Jeshi la Polisi, mnawajibika kulinda raia na mali zao. Uhai wa raia unatakiwa kuwa kipaumbele kwenu cha kwanza. Lakini ninyi mnafanya kinyume chake. Inakwaza.
Edgar Edaon Mwakabela, @Sativa255 ametekwa tangu 23.06.2024. Tumeendesha kampeni hapa ya kumtafuta. Mlikuwa kimya hata tulipoamua kufuata njia zenu.
Tumefungua jalada kituo cha Polisi Gogoni - Kimara. KMR/RB/3239/2024, lakini, hamkutusaidia kumtafuta Edgar kwa sababu gani? Mliamua kupuuza?
Leo mnachapisha taarifa, @Sativa255 kuonekana katika pori la Katavi. Mmeshindwa kwa intelejensia yenu kufahamu siku 4 ndugu yetu yupo wapi?
Edgar analalamika ameteswa DSM, ARUSHA, KATAVI. Amechomwa na kitu chenye ncha kali. Umuhimu wa polisi upo wapi kama raua WANATEKWA?