Nchi yetu inafurahisha sana. Fikiria eti Serikali imewashtaki watu hawa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma kwa kusema " mauaji ya 29 Oktoba 2025 hayawezi kufichwa na tume ya Uchunguzi" hapa kosa lao ni nini? Hivi tume ilisema wale 518 walijiua?
Nitawatetea watu hawa.
Moja ya hoja ambayo Bunge la Marekani limeweka kwenye "bill" kabla ya kuwa sheria dhidi ya Tanzania, ni pamoja na hoja kuwa Serikali ya Tanzania inaminya uhuru wa kuabudu (dini).
Jana wabunge waliojipitisha bila uchaguzi wanasema hakuna uhuru wa kuabudu unaominywa nchini. Swali; hivi kanisa la Gwajima (Ufufuo na uzima) lilifungiwa kwa kosa gani?
Namshukuru Mungu sana, kesi ya Kaunya na wenzake imeisha leo rasmi ambapo Kaunya yuko huru sasa.
Asante sana mawakili wenzangu, Chama Taifa,Bavicha Taifa, Uongozi wa Kanda ya Serengeti, LHRC, wadau na wanachama wote kwa kujitoa kwenu kuhakikisha haki inatendeka.
Bye bye Bunda!!
Shekhe Mwaipopo na kundi lako la watu waliohama toka Chadema kwenda chama kingine achane hicho mnachofanya mara moja. Achaneni na mpango wenu wa hizo "Press" zenye nia ovu dhidi ya CHADEMA na Kiongozi wake.
Nawaonya.
Tangu udogo wangu nimekua shabiki mkubwa wa Arsenal. Ilipofika mwaka 2015 vipigo vilizidi nikamua ili nisipate "pressure" niliapa kutokuangalia mechi yoyote ya Arsenal mpaka siku itakapochukua ubingwa tena.
Hatimaye leo ile siku imefika. Hakika hii ilikuwa ni "the long wait"
We are the champion ๐
Katika Kanda yangu ya Magharibi inayojumuisha mkoa wa Tabora, Kigoma na Katavi (Chadema) kuna mtu ambaye anaishi Dar es Salaam lakini ni mzaliwa wa Ukumbisinganga-Kaliua mkoani Tabora (sitamtaja kwa jina leo)
Mtu huyo anafahamika kwa kwa kufanya "press" nyingi zinazoisifia serikali na kui"ponda" Chadema. Hata majuzi amefanya "Press" akimsema Makamu wa chama CDM John Heche, amepewa kandarasi ya kutafuta watu wajifanye ni viongozi wa CDM toka katika maeneo mbali mbali katika Kanda yangu kwa kuwapa pesa kidogo huku yeye amepewa pesa nyingi sana toka sehemu.
Lengo la kutafuta watu wao ambao watavalishwa nguo za chama cha CDM ni kufanya "Press" zitakazo kuwa na lengo la kuonyesha hawakubaliani na msimamo wa Kamati Kuu na Uongozi wa CDM Taifa wa sasa.
Nina taarifa kuwa leo kundi la kwanza la watu hao watafanya "Press" Tabora Mjini muda wowote kuanzia saa tano Asbh hii.
Wakati sahihi ukifika nitafanya "Press" juu ya suala kwa ushahidi. Kwa sasa nitoe tu rai kwa viongozi, wanachama wote CDM na wapenda Haki na demokrasia katika Kanda yetu waepuke kukichafua chama chetu ambacho ndio tegemeo la watanzania kwa sasa kwa nia ovu ya wanaowatafuta kufanya hivyo.
19/5/2026.
Tarehe 9/4/2025 Lissu alikamatwa Mbinga-Ruvuma na kushtakiwa kwa Uhaini. Siku hiyo hiyo yaani tarehe 9/4/2025 Said Issa na wenzake wakafungua kesi iliyopelekea chama kuzuiliwa kufanya shughuli zake.
Mwaka huu; tarehe 20/5/2026 Mahakama Kuu itatoa uamuzi wa pingamizi la CDM kwenye kesi ya akina Said Issa juu ya kama walileta kesi hiyo nje ya muda au la?. Cha kushangaza ni tarehe hiyo hiyo yaani 20/5/2026 Msajili wa Vyama Siasa ametaka CDM wapeleke majibu ya barua yake kabla ya saa tisa mchana ili aweze kufanya maamuzi juu ya suala hilo. Ambapo anaweza kuifungia CDM au kuilipisha faini kwa mujibu wa barua yake ilivyosema. Coincidences?
Viongozi wengi TZ ukiwakuta ofisini au wakiwa kwenye ma-V8 kabla hawajaanza kuongea au kujibu hoja za wananchi, utasema viongozi si ndio hawa sasa, ila wakianza kuongea au kujibu hoja ndio unagundua ulikosea ulivyofikiri mwanzo.
Haina tofauti na huyu jamaa hapa.