoja tu tangu washuke daraja mwishoni mwa msimu wa uliopita.
MSIMAMO 🔝4️⃣ Championship
1. Geita Gold FC — mechi 28 — pointi 71
2. Kagera Sugar — mechi 28 — pointi 68
3. Mbeya Kwanza — mechi 28 — pointi 60
4. POLISI Tz FC — mechi 28 — pointi 60
#KitengeSports
Nimeamini Twitter ni sehemu ya kupoza akili na kutoa stress.
Leo Kili Fair Arusha 2026, nimefanikiwa kukutana na mwamba mmoja wa humu ndani anajifanya jobless kumbe CEO wa Kampuni moja kubwa sana ya Tours Arusha.
Ameweka stalls 4, na kila stall moja pale ni $3,000 kama sikosei.
Wachezaji wa AFRICA waliofanikiwa kucheza mpira level kubwa ULAYA wanakuwaga na mapenzi na MUNGU wao kinoma na wanamtukuza kweli.
Kuzaliwa Africa & kukulia AFRICA kisha unaenda bara la watu na kuaminiwa kuweka BENCHI wazawa sio mchezo wakuu.
YOUNG LISSU.
Dogo kaamua kuja Front kupambania haki za babaake aliepo gerezani zaidi ya siku 400.
Wakoloni weusi Hizi mbegu mbaya mnazopanda vifuani mwetu lazima mzivune.
Stay strong BRO-TUTAVUKA NA TUTASHINDA.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Issue umanifu 🎯
Niko kwenye uwanja wa fursa wa kuweza kumfungia mtu mzigo wa saa piece hata 200 kwa bei ya jumla na akapata faida mara mbili kwa Tanzania lakini issue ni uaminifu 🥹
Anaandika Askofu BAGONZA
YUDA AMECHOKOZWA; ASICHOKOZEKE❗️❗️❗️
Yuda wa Biblia alimsaliti Bwana Yesu. Siamini kama mleta hoja anamaanisha msalitiwa katika hoja yake ni sawa na Bwana Yesu!?!? Ipo siku tusiyoijua, “Yesu” huyu aliyefumbwa katika hoja hii, atafananishwa na “Mtume” asiyelinganishwa. Hapatatosha. Mleta hoja hajachagua vizuri maneno yake na mifano yake. NIMEMSAMEHE BURE.
Sakata hili lina mapichapicha 10 ya hatari.
1. Msemaji aliwahi kuchokonoana na Rais wake huko kwao mpaka akajiuzuru. Mama yetu akamchukua, akamteua. Ina maana Rais yule na Mama yetu hawako pamoja na hawaivi? Je Mama ni Yuda wa Rais yule kwa kuwa alimchukua mleta hoja ambaye ni msaliti wa Rais yule?
2. Mleta hoja ni Mzanzibari, anamnanga Yuda Mtanganyika. Hii ni kero au ufa katika muungano? Alikosekana Mtanganyika wa kumrudi Yuda Mtanganyika?
3. Mleta hoja anasali Ijumaa; anamnanga anayesali Jumapili kwa kutumia picha ya (Yuda) anayeomba huruma makanisani. Tuseme katumwa na msikiti?!
4. Maneno yake yameingia kwenye Hansard. Bunge halikukanusha. Je ni bunge zima linamwita Makamu kuwa ni Yuda?
5. Naibu Spika alipomwongoza ajikite kwenye hoja, wabunge walipiga makofi. Walifurahia Naibu Spika kuingilia au walimshangilia mtoa hoja. Je makofi hayo ni mashangilio ya tumbili wa Kijaluo anayeshangilia pori linaloungua bila kuwaza atalala wapi usiku?.
6. Hoja imetolewa siku Rais ameondoka nchini na kwa mujibu wa katiba, Makamu ndiye Mkuu wa nchi wa zamu. Mtoa hoja anamaanisha hamtambui Makamu kama Mkuu wa nchi wa zamu?
Kwa vyovyote, kuna dalili mbaya. Matiti ya binti wa Kijaluo yakiishaota, hayafichiki na hayarudi nyuma.
7. Wakristo wanaamini usaliti wa Yuda ulileta wakovu. Bila usaliti, Yesu asingekufa. Bila kifo, asingefufuka; na bila kufufuka, wokovu usingepatikana. Hakuna wokovu bila usaliti. Waliookoka wameisaliti dhambi ili wawe huru. Mleta hoja kakosea. Hakuna Yuda na hakuna Yesu katika hoja yake. Zilikuwa ni saa za jioni; Dodoma mapito ni mengi, hatujui alipitia wapi kuja bungeni.
8. Kisiasa, CCM bila tishio la upinzani wa nje, inayumba. Tulishauri mapema sana Lisu aachiwe ili aiunganishe CCM, tukapuuzwa. Angeachiwa mapema, CCM ingeungana na kusahau tofauti zake za ndani ili kukabiliana na upinzani. Hivi sasa wapo wana CCM wanamtamani Lisu ili awasaidie kuona thamani ya umoja wa chama chao. Hamjachelewa.
9. Mama alikuja na “R” nne. Moja ya “R” hizo ni REFORMS, yaani mabadiliko. Lisu akamuunga mkono Mama kwa kusema “Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi” (NO REFORM, NO ELECTION). Akakamatwa kwa uhaini wakati aliunga mkono falsafa ya 4R! Mbadilishie mashtaka mseme alikosea kumuunga mkono Mama!
10. Wenye madaraka punguzeni nguvu, ongezeni hekima. Ruto alipata urais kwa huruma ya kudhaniwa anaonewa na Uhuru Kenyata. Akakosea akatumia nguvu kumwondoa Makamu Gachagwa. Hivi sasa ana nguvu binafsi lakini urais (Presidency) ni dhaifu. Kambarage alitumia nguvu na hasira Januari 30, 1984. Mpaka anaondoka duniani, jambo hilo lilimtesa. Trump alimnanga Makamu wake Pence hadharani, akaangushwa na Biden kwenye uchaguzi. Rais na Makamu hawatenganishwi kirahisi. Si mnatuimbia maridhiano!? Ridhianeni basi ili machawa tukose kazi.
Kama Yuda alichokoza; aliyechokozwa asichokozeke. Kama Yuda amechokozwa; asichokozeke.
Wajaluo bhana! Eti, hata anayepotea ana anakokwenda.
Dadangu usinichoke maswali yangu juu ya katiba ya TZ. Unanifunza mengi juu ya katiba Siielewi vizuri katiiba . Hivi kama Bunge likimpigia Nchimbi vote of no confidence au akijiuzulu katiba inasemaje juu ya kimama? Anabaki au anaruhusiwa kuteua makamu mwingine? Yani what happens?