Leo Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya 6 ya Pasaka mwaka A wa Kanisa. Tunakaribia mwishoni mwa kipindi cha Pasaka, na Mama Kanisa anatuandaa kwa ajili ya Adhimisho la Sherehe ya Kupaa kwa Bwana na ile ya Pentekoste. Ujumbe wa leo ni ujumbe wa matumaini na faraja. Yesu, akiwa anakaribia kuondoka kati ya wanafunzi wake na kuingia katika Fumbo Takatifu la Pasaka, anawaambia wanafunzi wake na anatuambia sisi sote kuwa, “Sitawaacha Ninyi Yatima.” Anatuahidi Roho Mtakatifu, Msaidizi, Roho wa Kweli, atakayetufariji, kutufundisha na kutukumbusha yale yote aliyotufundisha Kristo.
Kristo anatualika kuishi katika upendo na muunganiko wa kudumu pamoja naye, upendo ambao hauthibitishwi tu kwa maneno, au kwa kufuata juu juu amri zake, bali upendo uliojikita katika utii wa hiari wa Amri zake. Katika Dominika hii, tunaalikwa kufungua mioyo yetu ili Roho Mtakatifu apate makao ndani mwetu, na atupe nguvu ya mashuhuda Hodari wa Injili, kama anavyotuambia mtume Petro, kuwa tayari kumjibu kila mtu aulizaye Habari za tumaini lililo ndani yetu, kwa upole na kwa hofu.
Roho Mtakatifu ndiye anayetupa hamu na uwezo wa kutenda kadiri ya amri za Mungu. Yeye tunaweza kusema ndiye ndiye injini ya maisha yetu ya kiroho. Kumbe katika Dominika hii tunajifunza kuwa ili kumsikia na kumtambua Roho Mtakatifu, ni lazima kwanza tujitofautishe na ulimwengu. Ulimwengu una kelele nyingi; tunajifunza kutafuta utulivu wa ndani ili kumtambua huyu mgeni wa ajabu anayekaa ndani yetu, Roho wa ukweli, Roho Mfariji.
Kila mbatizwa anao wajibu wa kuwa Nabii, kuhani na Mfalme katika ulimwengu huu unaoonekana kuwa yatima katika Nyanja mbalimbali. Kuwa Nabii ni kufundisha Neno la Mungu, kuonya, kukemea. Katika ulimwengu ambapo kumekua na mmomonyoko mkubwa wa maadili, tunaalkwa kuwa walimu thabiti wa Imani. Tunaitwa kuwa makuhani, kujitoa sadaka kwa wengine, kumdhihirisha Kristo kwa nafsi zinazoteseka, waliojikatia tamaa na kuona hawana thamani tena. Kwa njia ya Roho Mtakatifu tunakuwa wafalme, kuongoza wengine kumjua Kristo na kuujua ukweli wa Injili. Kristo anatutumia mimi na wewe, kudhihirisha uwepo wake wa kudumu katika ulimwengu huu.
Katika Dominika hii, tunaalikwa kufungua mioyo yetu ili Roho huyo wa Kweli atufanye kuwa mashahidi hodari wa Kristo aliyefufuka, kama anavyotuambia mtume Petro, “kuwa tayari siku zote kumjibu kila mtu atuulizaye Habari la tumaini hilo la ufufuko wa Kristo lililo ndani mwetu, kwa upole na kwa hofu.”🙏
Leo Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya Pili ya Kipindi cha Pasaka. Kadiri ya mapokeo, kilatini dominika hii inaitwa “domenica in albis deponendis,” kwa sababu ni siku ambayo waliobatizwa katika Mkesha wa Pasaka walivuliwa kanzu nyeupe waliyovalishwa walipobatizwa ambayo walipaswa kuivaa katika katika kipindi chote cha Oktava ya Pasaka. Ni “Dominika ya huruma ya Mungu”, kama ilivyowekwa na Mama Kanisa katika maadhimisho ya Jubilei Kuu mwaka 2000, kufuatia ufunuo alioupokea Mtakatifu Faustina Kowalska kutoka kwa Yesu Kristo mwenyewe. Ni katika Sakramenti ya kitubio huruma ya Mungu inajidhihirisha kwa waliobatizwa, wakaimarishwa kwa Roho Mtakatifu kwa Sakramenti ya Kipaimara na wanapokea Ekaristi Takatifu, Mwili na Damu ya Kristo, chakula cha kiroho.
Tomaso alipokuwa nje ya jumuiya hakuweza kukutana na Kristo mfufuka. Lakini aliporudi ndani ya jumuiya alikutana naye na kuukiri umungu na ubinadamu wa Kristo.Hivyo basi, tunalihitaji Kanisa na tunahitaji Jumuiya ya Kikristo ili kukutana na Kristo. Kumbe, tunao wajibu wa kuzitunza jumuiya zetu ziendelee kuwa ishara ya uwepo wa Kristo ulimwenguni ili watu wamtambue na kumkiri. Imani yetu kwa Bwana mfufuka inapaswa kutusaidia kujenga jumuiya ya Kikristo ambapo Kristo ndiye kiongozi wake mkuu.
Hii ni jumuiya isiyo na ubinafsi, inayomjali kila mmoja, inayozingatia sala. Ni katika jumuiya ya namna hii, Bwana mfufuka anajifunua, na kuwakirimia wanaomwamini baraka na neema zake. Kama kuna shida au changamoto yoyote katika jumuiya, suluhisho si kujitenga, bali kutatua changamoto iliyopo. Kama umejitenga na jumuiya yako kwa sababu yoyote ile, rudi mapema, na ushiriki shughuli zake ili ukutane na Yesu Mfufuka upate neema na baraka tele.
Mwisho tunaona kuwa Huruma ya Mungu inatupa uwezo wa kupenda. Hatuwezi kudai kuwa tunaipokea Huruma ya Mungu wakati hatuwaonei huruma wengine. Huruma inatufanya tuwe watii kwa amri ya upendo kwa Mungu na kwa Jirani zetu. Hitimisho. Katika dominika hii tunaalikwa sote, tuitumainie huruma ya Mungu isiyo na mipaka, nasi kama walivyokuwa Mitume wa Yesu baada ya Pentekoste, tuwe mashuhuda imara wa Huruma ya Mungu kwa njia ya maisha na utume wetu.🙏
Leo Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya 32 mwaka C wa kiliturujia katika Kanisa, kipindi cha kawaida. Tuko ukingoni na mwishoni mwa mwaka wa kanisa kilitrujia, ujumbe wa masomo unahusu maisha baada ya kifo, fumbo la maisha ya sasa na yajayo katika ulimwengu ujao.Kwa kuwa hakuna aliyeweza kuthibitisha kuwa hakuna maisha baada ya kifo, sisi tunaamini kuwa kuna maisha baada ya kifo na tunamuomba Mungu atustahilishe kuyashiriki.
Tunaalikwa kuwa mashahidi wa matumaini, si kwa maneno tu bali kwa maisha yetu, Kuisimamia imani bila woga, kama vijana wa Mmakabayo. Kudumu katika kazi njema licha ya mateso, kama anavyosema Mtume Paulo. Kuishi maisha ya sasa kwa mtazamo wa uzima wa milele, kama alivyofundisha Yesu.
Ee Bwana, Mungu wa walio hai, tupe moyo wa uthabiti kama wa vijana wa Mmakabayo.
Tuimarishe katika kazi njema, utuongoze kwenye uvumilivu wa Kristo, na utujalie kuishi maisha haya kwa macho ya matumaini ya milele. Ee Mungu wa walio hai, tukusikie katika sala hizi. Tufanye kuwa watu wa matumaini, tukimtazamia mwanao Yesu Kristo aliyefufuka na kutushindia kifo. Tunakuomba hayo kwa njia yake yeye anayeishi na kutawala milele.Tufanye mashahidi wa uzima, hata katika dunia yenye kifo. Amina.🙏
@Eric__Bernard “Waliokutafuta ndio real circle yako,”
but have you ever checked on those who didn’t? 🤷🏽♂️
You never know what they’re going through maybe they’re just surviving life in silence.
Stop blaming people jamani, everyone is fighting their own battles differently. 💭
Leo Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya 30 ya mwaka C wa kiliturujia katika Kanisa, kipindi cha kawaida. Ujumbe makuu unahusu umuhimu wa fadhila ya unyenyekevu ambayo kimsingi ni kanuni ya dhahabu inayomwezesha mwamini kukua na kukomaa katika fadhila ya imani, matumaini na mapendo kwa Mungu na jirani; kinyume chake ni madhara ya kiburi, kujikweza, kujikinai, kuwadharau wengine na kujiona wenye haki zaidi.
Injili ni kama ilivyoandikwa na Luka (Lk 18: 9-14). Fundisho lake kuu ni umuhimu wa unyenyekevu na madhara ya kiburi, kujikinai, na kuwadharau wengine; kwa maana mbele za Mungu hakuna aliye bora kuliko mwingine, na uzima wa milele ni zawadi ya Mungu kwetu, hakuna anayeweza kujistahilisha mwenyewe kwa nguvu zake.
Pili, tusiwahukumu, wala kuwadharau wengine kama farisayo kwa mtoza ushuru. Hii ni dhambi mbaya sana. Daima tukumbuke kuwa Yesu alikufa Msalabani kwa ajili ya ukombozi wa wote. Matunda ya dhambi zetu ni kuteswa kwake hata kufa Msalabani. Kila binadamu ni mdhambi kwa kiwango chake, hivyo hakuna mwenye haki ya kumuwekea Mungu mipaka katika kutoa neema na baraka zake.
Tatu, huruma ya Mungu ni zawadi, hatuwezi kuinunua wala kuidai, tunaistahilishwa na kuipewa kwa kujinyenyekesha na kukiri ukosefu wetu waziwazi mbele za Mungu.Basi tunaposali tuepuke vizingiti vinavyoweza kubatilisha sala zetu. Tuishinde hofu, tujiachie mikononi mwa Kristo, ili yeye atutendee kadiri apendavyo, yote ikiwa ni kwa sifa na utukufu wa Mungu ili kwao sisi tutakatifunze.🙏
Leo Mama Kanisa anaadhimisha dominika ya 24 ya mwaka C wa kiliturujia katika Kanisa, kipindi cha kawaida. Ujumbe mkuu wa masomo ya dominika hii ni kuwa; Huruma ya Mungu ni ya milele. Mungu daima yuko tayari kumsamehe mkosefu anayetubu, na anafurahi kusamehe, na furaha ya kweli kwa mwanadamu imo katika kung’amua kwamba amesamehewa na Mungu, baada ya kukiri na kutubu makosa yake, na hivyo anakuwa na amani tele moyoni mwake.
Ujumbe kwetu ni huu; tukitambua, tukajuta na kukiri dhambi zetu, Mungu Baba yetu ni mwenye huruma atatusamehe na kututakasa na uovu wetu wote.
Nasi tunaaswa kuwatafuta na kuwasamehe waliotukosea, kwa maana msamaha huanza kutolewa na aliyekosewa. Mungu hatushurutishi kutambua makosa yetu, kuyajutia, kuyakiri, wala kurudi kwake na kuomba msamaha. Lakini kwa saburi anatusubiri turudi na kusema nimekosa nihurumie, naye daima anamsamehe na kumfanya tena mtoto wake kwa kumkaribisha katika karamu ya uzima wa milele, kila anayetubu na kuomba msamaha, bila kuangalia idadi ya makosa yake.
kwa ambao hawana passport|pasipoti ya kusafiri na huwa wanajiuliza ni nini kinatakiwa ili kukamilisha zoezi pitia video hapo chini uweze kupata mwanga kidogo Asanteni🙏🏼
SHARING IS CARING @bongoinusa
https://t.co/SwukGmhGWD
Leo Mama Kanisa anaadhimisha Sherehe ya Pentekoste, ni siku ya hamsini baada ya ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni siku ya kuadhimisha tukio la kipekee na la msingi sana kwa Kanisa - kuzaliwa kwake kwa njia ya Roho Mtakatifu yaani kuumbwa upya kwa Taifa jipya la Mungu. Siku ya Pentekoste ni kilele cha Sherehe ya Pasaka, kwa sababu utajiri wote aliotufunulia Yesu mfufuka unaanza kuonekana katika mioyo na maisha ya Mitume. Roho Mtakatifu ni ishara ya umoja wa Kanisa, ni Sherehe ya waamini walei wote.
Tumruhusu Roho Mtakatifu akae ndani ya mioyo yetu, ndani ya nafsi zetu, ndani ya familia zetu na jumuiya zetu atufundishe kuishi kwa upendo, atufanye tuwe safi, aondoe tabia zinazoendana na hila za shetani. Awashe ndani mwetu moto wa mapendo, atupe Roho ya hekima na elimu, atufundishe kusali vizuri, atushushie kipaji cha ukweli na mapendo ya kweli. Aondoe vilema vyote vinavyoweza kutuvuruga na kutuletea maafa, atutie nguvu ya kuweza kufahamu madhaifu yetu, ili sote tuungane na kuwa mwili mmoja katika Kristo na tuione sura ya Mungu katika wenzetu kwa kuwapenda kama Kristo Yesu alivyoagiza.
Tumsifu Yesu Kristo!🙏