ليس كل محتاج يمد يده طالبًا للمساعدة؛ فبعض الناس تحفظهم ك��امتهم من السؤال، وتخفي وجوههم المبتسمة أوجاعًا لا يعلمها إلا الله
Sio kila mwenye uhitaji hunyoosha mkono wake kuomba msaada; baadhi ya watu heshima yao inawazuia kuomba, na nyuso zao zenye tabasamu huficha maumivu ambayo hakuna ayajuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu.
• Tuangalie hali za watu wanaotuzunguka, kwani huenda miongoni mwetu kuna mtu aliyelemewa na madeni, au maisha yamemwia magumu, au anasubiri mkono wa msaada umfikie wakati ambapo hawezi kuomba msaada.
• Yeyote anayeweza kumuondolea mtu dhiki, asisite kufanya hivyo; kwani thawabu ni kubwa, dunia ni yenye kupita, na yale yaliyoko kwa Allah ni bora zaidi na yenye kudumu.
• Msicheleweshe kufanya mambo ya kheri, kwani huenda furaha yenu duniani na Akhera ikawa ipo katika dhiki mliyoiondoa kwa mwanadamu.
��بل أن ترسم ثقتك على جدار شخص، تأكد من صلابة الجدار لكي لا يسقط عليك
Kabla hujaanza kuuchora uaminifu wako kwenye ukuta wa mtu, hakikisha kwanza ukuta huo ni imara ili usikuangukie.
من الضروري أن تبقى للإنسان مساحة لا يستعين فيها بالآلة: أن يقرأ ويفكر ويكتب ويحاول ويخطئ. فبعض القدرات لا تنمو إلا بالممارسة، ولا يصح أن نتنازل عنها لمجرد أن هناك أداة تؤدي المهمة بسرعة أكبر
Ni muhimu kwa mwanadamu kubakisha nafasi fulani ambayo hatumii mashine kumsaidia; nafasi ya kusoma, kufikiri, kuandika, kujaribu na kukosea. Kwa sababu baadhi ya uwezo wa mwanadamu haukui isipokuwa kwa kufanya mazoezi. Sio sahihi kuuacha uwezo huo kwa sababu tu kuna chombo kinachoweza kufanya kazi hiyo kwa haraka zaidi.
أحياناً لا يضرك إلا ثقتك الزائدة بمن لا يستحق
Wakati mwingine hakuna kinachoweza kukuumiza zaidi ya kumwamini kupita kiasi mtu ambaye hastahili kuaminiwa.
من أجمل ما يمكن أن يقدمه الوالدان لأبنائهما أن ينشؤوهم على محبة الصلاة، لا على أدائها خوفًا من العقاب فقط
Miongoni mwa mambo mazuri zaidi ambayo wazazi wanaweza kuwapa watoto wao ni kuwalea katika kuipenda Swala, sio kuwazoesha kuiswali kwa kuogopa adhabu tu.
ومِن الناس مَن يراك كالطبيب. يَأتيك وقت الحاجة، ثم يوَدِّعك متمنّياً ألا يَراك
Miongoni mwa watu kuna wale wanaokuona kama daktari; wanakujia wanapokuwa na uhitaji, kisha wanakuaga huku wakitamani wasikuone tena.
شكر نعمة الصحة يكون بحفظها، وشكر نعمة المال يكون بحسن إنفاقه، وشكر نعمة الأمان يكون بعدم الإضرار بالآخرين، وشكر نعمة الأسرة يكون بحسن رعايتها
Kushukuru neema ya afya ni kwa kuilinda, na kushukuru neema ya mali ni kwa kuitumia vizuri, na kushukuru neema ya amani ni kwa kutowadhuru wengine, na kushukuru neema ya familia ni kwa kuitunza na kuisimamia vyema.
أربح التجارة ذِكْر الله، وأخسر التجارة ذِكْر الناس
Biashara yenye faida zaidi ni kumtaja Allah, na biashara yenye hasara zaidi ni kuwataja watu (kwa kuwasengenya).
Nabii Isa (a.s.) Yesu alifundisha:
“Enyi wanadamu, msiifunge mioyo yenu kwenye dunia hii ya kupita. Dunia haitadumu kwa ajili yenu, wala ninyi hamtadumu ndani yake. Dunia humdanganya anayeitegemea na kumuangamiza anayeipenda kupita kiasi. Rejeeni kwa Muumba wenu na mcheni Mola wenu.”
من عجائب النفس البشرية أنها قد تألف النعم حتى لا تعود تراها. نعتاد وجود الوالدين، والصحة، والأمان، والأصدقاء الصادقين، ثم لا ندرك قيمتها إلا حين نفقد شيئًا منها
Miongoni mwa maajabu ya nafsi ya binadamu ni kwamba inaweza kuzoea neema hadi isiweze kuziona tena. Tunazoea uwepo wa wazazi, afya, amani, na marafiki wa kweli, kisha hatutambui thamani yake hadi pale tunapopoteza kimoja wapo.
أحياناً يكسرك من تحب، ويجبرك غريب
Wakati mwingine yule unayempenda ndiye anayekuumiza na kukuvunja moyo. Na yule usiyemjua (mgeni) ndiye anayekufariji.
Hamtotanguliza kheri isipokuwa mtaikuta kwa Allaah
Basi changia ujenzi wa marqaz hii ya Ahmad ibn hanbal
Watu wa kilosa mtendeni b wapate pakusemea Haq
Pakufundushia Haq na pakumuabudia Allaah kwa Haq
Mahtaji yetu ni mengi hivyo hatudharau hata jero
No ya kuchangia
0769141414
لا تخشَ أن تسير ببطء، بل اخشَ أن تتوقف عن السير. ليست العبرة في أن تصل قبل الآخرين، بل أن تواصل التقدم مهما طال الطريق.
✍️ Usiogope kutembea polepole, bali ogopa kuacha kutembea kabisa.
✍️ Jambo la msingi sio kufika kabla ya wengine, bali kuendelea kusonga mbele bila kukata tamaa, hata kama safari ni ndefu kiasi gani.
من أخطر آثار المعصية أن يضعف إنكار القلب لها، حتى يصبح ما كان يستحيي منه الإنسان بالأمس أمرًا عاديًّا في حياته اليوم
Miongoni mwa athari hatari zaidi za kufanya maasi ni kudhoofika kwa moyo katika kuyachukia maasi hayo, mpaka jambo ambalo mtu alikuwa akilionea haya jana linakuwa jambo la kawaida kwenye maisha yake ya leo.
أن تجد من تحب شيء جميل، أن تجد من يحبك حدث عظيم
Kumpata mtu unayempenda ni jambo zuri, lakini kumpata mtu anayekupenda wewe ni jambo kubwa sana. (Kwa sababu sio kila unayempenda atakupenda pia)