Top Tweets for #SikoSeli
Tanzania imefanikiwa kupandikiza uloto. Hii ni tiba inayoleta kupona kwa ugonjwa wa Siko Seli.
Hongera Tanzania
Hongera Wizara ya Afya
Hongera Hospitali ya BMH Dodoma
#sicklecell #sikoseli
#bonemarrowtransplant
WAPONA SIKOSELI BAADA YA KUPANDIKIZWA ULOTO
Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma imeandika historia ya watoto watatu kupona ugonjwa wa Sikoseli baada ya kuwafanyia matibabu ya upandikizaji wa Uloto.
Hayo yamebainishwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika wakati akitoa taarfa rasmi kwa vyombo vya habari leo jijini Dodoma baada ya mwaka mmoja tangu Hospitali hiyo ifanye Matibabu ya Upandikizaji wa Uloto kumtibu mtoto mwenye Ugonjwa wa Sikoseli
Dkt. Chandika amesema watoto hao hawana maradhi ya Selimundu tena, na kwamba serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza zaidi ya Billioni 3.6 kuwezesha huduma hizo ili kuokoa maisha watanzania.
“Leo ni siku muhimu sana, ninawataarifu watanzania, Afrika na Dunia nzima kwa Ujumla kwamba Watoto tuliyowapandikiza Uloto hawana Ugonjwa wa Selimundu, wana afya njema, na vipimo vimethibitisha hawana ugonjwa huo tena” ameeleza Dkt. Chandika.
Aidha, Dkt. Chandika, amewashukuru wazazi wa Watoto hao, ambao ni Grace Hosea (8), Elisha John (11), na Isack Kedmond (10), kwa kuiamini hospitali hiyo na kuruhusu Watoto wao kuwa wa kwanza kupokea Huduma za Upandikizaji wa Uloto.
Matibabu ya Upandikizaji wa Uloto yanagharimu kati ya Shilingi milioni 55-65, hata hivyo, tafiti zinaonesha kuwa, kumhudumia mtoto mwenye Seilimundu dawa za kupunguza makali ya ugonjwa, fedha hizo zinaweza kukidhi huduma kwa miaka mitano pekee.
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 1 katika bajeti ya Mwaka huu wa Fedha kwa ajili ya Matibabu ya Selimundu, hakuna hata mzazi mmoja ametoa fedha, gharama zote zimebebwa na serikali” ameshuku Dkt. Chandika.
Akitoa ushuda Mtoto Elisha John (11), kwa niaba ya Watoto wenzake waliyopokea huduma ya kupandikizwa Uloto, amesema changamoto zote alizokuwa nazo zimetoweka.
“Nilikuwa napata shida ya kuumwa kichwa, damu yangu ilikuwa haizidi sita, shuleni nilikuwa simalizi mwezi, lazima nitalazwa wiki nzima, sihudhurii vipindi shule, tangu nimetibiwa sijasikia maumivu yoyote”ameeleza Mtoto Elisha.
Kwa mujibu wa Mzazi wa Elisha, kumhudumia mtoto mwenye Sikoseli ni kujitoa sadaka, ambapo mzazi mmoja alilazimika kuacha kazi ili kuwa karibu na mtoto wao.
“Kupata wiki moja ya kutokuugua kwake lilikuwa jambo la muujiza, kwa miaka hiyo 11 ya kuugua kwake, ilibidi mama yake aache kujishughulisha na shughuli za kiuchumi, kwa sababu Ugonjwa huo hauna muda maalumu, hali ingeweza kubadilika muda wowote” alisema Joseph John.
Mbali na Shukrani kwa BMH na Serikali kwa nafuu aliyoipata mtoto wake, ametoa wito kwa serikali kuangalia uwezekano wa kujenga Hosteli Jirani na Hospitali hiyo, ili kusadia familia zinazotoka nje ya Dodoma kufuata huduma hiyo BMH.
Wito huo uliungwa mkono na Profesa, Cornell Uderzo, Bingwa wa Magonjwa ya Damu na Upandikizaji Uloto kutoka Shirika la Help 3 la nchini Italia, Washirika wa BMH katika huduma za Upandikizaji wa Uloto, kwa kusema kuwa hitaji la Hosteli ni Muhimu si tu kwa BMH, bali ni protokali ya matibabu hayo.
“Kote duniani, si hapa pekee, kunakuwa na makazi ya familia Jirani na Hospitali, kuziwezesha familia kukaa angalau kwa miezi 3 baada ya kuruhusiwa kutoka wodini, kuruhusu madaktari kumfuatili mgonjwa kwa karibu, ikiwa kuna changamoto yoyote, hasa maambukizi” alisema Profesa Uderzo.
Tanzania inashika nafasi ya nne duniani kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa Selimundu, ni ya 3 kwa nchi za Afrika, huku idadi ya Watoto 11,000 wakikadiliwa kuzaliwa na ugonjwa huo kila mwaka, ambapo asilimia 50 hufariki kabla ya kufikisha umri wa miaka 5.
Hospitali ya Benjamin Mkapa ilianza kutoa huduma za Upandikizaji wa Uloto mwaka jana, ikiwa ya kwanza kutoa huduma hiyo kwa nchi za Afrika Mashariki na kati, hadi sasa Watoto 7 wamenufaika na huduma hiyo, huku wengine tisa wakiwa katika mlolongo wa matibabu.

Ugunduzi wa mapema wa Sikoseli utatusaidia kuokoa maisha ya watoto wengi wenye ugonjwa wa #sikoseli. Nimeshuhudia watu wakisema watoto wao wamerogwa kutokana na kutojua kuwa mtoto ana ugonjwa wa sikoseli. Dalili za ugonjwa wa Sikoseli ni pamoja na;-
- Maumivu makali ya mwili
-Maambukizi ya mara kwa mara
-Kuvimba miguu na mikono
-Kubanwa kifua
-Upungufu wa damu wa mara kwa mara
-Ukuaji wa polepole au kuchelewa kukua kwa mtoto
#TuvunjeMduaraWaSikoSeli #MtuNiAfya #PimaAfyaYako
NDANI YA MIEZI SITA HOSPITALI ZOTE ZA HALMASHAURI ZIWE ZINAPIMA UGONJWA WA SIKOSELI KWA WATOTO WANAOZALIWA - WAZIRI UMMY
Na. WAF - Dar es Salaam
Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu amezitaka Hospitali zote za Halmashauri nchini kuwapima ugonjwa wa Sikoseli watoto wote wanaozaliwa katika Hospitali hizo ili kujua Hali zao mapema na kuanza matibabu.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo Octoba 2,2023 wakati akizindua kampeni ya kuelimisha jamii juu ya Magonjwa Yasiyoambukiza yaliyofanyika katika Hospitali ya Sinza - Palestina Jijini Dar es Salaam.
“Waganga Wakuu wa Mikoa mkalisimamie hili nataka Hospitali zote za Halmashauri nchini ndani ya Miezi Sita zipime ugonjwa wa Sikoseli kwa watoto wanaozaliwa katika Hospitali hizo kabla sijashuka vituo vya Afya”. Amesema Waziri Ummy
Waziri Ummy amebainisha kuwa zaidi ya asilimia 70 hadi 90 ya watoto wanaozaliwa na Sikoseli hupoteza maisha ndani ya kipindi cha Miaka Mitano ya mwanzo wa maisha yao kutokana na kutotambulika au kwa sababu ya unyanyapaa na kukosa elimu.
“Hali hii haikubaliki ni lazima tuchukue hatua za haraka ili kuokoa maisha ya watoto wachanga wenye ugonjwa wa Sikoseli kwa kuwatambua mapema ili kuhakikisha wanapata matibabu kwa wakati.
Waziri Ummy amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anatoa fedha za dawa kwa asilimia 100 kila mwezi, fedha hizo wanaruhusiwa kuzitumia kwa ajili ya kununua mashine za kupima ugonjwa wa Sikoseli.
Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema ugonjwa wa Saratani umeongezeka kwa kasi Mwaka 2020 ambapo umeonesha vifo vipya zaidi ya Elfu 40 na vifo Elfu 26,945 ikiongozwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi, tusipochukua tahadhari ugonjwa wa Saratani unaweza kufikia vifo Mil. Moja ifikapo Mwaka 2050
Akiendelea kufaganua kuhusiana na magonjwa Yasiyoambukiza, amesema magonjwa hayo ikiwemo Saratani yanachangia kwa asilimia 33 ya vifo vyote nchini Tanzania.
“Kwa upande wa nchi yetu takwimu zinaonesha magonjwa hayo yameongezeka kwa mara Tano hadi Tisa zaidi kati ya miaka ya 80 ambapo asilimia Moja tu ya Watanzania walikua na tatizo la Kisukari na 5% walikua na tatizo la Shinikizo la juu la Damu na sasa Kisukari 9% na Shinikizo la Damu 25%”. Amesema Waziri Ummy
Ili kupunguza tatizo la magonjwa Yasiyoambukiza, Waziri Ummy amewataka Watanzania kupunguza matumizi ya pombe kwa kuwa imekuwa sababu ya kuongezeka kwa magonjwa hayo nchini.
“Takwimu za mwaka 2023 zinaonesha ongezeko la matumizi ya pombe hadi kufikia matumizi ya wastani wa lita 10.4 kwa mwaka kwa watu wote wenye umri zaidi ya miaka 15 ambapo zinaiweka Tanzania kuwa nchi ya Tatu kwa matumizi ya Pombe”. Amesema Waziri Ummy
Mwisho, Waziri Ummy amesema takwimu za Ugonjwa wa Afya ya Akili zinaonesha kuwa wastani wa mtu Mmoja kati ya watu Wanne Duniani hupata maradhi ya Afya ya Akili kwenye maisha ambayo pia huchangia 21% ya ulemavu kwa mwaka.

#SickleCell in #Tanzania
Thank you for supporting #SickleCell
XXX
Tanzania na #SikoSeli
Asante kwa kutambua umuhimu wa #SikoSeli
@wizara_afyatz
@muhimbiliuniver
@sicklecellmuhas
#SickleCell #WorldSickleCellDay
#SikoSeli #SikuYaSikoSeliDuniani
“Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Tsh: Bilion 5 kwaajili ya huduma za ubingwa bobezi ikiwemo huduma za upandikizwaji wa uloto ambapo kwa awamu ya kwanza kwa mwaka huu watoto wenye ugonjwa wa Sikoseli 20 watapandikziwa Uloto bila malipo”. @ummymwalimu

*Siku ya Sikoseli Duniani // 19 Juni 2023*
Ugonjwa wa seli mundu ni ugonjwa wa kijenetiki wa damu unaoathiri mamilioni ya watu duniani kote, na kusababisha maumivu na magumu mengi kwenye maisha. Tueneze Elimu, Upendo, na Matumaini.
@pharmadawaa
#Sikoseli
#seliMundu

Gabo Zigamba ni mgeni rasmi leo.
Asante sana kwa kuwa balozi wa Siko Seli
@GaboZigamba_
@muhimbiliuniver
#boneandbloodfoundation
#sikoseli

Tanzania na Siko Seli
Mkutano kati ya Wizara ya Afya na MUHAS (Chuo Kikuu cha Afya na Afya Shirikishi Muhimbili)
@bint_mfalme
@SickleInAfrica
@muhimbiliuniver
#sikoseli #sicklecell
TUNAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA SIKOSELI NCHINI - DKT. SHEKALAGHE
Na. WAF - Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe mapema leo amekutana na timu ya wawakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) wanaosimamia mradi wa Sikoseli nchini wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Appolinary Kamuhabwa.
Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara Jijini Dodoma Katibu Mkuu Dkt. Shekalaghe ameihakikishia timu hiyo juu ya kuendelea kuboresha Sekta ya Afya hususan katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa Sikoseli nchini.
“Juhudi zinaendelea kufanywa na Serikali na wadau mbalimbali katika huduma za kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Sikoseli zikiwemo tafiti za kisayansi, upatikanaji wa matibabu ya hali ya juu kwa wagonjwa wa Sikoseli kama ubadilishaji damu na upandikizaji uloto.” Amesema Dkt. Shekalaghe
Aidha, wamejadiliana ukubwa wa ugonjwa wa Sikoseli nchini ambapo Mkurugenzi wa Jumuia hiyo Bi. Arafa amesema kuwa, watoto 11,000 hadi 14,000 huzaliwa na ugonjwa wa Sikoseli kila mwaka na inakadiriwa kuna jumla ya wagonjwa ni 200,000 wa Sikoseli nchini Tanzania.
Vile vile, timu hiyo imesema kuwa takribani asilimia 12 hadi 20 ya Watanzania wana vinasaba vya Sikoseli ambao wanaweza kupata watoto wenye ugonjwa wa s
Sikoseli na kuongeza idadi ya wagonjwa wenye ugonjwa huo hapa nchini.
Timu hiyo iliyoongozwa na Prof. kamuhabwa ameambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Elimu na Matafiti Mkuu wa Mradi wa Sikoseli Prof. Emmanuel Balandya, Mkurugenzi wa Jumuiya ya wagonjwa wa Sikoseli Tanzania Bi. Arafa Saidi, Watafiti katika mradi wa Sikoseli Dkt. Irene Minja, Dkt. Siana Nkya na Lulu Chirande

Asanteni sana kwa salamu zenu baada ya #SikoSeli kuongelewa kwenye bajeti ya @wizara_afyatz
Mafanikio ya #Tanzania yametokana na kazi & juhudi za watu wengi kwa miaka mingi.
Asante kwa wote waliohusika
@SuluhuSamia
@ummymwalimu
@bmhdodoma
@muhimbiliuniversity @MuhimbiliTaifa

Heri ya Siku ya Mama kwa akina Mama wote wazuri duniani kote.
Tunawasheherekea Akina Mama walio na #sikoseli na wamama wenye watoto wanaoishi na #sikoseli.
Tunawapenda akina mama wote. ❤️
.
@sicklecellpatientstz #matukionamaishablog
.
https://t.co/ppSZD5kBJI

Asante sana kwa kuboresha huduma za Siko Seli Tanzania
@ummymwalimu
@wizara_afyatz
@elimuyaafya
19 Juni ni Siku ya Siko Seli Duniani
#sikoseli
#SickleCell
#Tanzania
Leo ni Siku ya Sikoseli Duniani.
Ili kupunguza uwezekano wa kupata watoto waliorithi vinasaba vya sikoseli, ni muhimu kwa watu hususani vijana ambao wanataka kuoana na au kupata watoto kufanya upimaji wa vinasaba vya sikoseli kabla ya kuingia kwenye mahusiano/ndoa.

Maadhimisho ya Siku ya Ugonjwa wa Siko Seli Zanzibari.
📍Hospitali ya Mnazi Mmoja
📆 17/06/2022.
"TAMBUA SIKO SELI, TUUNGANE KUIMARISHA HUDUMA"
#sikoseli #sikuyasikoseliduniani #tuzungumzieafya #hpuzanzibar

Je, ni salama kwa mgonjwa wa Seli Mundu kuchanjwa dhidi ya Maradhi makali ya Uviko 19?
Kuna Umuhimu gani wa kupata CHANJO?
Jichanue Sasa na ufanye Maamuzi sahihi.
#SeliMundu #Uviko19 #Uviko #SikoSeli #Korona #Chanjo #ChanjoYaKorona #ChanjoYaUviko19 #SickleCell #SicklecellDisease
sheria na sera rafiki kwa upande wa mashujaa mfano elimu,afya na ajira!
Lakin pia kama wawakilishi wa matatizo yote ya wananchi wanatakiwa kujua sikoseli ni tatizo na liwe addressed properly.

#SikoSeli #Tanzania #mwanza
Pongezi @tasiwa_
XXX
#SickleCell in #Tanzania
@tasiwa_
#TanzaniaSickleCellWarriors
Towards #WorldSickleCellDay 19th June
Kuelekea siku ya sikoseli duniani, (june 19) TASIWA yapata nafasi ya “kuangazia sikoseli” katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania. #ijuesikoseli #tasiwa #WSCD2021 #bungelajmt #wizarayaafya #angaziasikoseli #shinelightonsicklecell

Mama zetu hawakutukatia tamaa na wala hawakuchoka kupambana na changamoto zetu za #sikoseli
Sisi ni mashujaa, Mama ni zaidi ya Shujaa
HAPPY MOTHERS DAY TO ALL STRONG MOTHERS RAISING BRAVE SICKLE CELL WARRIORS!
#mothersday #tasiwa #sicklecellawareness #ijuesikoseli

Currently, tukiwa tunafikia kilele cha mwezi wa uelewa wa sickle cell at Dodoma,
Nikiwa kama moderator #ijuesicklecel
#knowyourStatus #vunjamduarawaSicklecell

Currently, tukiwa tunafikia kilele cha mwezi wa uelewa wa sickle cell at Dodoma,
Nikiwa kama moderator #ijuesicklecel
#knowyourStatus #vunjamduarawaSicklecell

#Tanzania inatoa #elimu ya #afya kuhusu #SikoSeli kupitia @wizara_afyatz
#ElimuyaAfyakwaUmma
XXX
#Health #Education for #SickleCell in #Tanzania from Ministry of Health
@SickleInAfrica @elimuyaafya @wizara_afyatz @muhimbiliuniver
#SickleCellAwarenessMonth
#JIFUNZEAFYA
Mwezi Septemba kila mwaka ni mwezi wa kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa Sikoseli (Sickle Cell awareness Month).

Trends for you
Most Popular Users

Elon Musk 
@elonmusk
241.5M followers

Barack Obama 
@barackobama
118.8M followers

Cristiano Ronaldo 
@cristiano
114.5M followers

Donald J. Trump 
@realdonaldtrump
111.8M followers

Narendra Modi 
@narendramodi
107.1M followers

Rihanna 
@rihanna
98.7M followers

NASA 
@nasa
92.3M followers

Justin Bieber 
@justinbieber
91.8M followers

KATY PERRY 
@katyperry
90M followers

Taylor Swift 
@taylorswift13
84M followers

Lady Gaga 
@ladygaga
75.5M followers

Virat Kohli 
@imvkohli
73.5M followers

Kim Kardashian 
@kimkardashian
70.9M followers

YouTube 
@youtube
68.8M followers

Neymar Jr 
@neymarjr
66.5M followers

Bill Gates 
@billgates
65.3M followers

Selena Gomez 
@selenagomez
63.1M followers

The Ellen Show
@theellenshow
62.2M followers

CNN 
@cnn
61.7M followers

X 
@x
60.7M followers



























