Msemaji wa Yanga Ally Kamwe amesema wanamajasusi kwenye timu pinzani 😎
“Tunawatu wapo kwenye pitch kuna watu wapo ofisini na Kuna majasusi wetu wanavaa jezi za timu nyingine, wanacheza hizo timu nyingine ndio majasusi ambao Yanga tupo nao.”
Chambua 😎
Diarra kafanya Saves 5 dhidi ya JS Kabylie, kiwango chake cha leo unaweza kumpa sifa kwa maneno haya.
“Wewe ndiye mstari wa mwisho wa ulinzi, lakini pia mstari wa kwanza wa matumaini. Kila mpira unaookoa ni ushindi, bila kujali matokeo ya mchezo!”
FT: JSK 0-0 Yanga SC
MATOKEO LIGI KUU RAUNDI YA 4.
🛑 Pamba Jiji 2-1 Mashujaa
🛑 Fountain Gate 1-0 Dodoma Jiji
Fountain Gate na Pamba jiji zimeshinda kwa mara ya kwanza kwenye michezo ya Ligi kuu msimu huu.
Pamba jiji imefikisha alama 5, wapo nafasi 4. Fountain Gate wana alama 3 nafasi ya 15.
TAKWIMU LIGI KUU 25/26
•Imechezwa michezo 21
•Yamefungwa mabao 36
•Timu zilizoshinda michezo yao yote ni,
1. Simba SC ✅
2. Singida BS ✅
•Fountaine Gate ndo timu pekee ambayo haina alama hata moja. ❌
🛑Ligi imesimama itarudi tena Oktoba 17,kwa michezo ya raundi ya 4
Majina 6 makubwa ya Wachezaji walioachwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa leo OCT 01, 2025.
1. Samatta. 2. Msuva
3. Kibu Denis 4. Mudathiri
4. Zimbwe Jr 5. Kapombe
6. Idd Nado
Tanzania itacheza dhidi ya Zambia mchezo wa kufuzu kombe la Dunia.
Kwenye michezo 5 ya mwisho Simba dhidi ya Yanga,
•Yanga kashinda Mechi zote 5
•Yanga kafunga mabao 11
•Simba kafunga mabao 2
⛔️Kwa mujibu wa takwimu hizi Simba kesho anaingia kwenye mchezo akiwa ni Underdog. 😎
Dakika 45’ kwenye nafasi za wazi za kufunga ilikuwa ni Yanga dhidi ya golikipa wa JKT Yakubu Suleiman. Yanga wamefanikiwa kui-beat defense ya JKT Tanzania kipa kipa tu Yakubu alikuwa kikwazo wananchi wameikamata game pande zote.
HT: Yanga SC 1-0 JKT Tanzania
Mgawanyo wa makombe Uingereza msimu huu 2024-25.
🏆Ngao ya Jamii- Manchester City
🏆 Ligi Kuu EPL - Liverpool
🏆 Carabao Cup - Newcastle United
🏆 FA Cup - Crystal Palace
VIPORO VIMELIWA🦁
🛑Mechi 4 ndani ya Siku 11 Simba SC kashinda zote kafunga bao 10 kafungwa bao 3.
🛑Ushindi wa simba dhidi ya KMC unawafanya wafikishe michezo 20 mfululizo waliyocheza bila kufungwa. Mara ya mwisho Simba kifungwa ilikuwa Oktoba 19, 2024.
FT: KMC 1-2 Simba SC
Kukosa magoli ni moja kati ya sifa ya washambuliaji wa Simba SC msimu huu. Mpaka sasa wakiwa mapunziko dhidi ya KMC tayari wamefunga mabao 61 kwenye michezo ya Ligi.
⛔️kama wangekuwa wanatumia nafasi vizuri Simba wangekuwa na bao hata 100 za Ligi 😀😀
HT: KMC 1-1 Simba SC
Ni vyema Serikali kupitia vyombo vyake waliangalie hili jambo la tuhumu za rushwa/ upangaji matokeo kwenye mpira wetu. watu wanaongea wazi wazi tena bila uoga.
⛔️Nadhani vyombo vya usalama waanzena na hawa mashujaa wanotuhumu hadharani wanaweza kutupa ukweli wanaoujua.
Mikataba ya udhamini wa Jezi Simba SC 2021 - 2025.
1. 2021 Simba mkataba na Vunja bei Bilioni 1 kwa mwaka mkataba wa miaka 2.
2. 2023 Simba mkataba na Sandaland Bilioni 2 kwa mwaka mkataba wa miaka 2.
3. 2025 Simba mkataba na Jayrutty Bilioni 5.6 kwa mwaka mkataba wa miaka 5.
FT: Al Masry 2-0 Simba SC
Leo Mnyama Simba SC
👉kakosa bahati
👉Walikosa ubora mbele ya goli
👉Waamuzi wamewaua Simba
🛑Huu ni moja kati ya mchezo wa robo fainali wa ugenini ambao ulikuwa mwepesi kwa Simba mnoo.
Baada ya ushindi wa leo dhidi ya Tabora Yanga imefikisha michezo 13 mfululizo ya Ligi wamecheza bila kupoteza. Mara ya mwisho kufungwa kwenye Ligi ilikuwa Novemba 7, 2024.
•Kwenye michezo hiyo 13 (Ushindi 12, sare 1), wamefunga mabao 47 wamefungwa mabao 5.
Yanga Afrika 🔥🔥🔥
Hakuna Kiongozi wa Simba & Yanga au muwekezaji anayepewa nafasi kwenye hivi vilabu bila baraka za Serikali.
👉Hutakiwi hupewi timu, unatakiwa utapewa nafasi .
⛔️Hizi timu ni TUNU ya Taifa
Taifa la Japan kutoka barani Asia , limekuwa taifa la kwanza kufuzu kombe la Dunia la 2026.
Japan wamefuzu baada ya kuifunga Bahrain mabao 2-0 na kufikisha alama 19 kwenye kundi C.
👉Hii ni mara ya 8 mfululizo Japan 🇯🇵 wanafuzu kucheza kombe la Dunia.
Liverpool kutoka kwenye nafasi ya kushinda makombe 4 mpaka sasa wamebaki na kombe 1 tu.
🛑FA Cup wametolewa Roundi ya 4
🛑UEFA CL Wametolewa raundi ya 16 bora
🛑Carabao Cup wamefungwa Fainali
✅Wanaongoza Ligi Kuu Uingereza EPL kwa tofauti ya alama 12.