Imani hudumishwa pale madai yanapojibiwa kwa ukweli na uwazi. Siyo mara ya kwanza kusikia tuhuma kama hizi za wizi wa Fedha za Chadema zikimhusisha moja kwa moja @HecheJohn lazima hatua za haraka zichukuliwe na avuliwe Mwenyekiti kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassanakiwa kwenye picha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Daniel Francisco Chapo baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kikazi, tarehe 03 Julai, 2026.
Viongozi, wafanyabiashara pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 30 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, tarehe 01 Julai, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza historia ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani CityJijini Dar es Salaam, tarehe 01 Julai, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na mmoja wa wafanyabiashara ambaye ni mlemavu katika Maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, tarehe 01 Julai, 2026.
Usiku wa leo mkoani Dar es Salaam, nimeungana na viongozi na wananchi wenzangu kuadhimisha miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Maadhimisho haya yametupa fursa ya kuendelea kutambua na kujivunia mchango mkubwa wa TRA pamoja na walipakodi wote katika maendeleo ya Taifa letu.
Tunapotekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ni muhimu kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani. Hili litafanikiwa wananchi wakilipa kodi kwa uaminifu, TRA ikikusanya kwa haki, na Serikali ikitumia mapato kwa uadilifu.
Sote tuendelee kukumbuka kuwa, kulipa kodi ni wajibu, ni uzalendo, ni heshima, na ni dhamana inayorudi kwa wananchi kupitia huduma na shughuli za maendeleo.