November 20 kila mwaka ni siku ya watoto Duniani, huadhimishwa na Umoja wa Mataifa lengo ni kuboresha haki za watoto na kuboresha ustawi kwa watoto wote Duniani.
Pia ndo siku ya mkataba wa Haki za watoto ulipitishwa mnamo mwaka 1989.
Mitambo yote tisa ya kuzalisha umeme katika Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) sasa inafanya kazi, ikiwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 kwa pamoja.
Hii itafanya Tanzania kuweza kuzalisha umeme wakujitosheleza.
#MamaYukoKazini
Leo Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya tano ya Kipindi cha Kwaresima, mwaka C wa Kiliturujia katika Kanisa. Kadiri ya utamaduni na mapokeo ya Kanisa, kuanzia Dominika hii Misalaba inafunikwa, mpaka Ijumaa Kuu wakati wa kuadhimisha mateso ya Kristo.Masomo ya dominika hii yanasisitiza juu ya upendo na huruma ya Mungu kwa wadhambi. Somo la kwanza ni la Kitabu cha Nabii Isaya Katika somo hili Mungu kwa upendo na huruma yake anaahidi kuwakomboa waisaraeli kutoka utumwani Babeli kama alivyowakomboa kutoka utumwani Misri. Somo la pili ni la Waraka wa Mtume Paulo kwa Wafilipi Katika somo hili mtume Paulo anatufundisha kuwa, tukiwa na imani juu ya nguvu ya mateso, kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, tutayaona mambo ya dunia hii si kitu, ni ya kupita tu.
Sehemu hii ya Injili inahusu simulizi la mwanamke aliyefumaniwa katika dhambi ya uzinzi. Iko hivi, kipindi hiki wayahudi walikuwa chini ya utawala wa kirumi na hawakuruhusiwa kutoa adhabu yoyote ya kifo. Hivyo Yesu angesema watekeleze sheria ya Musa, wampige huyu mwanamke kwa mawe mpaka kufa, yeye mwenyewe angekuwa na hatia ya kuuwawa kadiri ya sheria ya Serikali ya Kirumi. Lakini pia angepingana na mafundisho yake juu ya huruma, upendo na kutowahukumu wengine. Na angesema wasimuue, angepingana na sheria ya Musa. Na yeyote aliyepingana na sheria ya Musa alistahili adhabu ya kifo. Yesu kwa kufichua nia yao ovu anawaambia kuwa yule asiye na dhambi awe wa kwanza kumtupia jiwe. Hii haina maana kuwa Yesu hachukii dhambi, bali anawahurumia wakosefu ili wapate nafasi ya kutubu na kuacha dhambi.
Fundisho la pili ni hili, mbele za Mungu hakuna binadamu asiye na dhambi ndiyo maana wote waliondoka na hakuna aliyedhubutu kuwa wa kwanza kumrushia jiwe mwanamke mdhambi. Mungu haadhibu mara, bali anampa kila mtu nafasi ya kubadili mwenendo wake na kurudi katika njia ya kweli na haki. Mwanadamu mdhambi anaendelea kuishi kwa huruma na upendo wa Mungu na sio kwa mastahili yake. Mungu anaendelea kutupa nafasi ya kuishi hata kama tu wadhambi ili tutubu, tubadilike na kuomba msamaha naye daima anamsamehe kila anayekiri na kutubu makosa yake.
Tunaalikwa kufanya toba, tusamehewe na tusirudie kutenda dhambi tena kwa neema za Mungu. Tuweke nia thabiti ya kuanza maisha mapya, maisha yanayompendeza Mungu. Lakini zaidi sana tusiwahukumu wengine kwa dhambi zao bali tuwasiaidie kuachana na mazoea ya kutenda dhambi.
Fundisho la tatu ni hili, binadamu hana mamlaka ya kumhukumu mwingine kwa adhabu ya kifo maana uhai wa mwanadamu ni mali ya Mungu. Uhai ni zawadi na tunu pekee ambayo Mungu ametupatia sisi wanadamu, hivyo ni jukumu letu kuupokea, kuutunza na kuulinda. Thamani ya maisha yetu mbele za Mungu ni kubwa mno kwa kuwa tumeumbwa kwa sura na mfano wake.
Tunaalikwa Tukaze mwendo katika kuishi maisha ya kitakatifu, huku tukiitumainia huruma na neema za Mungu ili tubaki kuwa waaminifu katika kuziishi amri zake kwa ajili ya sifa na utukufu wake nasi tutakatifuzwe tuweze kuisherehekea sikukuu ya Pasaka kwa furaha na amani tukiwa tumeungana Kristo Mfufuka.
Tumsifu Yesu Kristu. 🙏
Nimefika Majiji yote matano Tanzania, ila Mwanza ni special sana na kama serikali wakiikomalia Mwanza zaidi basi itakuwa Kituo kikubwa sana kwa nchi za Maziwa Makuu.
Mwanasiasa, si kila mfanyabiashara ni jamaa yako. Toka madarakani uone. Mfanyabiashara, si kila mwanasiasa ni jamaa yako. Filisika uone. Mwanasiasa, si kila mwanasiasa jamaa yako. Pendwa na watu uone. Mfanyabiashara, si kila mfanyabiashara jamaa yako. Ingia biashara afanyayo uone