Lengo la Uhusiano ni KUONGEZA FURAHA, AMANI na MAENDELEO CHANYA katika Maisha ya mtu. Ukiona uko na Uhusiano na Mtu na Hupati hivyo vitu Vitatu, Kaa chini kwa Utulivu Ujiulize Je uko Mahala Sahihi?? Ukipata majibu utajua cha kufanya.
Tukio la Kariakoo liwe ni Alert kwa Serikali yetu kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani Kufikiria, Kuongeza Vifaa na Nguvu Kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kama Nchi Tuumie Kupoteza Maisha ya Mlipa Kodi Hata mmoja Tu.
Poleni wana Kariakoo.
#prayforkariakoo#Kariakoo
Ukifanya Utafiti wa Kawaida tu, utagundua wengi hulalamika wenzi wao wamebadilika baada ya kuwa wameoa/kuolewa nao maana kipindi cha Mahusiano aliigiza Usahihi badala ya Uhalisia ili ampate mtu husika ila alipoingia kwenye ndoa akabadilika akawa Yeye Halisi Sasa.
Wakati Mwingine tunakosa tulivyo vitamani na kuvitaka tuwe navyo sio kwasababu hatuna akili, hekima ya kuvitunza au bahati mbaya ila ni kwasababu Hekima ya Mungu ni Kubwa kuliko akili na Mipango yetu. Pengine angeviacha kwetu vingeharibu maisha yetu yajayo.
Nafikiri Tuna Mengi ya Kujifunza kwa wenzetu wachina na wajapan, Wamechukua Teknolojia tu kwa Mzungu ila hawajahangaika kuiga Culture yao. We Africans tuko Busy Kujisifia Kuongea Kingereza, Na Kuiga Culture ya wazungu badala ya Kuiga Tech zao. Ujinga ni Kama Umerogwa Vile.
@PabloYende Hakuna Kitu Ni Raha Sana Kuishi Tanzania na Nyumbani...Kuishi Ulaya Upweke ni Mwingi sana Ni Vile Hamjui tu. Unaweza kuwa na Maokoto ila Kama huwezi Socialize Depression itakutafuna na Hela utaziacha hiyo ndio sababu watu tunarudi bongo tukishazichanga mbele.
Kuna mdada mpaka muda huu yupo kwa wrong relationship kwa sababu tu ya gari na nyumba kali ya jamaa. Analia na kutukanwa kama mbwa mwizi kila siku, ila waaapi anajikazaa tu kisa ataacha kupiga ka selfie na mkanda kwenye gari na kujirekodi tiktok kwenye nyumba nzuri.
Hakikisha mitandao ya Kijamii haikufanyi ujione hujafanikiwa, Huna Maisha, Hakikisha haikufanyi ujione wewe sio mzuri au Huna Akili za Maisha. Kumbuka Jirani ambaye amebahatisha kupika pilau kuku huwa na fujo sana tofauti na siku akipika tembele.
Kitu usichojua kuhusu Wanawake ni kwamba Hela zao huwa zinawauma kutumia hata kwa matumizi yao wenyewe ni basi tu huwa wanajikaza. Ndio maana anajiona ana Raha sana akipewa hela zisizo zake kuzitumia.😂
Ukiwa Brand Strategist & Designer afu Mwana Simba(Shabiki wa Simba),Afu ukakutana na hili la Jezi na yote kwa ujumla wake. Unapata hasira; unakunywa maji afu anatulia tu.
Bro Kama Babe wako hakupi umbea wa siku husika, Jua she is not free or inlove with you. Mwanamke akikupenda atakupa sana umbea. Yani utakua unamuwasha yani wowote ule ilimradi umbea, Uwe unahusu kazi, majirani, marafiki ilimradi umbea. Ukiona hupewi umbea ujuwe kuna mtu anampea.
Wazazi walikulea vizuri ila wakati unakuwa, ukajifunza tabia mbaya toka kwa marafiki, Nawe ukazikubali ili usionekane mshamba, Badala yake Tabia Hizo ulizofanya utotoni/ujanani zimekuharibu hadi ukubwani, Umekuwa tofauti na wazazi wako walivyotazamia uwe. HUYO SIO WEWE NASEMA.