Top Tweets for #urusi
MOSCOW, URUSI:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania, #Samia Suluhu Hassan, amewahakikishia wawekezaji wa #Urusi kuwa Tanzania ni eneo salama kwa uwekezaji kutokana na amani na utulivu, mazingira wezeshi ya biashara, miundombinu bora na ukuaji imara wa uchumi.
Samia amesema Tanzania inatoa fursa ya kufikia soko la zaidi ya watu milioni 500 katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, huku sekta za madini, kilimo, nishati safi, mafuta na gesi, afya na usafirishaji zikiwa miongoni mwa maeneo ya kipaumbele kwa uwekezaji.
Rais Samia ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kitaifa nchini Urusi, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin, jijini Moscow.
#SautiyaAfrika

#URUSI: PUTIN KUHUTUBIA KONGAMANO LA UCHUMI LA ST. PETERSBURG CHINI YA HOFU YA USALAMA
Rais Vladimir Putin anatarajiwa kutoa hotuba katika Kongamano la Uchumi la St. Petersburg, jukwaa linalokusanya wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali duniani, huku kivuli cha hofu ya usalama kikitanda baada ya mashambulizi ya droni ya Ukraine wiki hii.
Ikulu ya Kremlin imesisitiza kuwa ratiba ya Putin haijabadilika licha ya mashambulizi hayo yaliyolenga mji wa kaskazini magharibi mwa Urusi siku ya Jumatano.
Hatua hiyo inaashiria msimamo wa serikali kuendelea na shughuli za kifahari za kiuchumi hata wakati taifa linakabiliwa na changamoto za vita.
Kongamano hilo linajiri wakati uchumi wa Urusi unakumbwa na mdororo mkubwa: kupanda kwa bei za bidhaa, ongezeko la kodi, kufungwa kwa biashara na kupungua kwa nafasi za ajira.
Hali hii imeweka shinikizo kwa Kremlin kuonyesha uthabiti na kuendeleza ushawishi wake wa kiuchumi mbele ya washiriki wa kimataifa.

#URUSI: URUSI YAHAKIKISHIA CHINA UPATIKANAJI WA NISHATI
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema taifa lake litaendelea kusambaza nishati kwa China, akisisitiza kuwa ushirikiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili umejengeka kwa misingi thabiti na hauyumbishwi na shinikizo la nje au misukosuko ya masoko ya dunia.
Akizungumza baada ya hotuba ya Rais wa China, Putin alibainisha kuwa Moscow na Beijing zimejizatiti kuendeleza sera huru za mambo ya nje na kuimarisha nafasi zao katika kudumisha utulivu wa kimataifa.
Kauli hiyo inakuja wakati ambapo ushirikiano wa kiuchumi kati ya Urusi na China unaendelea kupanuka, hususan katika sekta ya nishati, na kuashiria dhamira ya pande zote mbili kulinda maslahi ya muda mrefu licha ya changamoto za kisiasa na kiuchumi duniani.

YAJAYO katika taarifa zetu za leo.
#Urusi yaahidi kutosajili raia wa #Kenya kuwa wanajeshi katika vita ya Ukraine.
Ishara zinaonyesha Rais wa Congo-Brazaville Dennis Sassou #Nguesso atasalia madarakani.
#Tanzania kumbukizi ya sera ya John Pombe Magufuli miaka mitano baada ya kufariki dunia.
Haya na mengine mengi usikose kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii na Radio Washirika hapo ulipo.
Most Popular Users

Elon Musk 
@elonmusk
240.4M followers

Barack Obama 
@barackobama
119.3M followers

Donald J. Trump 
@realdonaldtrump
111.7M followers

Cristiano Ronaldo 
@cristiano
110.2M followers

Narendra Modi 
@narendramodi
107M followers

Rihanna 
@rihanna
97.6M followers

NASA 
@nasa
92.1M followers

Justin Bieber 
@justinbieber
90.8M followers

KATY PERRY 
@katyperry
87.4M followers

Taylor Swift 
@taylorswift13
81.3M followers

Lady Gaga 
@ladygaga
72.8M followers

Kim Kardashian 
@kimkardashian
69.7M followers

Virat Kohli 
@imvkohli
69.5M followers

YouTube 
@youtube
68.7M followers

Bill Gates 
@billgates
63.7M followers

The Ellen Show
@theellenshow
62.5M followers

Neymar Jr 
@neymarjr
62.2M followers

CNN 
@cnn
61.9M followers

X 
@x
60.8M followers

Selena Gomez 
@selenagomez
60.5M followers

















