- Hivi ni baadhi ya vipimo tu, ila mtoa huduma wako anaweza kuongeza vipimo vingine, kulingana na mazingira, historia ya mjamzito kwa ujumla na mumuwe, n.k
- Hivyo kwa ushauri zaidi unaweza kwenda kituo cha afya au hospitali iliyo karibu yako.
Vipimo vya muhimu kufanya katika udhurio la kwanza kwa mama mjamzito.
. Kipimo cha mkojo (urinalysis)
. Magonjwa ya zinaa
. Saratani ya shingo ya kizazi
. Kiwango cha sukari
. Malaria
. Shinikizo za damu
. Uzito
. Kimo / urefu
. Ultra - sound.
#afyayamamanamtoto#unicef#afya
Ambapo hutoa muda mwingi kwa virutubisho na maji kurudishwa (kufyonzwa) kwenye mwili na kupelekea haja kubwa kuwa ngumu kwa uhaba wa maji kwenye haja kubwa.
#afyayamamanamtoto#afya#WHO#elimukwaumma.
Kwanini Wajawazito Hupata Haja Kubwa Ngumu (Constipation).
Kipindi cha ujauzito mwili huzalisha kiwango kikubwa cha homoni ya "progesterone" ambayo husababisha misuli ya utumbo kutokufanya kazi vizuri (relax) kusafirisha vitu na kusababisha chakula na taka kutembea taratibu,
Je unajua kutokutumia vidoge vya Vitamini B9 (Folic Acid) kabla ya ujauzito au miezi mitatu ya awali ya ujauzito inakuweka kwenye hatari ya kupata mtoto mwenye ubongo wazi/ ubongo mdogo/ bila ubongo kitaalamu "anencephaly".
#mahudhulioyotekliniki#mimbasalama#elimukwaumma
Je unajua muda sahihi wa kujua jinsia ya mtoto wako akiwa tumboni kwa kutumia "ultrasound"?
Ni kuanzia wiki ya 20 unaweza kujua jinsia ya mtoto wako.
#afya#magonjwayamamanamtoto#WHO
Tatizo la kunuka mdomo au kutoa harufu mbaya kinywani kitaalamu hujulikana kama "halitosis", ambayo utokana na sababu mbalimbali kama vile, magonjwa ya fizi, ukosefu wa unyevuunyevu mdomoni, kutokusafisha kinywa,kutokusafisha kinywa vizuri, kukaa muda mrefu bila kuongea, n.k
Halitosis ni tatizo ambalo linaweza kuondolewa kabisa ( to be eliminated) kwa njia mbalimbali kama vile:-
Kusafisha kinywa kwa namna sahihi na kwa muda sahihi, kutokukaa muda mrefu bila kuongea, kutoacha kinywa kikavu kwa muda mrefu, n.k
Namna ya Kutengeneza Mbadala wa ORS ukiwa Nyumbani.
Ni vema kutumia ORS kutoka hospitali au sehemu nyingine ya kutolea huduma za afya, ila ikishindikana basi unaweza kufanya yafuatayo kama mbadala wake huku ukijiandaa kununua ile inayotakiwa.
- maji Safi na salama = Lita 1.
- sukari = vijiko 6 vya Chai
- Chumvi = 1/2 (nusu) kijiko cha Chai.
Baada ya kuwa na hivyo vitu, unatakiwa kuvichanganya kwapamoja, baada ya kupata huo mchanganyiko, unaweza anza kumpa mtoto au mhusika.
Kama utaitunza kwenye friji basi itumike ndani ya masaa 24.
Je Wajua?
Mama mjamzito aliyekuwa na uzazi pinganifu (obstructed labour) anatakiwa kukaa na mpira wa mkojo (urinary catheter) kwa angalau siku 7 hadi 14 baada ya kufanyiwa upasuaji au kujifungua.
Lengo la kufanya hivyo ni kumkinga mama dhidi ya "Fistula"
KIWANGO SAHIHI CHA DAMU KWA MJAMZITO (Normal Hb in pregnancy women).
Kiwango cha damu kinachohitajika kwa mama mjamzito ni kuanzia 11g/dL na kuendelea (Hb > 11g/dL)
VIATARISHI VYA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA.
-matumizi ya sigira / bidhaa za tumbaku.
- kuongezeka kwa shinikizo la damu.
- uzito mkubwa / uliyopitiliza.
- kiwango kikubwa cha sukari (hyperglycemia).
- kiwango kikubwa cha mafuta mwilini
- Kutokufanya mazoezi.
JE UNAJUA CHANJO DHIDI YA "Tetanus" INAKULINDA KWA MUDA GANI?
TT1: haikulindi Kwa muda wowote
TT2: inakulinda Kwa mwaka mpaka miaka mitatu (1 - 3).
TT3: inakulinda Kwa miaka 5
TT4: Inakulinda Kwa miaka 10.
TT5: Inakulinda Kwa miaka yote ya uzazi (childbearing years)