KWAKUWA NI HALALI KWA WAZANZIBARI KULINDA HAKI ZA WAZANZIBARI HAIWEZI KUWA HARAMU KWA WATANGANYIKA KULINDA HAKI ZA WATANGANYIKA.
Kwa yanayoendelea kujitokeza katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu kujitanabaisha kwa misingi ya Uzanzibari na kulinda maslahi ya Zanzibar, je, si wakati sasa kwa Watanganyika nao kuzungumza kwa uwazi, kuhoji kwa uhalali na kujadili kwa kina masuala yanayohusu haki, hadhi na maslahi ya Tanganyika?
Je, Watanganyika hawana haki ya kuhoji na kulinda:
1. Bandari zilizopo ndani ya Tanganyika.
2. Misitu na rasilimali za mazingira za Tanganyika.
3. Rasilimali za asili zilizopo katika eneo la Tanganyika.
4. Hadhi, haki na umiliki wa ardhi ya Tanganyika.
5. Nafasi, haki na uwepo wa watu wasio Watanganyika katika idara na taasisi ambazo si za Muungano.
6. Uhalali wa viongozi wasio Watanganyika kuingia au kusaini mikataba inayohusu rasilimali za Tanganyika, hususan pale ambapo baadhi ya masuala hayo tayari yameondolewa katika eneo la Muungano kwa upande wa Zanzibar.
7.Kuhoji mchango wa Zanzibar katika kugharimia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano na Ulipwaji wa Deni la Taifa.
Ikiwa ni halali kwa Wazanzibari kujadili, kuhoji na kulinda maslahi ya Zanzibar kwa misingi ya utambulisho wao wa kisiasa na kikatiba, kwa mantiki hiyo hiyo haipaswi kuwa kosa kwa Watanganyika kuhoji, kujadili na kutetea maslahi ya Tanganyika.
Katika mfumo wowote wa haki, usawa na kuheshimiana ndani ya Muungano, haki ya kulinda maslahi ya Zanzibar haiwezi kutenganishwa na haki ya Watanganyika kulinda maslahi ya Tanganyika.
Haki hizo zinapaswa kutambuliwa kwa usawa, bila upendeleo na bila kuonekana kuwa ni tishio kwa Muungano, bali kama sehemu ya kujenga Muungano wenye misingi ya haki, uwazi na kuheshimiana.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI ndiyo Msingi bora wa kuliongoza Taifa kutoka katika vitendo vya Ukatili dhidi ya ubinadamu,ukiukwaji wa Haki za Raia na,Mauwaji na Utekaji vilivyofanyika kanla,wakati na Baada ya Tarehe 29 Oktoba 2026.
BAK MWABUKUSI.
💨Kwa nini ununue Mic za DJI Mic 2?
Hizi hapa ndo sifa za mic za DJI Mic 2 ambazo zimeshika soko la dunia kwa sasa.
🎤 Audio
Omnidirectional microphone (hukusanya sauti kutoka pande zote)
48kHz / 24-bit audio recording