Mimi na Mathematics ni paka na panya tokea shuleni lakini kwenye maisha niligundua Kuna hesabu ndogo sana inawashinda watu wengi sana, na nilitoka kwenye hilo kundi la watu wengi.
Ni hivi;
Inachukua Dakika 5 kumtumia DM mtu aliyekuzidi na ambae unatamani kujifunza kwake au kufanya nae kazi. Mfano @moodewji .
Akikujibu inaweza kuwa a life changing opportunity. Asipokujibu unakuwa umepoteza dakika 5 katika dakika 1,440 za siku yako moja then maisha yako yanaendelea kama kawaida.
Wengi wetu tunaogopa kupoteza dakika 5 kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yetu ambapo dakika 5 izo zikienda as you wish maisha yako yanaweza kubadilika kabisa.
Kwa itakayemsaidia: Motivational statement ni andiko ambalo unaelezea kwanini umeamua kuapply na kuelezea ni namna unaweza kuongeza value kwa hiyo kampuni.
Kwa fursa kama hiyo ya kuvolunteer UN, Motivational Statement inaweza kuwa hivi:
PERSONAL STATEMENT
With great respect, I would like to apply for the volunteer opportunity at the United Nations. I have always been deeply motivated to help communities, and I am eager to use my skills and experience to create positive change. I believe this opportunity will provide me with the chance to contribute to global agendas focused on peace, human rights, and sustainable development.
For the last 4 years, I have been involved in volunteer activities at the community level with Tanzania Youth Vision Association (TYVA) and Youth of United Nations (YUNA) Tanzania, and I have learned that collective effort can transform lives. I have dedicated myself to serving people with special needs, working in building capacity of youth, and supporting overall economic empowerment for the marginalized. Volunteering with the United Nations would be a major step in my journey of service and in learning more about global challenges.
I am committed to putting forth my full energy, professionalism, and volunteer spirit to effectively contribute to the goals and projects of the United Nations. I am determined to be part of a team that works hard to bring about positive impact in the communities we serve. This opportunity is a call to serve, and I am highly passionate about contributing to it.
Yours dutifully,
Nyamayao Kibakuli
(Kama una mifano ya miradi uliyofanya au uliyoshiriki ni bora zaidi)
A sober 🧵.
Kuna watu hawanifahamu vyema. Mimi nimesoma TARIME shule ya msingi na sekondari form one. Nikahamia Mara secondary ambapo nimemaliza form 4 mwaka 2000 nikahamia Dar rasmi. Baba yangu alikuwa daktari, mama mwalimu. Ila ndoto yangu mwanzo ilikuwa kuwa professional DJ..
HIZI NDIZO BIASHARA UNAZOWEZA KUFANYA KWENYE MIKOA 26 YA TANZANIA.
Pia nimeunganisha na mawazo 190 ya biashara
Kupata hii PDF yenye Pages 10.
commment "nahitaji"
"Repost" hii post
Na, hakikisha umenifollow ili niweze kuingia kwenye inbox kukutumia.
📌
Mara nyingi sana watu wengi huwa hawaelezi ‘watu wa mbali’ siri za mapito halisi ya maisha yao. Pengine kwa kutokuwa na uwezo wa kuhadithia, ama kwa kuhofia kutosikilizwa na watu. Ama kwa kuona mambo haya ni ‘too private!’.
Wakati mwingine huwa wanaona hakuna haja wala sababu ya kuelezea.
Aidha, siyo kawaida kwa wanasiasa kuelezea mambo ya ndani yanayowahusu. Pengine sababu wanaogopa kujiweka wazi sana ama imekuwa siyo culture tu ya viongozi kuwa wazi kiasi hicho.
Mimi nimekuwa wazi sana. Sababu ya kukua kiuongozi kwenye zama za kuibuka kwa social networks na kwenye zama za kukua kwa idadi ya vijana ukilinganisha na wazee (demographic dividend).
Mwanzoni niliamini nafanya vizuri sababu ntapata umaarufu utakaonisaidia kukua kisiasa. Leo najuta! Why? Story for another day.
Jana nilizungumza kwa kirefu sana na rafiki yangu wa karibu tuliyepotezana kwa muda mrefu. Nilimueleza namna nilivyowakata watu wengi baada ya kuwa nje ya cabinet. Nikamuambia hata yeye kuna wakati nilimuona amezingua, naye nikamkata!
Akasema nilijua, sema ulizidisha kuji-victimize sana kiasi kwamba ulifanya iwe ngumu hata kuwasiliana na wewe kwenye mambo kadhaa. Lakini niliamua kukupa muda tu. Nilipoamka leo nikatafakari sana mbio za maisha yangu miaka hii mitatu na nusu nikasema leo niwe tofauti na watu wa aina yangu niongee hii story bila kuchagua ya kusema na ya kuacha. Lengo ni watu wengine wapate somo chungu na gumu la maisha na wala siyo kitu kingine chochote kile!
Ilikuwa siku njema kama nyingine. Naelekea Mwenge kikaoni, saa 9 - 10 mchana; kisha kikao kingine Hotel Seacliff.
Nikiwa namalizia mazungumzo yangu Mwenge, nikachungulia simu yangu ili ku-confirm kikao kinachofuata. Nakutana na meseji ya mmoja wa wasaidizi wangu wa zamani kule Afya, na ile picha ya ukumbi na mic ya Ikulu, ananiambia Chief Secretary anaongea muda si mrefu, all the best Mkuu! Nikajua ni cabinet hii inatangazwa. Kumbe hii ilikuwa ni meseji ya zaidi ya saa moja na ushee liliopita.
Nilipo-scroll chini kidogo, zikaanza kuja meseji kedekede. Kumbe baraza liliishatangazwa. Moyo paap! Kwa meseji chache nilizoweza kufungua sikuona ya pongezi hata moja, nikajua Mhh! Simo hapa. Nikapoteana kwa sekunde kadhaa, kiza kikatanda machoni, nikahisi kuelemewa na mzigo kichwani; nikaaga na kuondoka. Nilikuwa najiendesha mwenyewe siku hiyo. Nikaingia kwenye gari na kuondoka kuelekea Seacliff kwenye kikao kingine, njia nzima nikitafakari kilichotokea.
Maswali yakiwa mengi zaidi ya majibu. Mpaka nafika Seacliff nikawa tayari niliishaji-compose vizuri, na niliishaanza kukubali matokeo. Nikawa tayari niliishamshukuru Mungu na kuamua kusonga mbele. Baadaye nilikuja kujua hii ilikuwa ni reaction ambayo ingedumu kwa muda mfupi tu, maumivu ya mabadiliko ya status ni makubwa na makali kuliko nilivyodhani! Kumbukumbu ni nyingi na ni ngumu kusahau na ama kusahauliwa na wengine, Maana Kuna wakati utajikumbusha, utakumbuka na ama utakumbushwa. Maisha yako hayawezi kuwa sawa tena baada ya kupanda na kisha kuanguka! Wewe ni aina nyingine tena ya mtu, kuna experiences tofauti ambazo utapaswa kujifunza na kuzizoea.
Leo naandika hapa nimejifunza kitu kipya kabisa kwenye maisha ya siasa na uongozi. A whole new experience! Hii experience ni mpaka uipitie ndiyo utajua.
Mwanzoni nilijiuliza sana; hivi Rais Magufuli nimemkosea nini mpaka asiniteue tena? Nimekosea wapi? Mbona nimepiga kazi sana, rekodi yangu ya uchapakazi, utendaji, ubunifu, kukua kwa idadi ya watalii, kukua kwa mapato na uzalendo iko wazi na anaijua na kila leo amekua akiisema, na kunisifia? Kwa nini leo kanibadilisha? Nilijihukumu sana, niliitafuta sababu sana. Kiukweli sikuipata.
Nilijifariji na kujituliza moyo na msemo kwamba “you become what you become at the pleasure of the President!.” Nikasema sina kosa ila Mkuu hajapendezwa tu kuniteua tena, maana nafasi ni zake na anazitoa kwa raha yake!
Hata hivyo roho haikuwa ikitulia kirahisi namna hiyo. Asikudanganye mtu. Maswali yalikuja tu….inaendelea! #HK #Fighter #NjeYaBox
CASK IN DAR!
Watu wa kisasa, wale legevu legevu, ukisingiziwa kuwa una project kubwa na maarufu kama Cask in Mwanza na Cask in Dar ungefurahi na kuvimba kichwa. Tena wakati mwingine ungejisingizia kuwa ni ya kwako hata kabla hujasingiziwa.
Watu wa kisasa, walio wengi huwa hawaamini kwenye watu wasafi na wanaofanya mambo yao kihalali na kwa uwazi tu. Hawaamini kwamba kijana mdogo kama Joe anaweza kumiliki utajiri wote ule alionao.
Watu wa zama hizi wanaamini kwamba Joe hawezi kuwa na mali zote hizo, ni kwamba ni za jamaa yake HK, kwa kuwa nilikuwa Waziri. Wengi wanaamini HK aliiba pesa Wizara ya Maliasili na Utalii na akaficha pale Cask na kwenye miradi ya Joe.
Kwanza ni dharau kwa Joe, na pili ni matusi na kunichafua kwangu. Joe ni mpiganaji na mbunifu wa kupigiwa mfano. Nilikutana naye China miaka zaidi ya 18 iliyopita! Story for another day.
Aidha, mimi siwezi kuuza pombe! Sema kwa udugu wangu na Joe napata tabu kuacha kumsupport! Mungu ni mwenye kusamehe. Naendelea kuomba maghfira kwake. Kwa hakika atanisamehe!
Siwezi kumiliki hisa kwenye biashara ya pombe. Siwezi kujisifia wala kuchukua credits kwenye mafanikio ya Joe. Sababu mimi siyo mdogo kiasi hicho. Cask ingekuwa biashara yangu ningesema tu. Biashara na mali zangu ziko wazi. Sababu sina cha kuficha.
Tarehe 31 May twendeni Cask Kawe beach tukaone kazi nzuri ya Joe!
#HK #Fighter #NjeYaBox
*KIKAO CHA DHARURA CHA FAMILIA.*
Mama yetu alifanya kitu cha kustaajibisha na kisichotegemewa. Alitutumia ujumbe wa mkutano wa dharura wa familia nyumbani.
Sote wanne tulifika, lakini mama hakutupokea kwa furaha tuliyozoea.
Hata baba alishangaa kutuona watoto wake wote wa kiume pamoja na akamuuliza Mama kulikoni, akajibiwa subiri utajua sababu.
Mama akatushukuru kwa kuacha shughuli zetu na kufika lakini tumemuudhi. Na yeyote anayemuudhi yeye anakuwa amemuudhi Mume wake.
Baba alijaribu kusema lakini mama alivyomtazama akanyamaza na kutabasamu tu.
Akatuuliza siku ya kuzaliwa ya baba yenu ilikuwa lini?Tukaangaliana kwa nyuso za hatia. Ilikuwa ni jana nikajibu.
Mama akasema kama nakumbuka vizuri hakuna hata mmoja wenu aliyepiga simu wala kutuma ujumbe kwenda kwa baba yenu. Kama ingekuwa ni yangu nyote pamoja na wake zenu msingeisahau na mngeirusha mitandaoni. Na mgenipigia simu na kunitumia na kunijazia hela kwenye akaunti yangu. Nimewaangalia kwa miaka kadhaa lakini siwezi nikaachia hali hii iendelee.
Baba alishangazwa sana na sababu ya mama kuitisha mkutano ule.
Kila mwezi mnanitumia hela bila kuwaomba. Lakini hamfanyi hivyo kwa Mume wangu kama vile siyo Baba yenu. Kwa ukweli acheni kunitumia Mimi tu. Namba ya Baba yenu mnayo lakini hamumpigii bali mnaniambia mpe salamu Baba.
Tukajisikia vibaya kwa sababu ya ukweli aliyotuambia. Nikakumbuka kwenye sherehe yake mama niliagiza hadi matarumbeta.
Mnafikiria ni nani alilipa ada zenu wote nyie Hadi mkahitimu vyuo vikuu. Nani alilipa kodi, alileta chakula tulichokula, aliyelipa kodi mpaka tukahamia kwenye nyumba yetu. Yeye ndiye alitafuta hela za kila kitu na Mimi nilimsaidia tu. Mnafikiria Baba yenu hapendi mapenzi na ukaribu na watoto wake. Mnadhani ni mama tu anayestahil!!
Mama alijifuta machozi.
Mshukuru Mungu na nyie mna watoto na mtavuna mnachopanda. Msifikiri mume wangu halii na kusononeka. Au hasikii uchungu. Hamuwezi kujua.
Sintokuwa miongoni mwa kundi la wanawake wanao watenganisha watoto na baba zao kwa kuwaambia uongo kuwa baba yao hakuwajali na hakuwafanyia lolote.
Wapo wanaume wachache wasiojali lolote, lakini siongelei hao. Huyu baba yenu ni Simba wangu na katika miaka yake 75 bado anaustua moyo wangu
. Sintoruhusu nyie mumdharau baba yenu.
Wakati tunatafakari mama aliondoka ghafla kwenda chumbani kwao na kurudi na funguo za gari la baba na pochi yake na kumshika baba mkono.
Twende alisema mama, na baba hakukataa na kumfuata.
Mnaenda wapi? Wote tulisema kwa pamoja.
Tunaenda na mume wangu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hakutujibu wala kutupa nafasi ya kusema lolote.
Fungeni milango na geti, alimwambia Kaka mkubwa, ninao ufunguo wa akiba.
Waliingia kwenye gari na kuondoka.
Watoto tukabaki na mkutano wetu.
Tuliafikiana kuwa tumekosea na tukatambua kuwa hatuwezi kurudi makwetu mpaka tufikie muafaka wa suala hili. Tukawaambia Wake zetu kuwa hatutorudi kwa sababu hatujui wazazi watarudi saa ngapi. Tutalala huku.
Walirudi saa 1:30 usiku. Mama hakushangaa kutukuta, ila baba alishangaa. Sote tuliomba msamaha wazazi wetu, na kuahidi kubadilika.
Mwisho alimtaka baba kutuombea. Alifurahi na kutusalia sala kutoka moyoni.
Hatukurudi makwetu na tuliongea hadi usiku sana.
Sina Budi kusema mama alitupikia chakula kitamu sana.
Mpendwa msomaji, usingojee mpaka sikukuu ya Baba au ya kuzaliwa baba ndiyo umuenzi baba yako. Nyanyua simu yako na umpigie. Usimsahau katika maisha yako.
Wake waenzini Waume zenu. Msijiunge na wanawake wanaowachochea watoto wao kuwachukia na kuwatenga baba zao. Usiwageuze watoto wako kuwachukia baba yao.
Mahusiano ya familia ni ya thamani na hayana budi kuenziwa na kutunzwa siku zote kiendelevu.
Usingoje siku maalum kuonesha mapenzi na fadhila kwa wazazi wako.
Fanya hivyo kila WAKATI
ITAKUWA BARAKA kwako!!!
SIKU NJEMA!!!
For boys (na Labda wasichana pia wanahitaji kusikia haya! 🤷🏾♂️):
1. Hakikisha unaoa. Kuoa ni lazima. Kuoa siyo lazima uwe na pesa. Ukikua kiasi cha kuzalisha mwanamke, oa! Mengine yatajipanga. Uoe nani sasa, sikia mtazamo wangu!
2. Oa tu mwanamke kama unampenda na una nia ya kuanzisha familia iliyo bora. Oa mwanamke atakayekuwa rafiki mzuri kwako na mama mwema kwa wanao. Oa mwanamke mwenye MUNGU ndani yake. Ni bonus ukipata mwenye shape, lakini lazima awe na Mungu ndani yake.
3. Ikitokea ukaoa usiwe mwepesi kutoa talaka. Ipambanie ndoa yako isimame. Hakuna viumbe wagumu kuwaelewa kama wanawake. Wanadamu tuko wawili tu - Ke na Me! 😀. Lakini Ke my brother, ni mgumu sana kumuelewa. Ukiishaamua kumuoa, jifunze kumvumilia, kumhurumia, kumpuuza (akianza maneno, maana kwa uhakika ataanza tu!)
4. Usije ukarogwa hata siku moja ukamuoa msichana ambaye ana MENTALITY, ya kuwa eti Wewe ni chanzo chake cha pesa na maisha mazuri; ila zingatia tu kwamba wanawake wote duniani watakupenda na kukukubali kama una pesa!
5. Jua kwamba ni jukumu lako kumhudumia mwanamke wako, lakini mwanamke aliye bora ni yule asiye na mentality ya kukuchuna, ni yule mpiganaji anayezalisha chake, anayeweza kukizalisha chako/chenu na anayeweza kukusaidia kujenga maisha ya familia yenu.
6. Mwanaume kamili aliye bora haulizi kipato cha mkewe, hamgawii mwanamke majukumu ya familia (hata kama mwanamke ana kipato kikubwa kuliko yeye). Zingatia neno ‘mentality’ ya kiume. Na mentality ya ‘kike’! Kaa kwenye mentality yako, ila kama ulichagua mwanamke sahihi, ata-step in kuinyanyua familia na hali ya maisha yenu bila kuambiwa, bila kulalamika, kwa siri na staha kubwa, na bila kukudhalilisha.
7. Epuka kukaa kwenye mahusiano na mwanamke anayekuomba nauli kila siku mkitaka kwenda out, anayekuomba pesa ya salon kila mkitaka kutoka, anayelewa pombe sana, anayependa kuwasiliana na kujenga urafiki na wanaume wengine, anayependa kufuatilia maisha ya couples nyingine na kujifananisha nao, anayetamani vitu vikubwa vikubwa wakati anakuona unajitafuta!
8. Epuka kuwa na mahusiano na mwanamke anayeona anakupa favour kuwa na wewe, anayeona uzuri wake ama show zake kitandani ndiyo kila kitu!
9. Epuka kuwa na mwanamke anayeona wewe siyo saizi yake sema basi tu, asiyeweza kukutambulisha kwa ndugu na rafiki zake, asiyejivunia kuwa na wewe, asiyeweza kwenda out na wewe! Epuka huyo!
10. Epuka mwanamke mwenye password nyingi sana kwenye simu yake, anayesevu namba za wanaume kwa codes, asiyeweza kupokea simu mbele yako, anayeweka airplane mode mbele yako, anayezima data mbele yako, anayeanzisha biashara bila wewe kujua mipango yake, anayependa sana kujiremba hadi kupitiliza! Epuka huyo!
#HK #Fighter #NjeYaBox
Wakati ww unawaza kuhusu kununua kiwanja ujenge kuna wenzako tayari wameshaandaliwa Viwanja, Majumba na Mashamba.
Ukiwaza kununua pikipiki kuna wenzako washaandaliwa magari ya kila aina.
Ukiwaza kupata mtaji kuna wenzako wameandaliwa Makampuni.
ACHA KUSHINDANA NA WATU.