@kigogo2014 Screen shot utume bcs najua allowance ulikua hujapokea Lowassa hajaangukia pua still alive ,ushajitafutia mradi wa 2030 tutakutana sitting room ambayo huwa tunakutana , mzee lazima tuwepo ili uishi huwa unanisaidia kujua Script writer wako toka March 2021 huwa nihifadhi kila
πTazengwa - Nzega
Kila nikiwa Nzega hapa ndio sehemu ambayo hunipa tumaini langu la kesho.
Niliwahi kuwapa story humu kuwa Mwaka 1993 nikiwa kidato cha 3 Marehemu Mzee MWANIKOLONGO aliniuzia ekari 6 na ndipo nililima shamba langu la kwanza la mpunga kwa mbegu nilizopewa na Marehemu Mzee Nduju na hapa ndipo nilijenga zizi langu la kwanza la MASANZU na kuweka Ngβombe za kwanza 6 za kufuga nilizonunua Mnada wa Ushirika nikiwa na kaka yangu Marehem Vumilia Ngβhwani.
Huyu ni MIMI na haya ni Maisha yangu ya kila siku nikiwa Nzega hapa lazima nifyeke nikiwa sipo Nzega lazima nipige simu kujua wameamka vipi.
Allah kamuelezea Ngβombe katika Qur-aan kaelezea ardhi na manufaa yake.
Jumaa Mubaraak
Surah An-Nahl (16:5-7)
βAnd the cattle He has created for you; in them is warmth and [numerous] benefits, and from them you eat.β
(Surah An-Nahl 16:5)
Surah Al-Muβminun (23:21)
βAnd indeed, for you in grazing livestock is a lesson. We give you drink from what is in their belliesβ¦β
Ya Allah Barik ππΎ
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. @SuluhuSamia , leo tarehe 21/09/2025 ameendelea na mikutano ya kampeni mkoani Ruvuma.
Akihutubia wananchi katika mkutano uliofanyika Mbinga Mjini, Dkt. Samia amesisitiza kuwa Mbinga imebeba historia kubwa , akibainisha kuwa Rais wa Awamu ya Nne, Hayati Benjamin William Mkapa, alipata elimu yake ya sekondari katika eneo hilo kati ya mwaka 1952β1955. Dkt Samia pia amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kuilaza roho yake mahali pema peponi. π
Aidha, Dkt Samia ameeleza kuwa Mbinga ni kitovu muhimu cha uzalishaji wa mazao ya kilimo, jambo linalochangia ustawi wa Taifa. Akiwa amerejea Mbinga baada ya ziara yake ya Septemba mwaka jana iliyolenga kuzindua miradi ya maendeleo, safari hii amesema amekuja kwa lengo la kuomba kura ili kuendeleza kazi kubwa iliyoanza katika miaka mitano iliyopita.
Kwa kujiamini na ujasiri mkubwa, Dkt. Samia amesema kuwa Miaka mitano iliyopita tumeweza, na miaka mitano ijayo, kwa uwezo wa Mungu, tutaweza zaidi.
#HaijapataKutokea #DiraYaSamia #KaziNaUtu2025 #SamiaHadi2030
HODI HODI RUVUMA! π
Wananchi wa Ruvuma, leo ni siku ya kihistoria! Karibuni kwa wingi kumpokea na kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia @ccm_tanzania , Mhe. Dkt. @SuluhuSamia ππ
Usikose kufuatilia hotuba yenye dira ya maendeleo, sera madhubuti na mipango thabiti itakayoendeleza ustawi, mafanikio na maisha bora kwa kila Mtanzania.
#HaijapataKutokea #DiraYaSamia #KaziNaUtu2025 #SamiaHadi2030
SAFARI YA USHINDI WA KISHINDO IMEFIKA TABORA MJINI! π
Leo ni zamu yetu wana Tabora Mjini kumpokea kwa shangwe na hamasa, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
@ccm_tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia. ππ
Wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia na kumsikiliza moja kwa moja akieleza sera, dira na mipango madhubuti ya maendeleo ya taifa letu.
#HaijapataKutokea #DiraYaSamia #KaziNaUtu2025 #SamiaHadi2030 β
TMA: MVUA ZA VULI 2025 KUISHA JANUARI 2026
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Mvua za vuli zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani katika maeneo mengi na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu.
@WizaraKilimo@UvuviNa@HusseinBashe
Kaka yangu @HusseinBashe kaweka ombi lake kisomi sana na kwa facts nyingi sana.
1.Ukubwa wa Mkoa wa Tabora
2.Idadi ya watu katika mkoa wa Tabora na katika eneo alilopendekeza liwe mkoa mpya.
3.Uwezo wa kujiendesha kwa mkoa mpya.
Kwa mimi kama mzaliwa na mkazi wa Igunga na Nzega
Nimpongeze kaka yangu @HusseinBashe katenda haki sana kwa kuomba tuwe na Campus ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam pale Lusu.
Hii itafungua uchumi wa ukanda wetu na pia kusogeza huduma za elimu ya juu karibu na watu wetu.
Hongera sana @HusseinBashe kwa uwakilishi huo
Katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Nzega Mjini, mgombea wa jimbo la Nzega, @HusseinBashe , ameeleza maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta ya maji katika miaka minne ya Dkt Samia akiwa madarani.
Ameeleza kwamba miaka mitano iliyopita, dumu moja la maji katika mji huo lilikuwa likinunuliwa kwa bei ya kati ya Tsh 500 hadi 1,000. Ili kupata maji ya kunywa, familia nyingi zililazimika kufuata vyanzo vya maji vilivyokuwa mbali, wakipanda zaidi ya kilomita 4 hadi 5.
Leo, shukrani kwa jitihada za serikali ya Dkt. @SuluhuSamia , kata zote 10, vijiji vyote 21, na vitongoji vyote 176 vina huduma ya maji safi na salama. Hii ni baraka kubwa kwa wananchi, hasa wale wanaoishi vijijini, kwani sasa wanaweza kupata maji kwa urahisi na bila gharama kubwa.
#HaijapataKutokea #DiraYaSamia #SamiaHadi2030 #KaziNaUtu2025 #NzegaYetuKeshoYetu
Chama Cha Mapinduzi kimejengwa juu ya imani ya watu wake. Wanachama na wapenzi wapo tayari kukipigania, kukisemea na kukitangaza pasipo kuchoka. π
Safari ya ushindi wa kishindo kuelekea Oktoba 29, 2025 imejaa nguvu na mshikamanisho wa kweli. β
@ccm_tanzania@SuluhuSamia
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. @SuluhuSamia, akiendelea na mikutano yake ya kampeni mkoani Singida, amewahutubia wananchi wa Wilaya ya Manyoni.
Katika hotuba yake, Mhe. Dkt. Samia amewakumbusha wananchi wa Manyoni kuhusu ziara yake ya Oktoba 2025 ambapo aliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya MkiwaβItigiβNoranga yenye urefu wa kilomita 25. Ameeleza kuwa ujenzi huo kwa sasa umefikia hatua nzuri na upo katika asilimia 75 ya utekelezaji.
Aidha, amewapa wananchi habari njema kwamba tayari mkandarasi amepatikana kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha barabara kinachoelekea Bukiwa chenye urefu wa kilomita 31. Ameongeza kuwa serikali imedhamiria kuendeleza barabara hiyo kuelekea Makongorosi, hatua ambayo itaongeza fursa za biashara na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Singida na Mbeya.
Mhe. Dkt. Samia amesisitiza kuwa ahadi hiyo ni sehemu ya dhamira ya serikali ya kuhakikisha miundombinu bora inafungua njia za maendeleo na ustawi wa wananchi wote.
#HaijapataKutokea #DiraYaSamia #KaziNaUtu2025 #SamiaHadi2030