Mnaua watu kwa maelfu, Mnateka watu na kuwapoteza. Mnaiba uchaguzi kwa nguvu..
Alafu mnasema kuna watu wanawaonea wivu kwasababu ya rasimali!!!!
Hivi mnawaona Watanzania ni wajinga?
Kwamba Mataifa ya nje ndio yaliwatuma kuiba uchaguzi ambao hamjashinda!!!!
Watu sio sisimizi mmeua lazima muwajibike.
Amid major concerns in #Tanzania, leaders from @SFRCdems have warned of the 'least competitive election since the country embraced multi-party politics.' Abductions, disappearances, deaths and widespread intimidation have combined to create an impending disaster. #FreeTunduLissu
Wazanzibar kibao wanafanya biashara huku bara wengine wameoa na kujenga huku! Sisi kufanya kazi hotels tu hawataki, Ninani ananufaika na muungano nanani anapunjwa kwa maoni yako?
Watanganyika mmefikiwa. Kila kona mmebanwa huku wamejaa Kunduchi, Ikulu, Bungeni, Jeshini, Polisi, Usalama. Hawa watu ni wa kuwarudisha makwao. Hawana faida Tangayika.
Wazanzibari wametangaza vita na Watanganyika. Ni wa Kufukuza warudi makwao wakale Papa na Urojo
Wazanzibari wanatuua, wanatutawala
Wanatubagua, Wanahodhi ardhi kila sehemu, Wanakula vya kwetu. Lakini kwao hatuwezi kununua ardhi, hatuwezi kuishi bila vibali na hatuwezi kutibiwa.
Hawa Makenge warudi kwao. Tutagawana mbao sio muda
Huyu Saada Mkuya Salum amekua mbunge na waziri wa fedha huku bara..
Maneno muhimu kutoka kwako:
Unaelekeza mtu akienda hospital akitoa kitambulisho cha Taifa asitibiwe mpaka atoe cha Mzanzibari!!!! Ni mtu gani anaweza kuwa na kitambulisho cha Mtanzania lakini hana cha Mzanzibari?
Bila shaka ni mtu kutoka Tanganyika.
Umesema hatuna uwezo wa kutibu watu milioni 60 ambayo hiyo ni idadi ya Watanzania ambao wengi ni Watanganyika.
Je kuna siku wote wamevuka kuja kutafuta matibabu huko?
1. Saada unaweza kuwambia watu deni la Taifa ambalo kila mwezi tunalipa karibia trilioni moja na kadhaa ni kiasi gani kinatoka kwenye makusanyo ya Zanzibar?
2. Serikali za mitaa sio suala la muungano kwa katiba yetu,
Je unajua kuna wakurugenzi wa halmashauri za miji na majiji wameteueliwa kutoka Zanzibar huku Tanganyika?
Unajua kuna MADC wengi tu wameteueliwa kutoka Zanzibar wako huku bara?
Umefuatilia kwenye idara za madini, utaliii na wizara nyingi ambazo sio za Muungano kuna wakuu wa idara wangapi, wakurugenzi wa idara na maafisa wangapi kutoka Zanzibar?
Unataka Watanganyika wanaoishi huko wabaguliwe na wasipewe matibabu kwasababu ya kukosa kitambulisho cha Mzanzibari hata kama ana matibabu kadi ambayo ni sawa na bima ya afya….
Je Wazanzibari wanaoishi huku Tanganyika na wana bima za afya za NHIF nao wanyimwe matibabu?
Huyu ni waziri wa pili ndani ya mda mfupi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya Watanzania wengine na hakuna kauli yet kutoka kwa aliewateua… Kwahiyo huu ndio msimamo wa ccm na ndio msimamo wa wateuzi wao.
Nani anaewatuma hawa kusema haya? Maana sio bahati mbaya… nani anaewatuma kuwabagua Watanganyika?
TANZANIA INAWEZA KUJIFUNZA NINI KUTOKA SINGAPORE?
Anaandika Rev. Peter Msigwa
Ujio wa Rais wa Singapore nchini Tanzania ni fursa nzuri ya kutafakari. Si kwa sababu Singapore ni nchi kubwa kuliko Tanzania. Si kwa sababu ina rasilimali nyingi kuliko Tanzania. Wala si kwa sababu ina watu wengi kuliko Tanzania.
Kwa kweli, Singapore ina eneo dogo sana na haina utajiri mkubwa wa madini, gesi, ardhi wala maji kama tulivyo navyo sisi.
Lakini leo Singapore ni miongoni mwa nchi tajiri, zenye utawala bora, huduma bora za umma na uchumi imara duniani.
Kwa nini?
Jibu si rasilimali.
Jibu ni uongozi, mifumo na usimamizi.
Baada ya kupata heshima ya kulitumikia taifa letu kama Mbunge na nipata nafasi ya kutembelea Singapore na kamati ya kilimo, na pia nimepata nafasi ya kutembelea maeneo mengi ya Tanzania. Nyakati mbalimbali.
Nimeona uzuri wa nchi yetu.
Kutoka Kusini mpaka Kaskazini.
Kutoka Mashariki mpaka Magharibi.
Tanzania ni nchi nzuri sana.
Lakini kadiri ninavyotembea, ndivyo ninavyozidi kuamini kwamba tatizo letu kubwa si ukosefu wa rasilimali.
Tatizo letu kubwa ni usimamizi mbaya wa rasilimali tulizonazo.
Nchi yetu mara nyingi haithamini wala kutuza uwezo, maarifa, ubunifu, weledi na uaminifu.
Badala yake, mara nyingi mfumo huwapa nafasi wale wanaojua kujipendekeza kuliko wale wanaojua kufanya kazi.
Matokeo yake ni kwamba watu wengi wenye uwezo mkubwa hukata tamaa.
Ubunifu hufa. Motisha hupungua.
Vipaji huzimika.
Kwa sababu katika mazingira mengi ya utumishi wa umma, kufanya kazi kwa bidii hakulipi kama ambavyo unafiki na kujipendekeza vinavyolipa.
Tanzania inaweza kujifunza mambo matatu muhimu kutoka Singapore:
1. MERIT (SIFA NA UWEZO)
Singapore iliamua kwamba nafasi za umma zitolewe kwa watu wenye uwezo, si kwa watu wenye mahusiano.
Taifa haliwezi kujengwa kwa ukabila.
Taifa haliwezi kujengwa kwa upendeleo.
Taifa haliwezi kujengwa kwa nepotism.
Taifa haliwezi kujengwa kwa kuangalia dini, chama au urafiki.
Lazima tujenge mfumo unaosema:
“Mtu bora zaidi apewe nafasi, bila kujali anatoka wapi.”
Wakati nchi inawachagua watu wasio bora kuongoza taasisi zake, gharama hulipwa na wananchi.
2. PRAGMATISM (KUTANGULIZA MATOKEO KULIKO ITIKADI)
Kiongozi wa zamani wa Singapore, Lee Kuan Yew, aliongozwa na falsafa rahisi:
“Haijalishi paka ni mweusi au mweupe, muhimu ni kwamba anakamata panya.”
Tanzania inahitaji kujifunza falsafa hiyo.
Mawazo mazuri yasichunguzwe kwanza yametoka chama gani.
Yasichunguzwe kwanza yametoka dini gani.
Yasichunguzwe kwanza yametoka kwa rafiki au mpinzani.
Kinachopaswa kuulizwa ni:
“Je, wazo hili lina manufaa kwa taifa?”
Nchi zinazofanikiwa hukusanya mawazo bora kutoka kila upande.
Nchi zinazoshindwa hubaki zikitetea makosa kwa sababu tu yametoka upande wao.
3. HONESTY (UAMINIFU NA UKWELI)
Hakuna taifa linaloweza kuendelea bila uaminifu.
Hakuna taasisi inayoweza kuwa imara bila ukweli.
Hakuna uchumi unaoweza kukua kwa misingi ya uongo.
Tunahitaji watumishi wa umma wenye ujasiri wa kusema ukweli.
Tunahitaji viongozi wanaopenda ukweli kuliko sifa.
Tunahitaji mfumo unaolinda waaminifu badala ya kuwaadhibu.
Tunahitaji kuacha:
Unafiki Kujipendekeza, Uoga ,Uongo
Kwa sababu maendeleo ya kweli hayawezi kujengwa juu ya msingi wa hofu.
Tanzania si nchi maskini.
Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa ambao bado haujasimamiwa vizuri.
Tuna ardhi. Tuna madini. Tuna gesi Tuna maji. Tuna watu.Tuna vipaji.
Lakini bado mamilioni ya wananchi wanaishi katika umaskini.
Ndiyo maana maneno ya Bob Marley yanaonekana kuwa ya kweli hata leo:
“In the abundance of water, a fool is thirsty.”
Kwa maneno mengine:
Unaweza kuwa umezungukwa na utajiri mkubwa lakini bado ukaendelea kuwa maskini kwa sababu ya usimamizi mbaya.
Singapore ilitufundisha kwamba utajiri wa taifa hauanzi ardhini.
Unaanzia katika ubora wa mifumo. Unaanzia katika uaminifu wa viongozi. Unaanzia katika kuthamini uwezo. Unaanzia katika kuwajibika.
Siku tukiweka MERIT, PRAGMATISM na HONESTY mbele ya siasa, mbele ya upendeleo na mbele ya propaganda. Tunaendelea
Kweli mipango ya Mungu ni siri kubwa. Fikiria huyu ndiye angekuwa Makamu Mkiti wa Chadema chini ya Mbowe.
Ni maridhiano gani anayotaka kufanya na vyama?
Waathirika wa 29.10.2025 na hali ya siasa nchini ni WANANCHI.
Anataka kukataa kwamba wananchi walio wengi wako na Chadema?
Ingekuwa ni kutoa tuzo
1. Best politician- Lissu
2. People’s president- Lissu
3. Best lawyer-Lissu
4. Best Orator- Lissu
4. Best public speaker- Lissu
Simply best
Kata ya Idukilo wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga. Iko jirani na Maganzo Magharibi ya Mwigumbi.
Wananchi wamemkataa Diwani fake wa ccm aliejiweka madarakani 2025…
Tangu wakati huo wananchi hawamtaki.
RPC Shinyanga amepeleka Oparesheni hapo, mamia ya watu wamepigwa na kuumizwa wengine zaidi ya 150 wana kesi mahakani Kishapu..
Uonevu huu haukubaliki.
Nimeelekeza Mawakili wa chama waingilie kati na chama ngazi ya kanda wafanye mkutano Idukilo kuzungumza na wananchi.
RPC Shinyanga sio wajibu wako kisheria kulazimishia wananchi Kiongozi wasiemtaka ambae hawajamchagua.