🚨Hassan Kabunda anafunga kwenye mechi mbili mfululizo za ligi kuu,alifunga dhidi ya Mbeya City,kafunga dhidi ya Yanga,ule upande wa kushoto wa Wananchi,kama Namungo wataendelea kuutumia vizuri,watakuwa na madhara !.
SIMBA sports imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kuwakanda Coastal kwa chuma mbili kwa moja,Chama tena na mechi hii amekuwa Man of the Match! !.....
Kurudisha histori za waliofanya wengine kuhusu uwanja wa Kaunda na kushindwa kuwa ndoto kamili ni kuwaokea heshima na kuwavunja MOYO viongozi wa sasa walio madarakani,kwa HATUA tu waliyofikia wanahitaji kupongezwa zaidi kuliko kuupinga huu UTHUBUTU wao !!....
🚨‼️Ilikuwa Yanga wenyewe ndiyo walikuwa wanawarejesha mchezoni Dodoma Jiji,hizi timu kubwa ukiwa tu na uwezo wa kuzilazimisha kufanya makosa unakuwa na uhakika wa kupata alama,hatimae UNBEATEN ya Yanga ya muda mrefu imepotezwa na Dodoma Jiji,Imagine,sio kama ulivyodhani SIO?!
Mechi iliyopita (dabi) kwenye Muungano Cup, mwamuzi alitoka Kenya,kwa hii trends na tutegemee mwamuzi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kutangazwa kuchezesha dabi au apewe nani wa ndani (mwamuzi) hii mechi?!!....
🚨Afrika Kusini hasa Mji wa Durban,kuna kundi kubwa la raia linasaka au kupita mtaa kwa mtaa kwa kuwatafuta wahamiaji haramu, yaani wakikukuta kuwa Mwafrika mwenzao na huna vitu muhimu vinavyokufanya ukae nchini humo kazi unayo,taifa kama la Ghana ndio limeathirika zaidi .
🚨Al Ahly baada ya Anguko lao hasa la michuano ya klabu Bingwa msimu huu,na wao wameanza maboresho,Zougrane kutoka MC Alger,Tougai kutoka Esperance pia anatajwa kunyatiwa na Ahly,hawa msimu ujao wakiwa mabingwa tutashangaa tena?!.
🚨MAFIA kuwarudisha tena Ulingoni Mfaume Mfaume na Iddy Pialali,pambano sasa rasmi kupigwa tarehe 27 ya mwezi wa Saba,kwenye tukio la USIKU WA VISASI,Pialali na Mfaume walitaka kuzichapa "kavukavu" kabla ya kutangazwa kwa Pambano hilo !!.