Mojawapo ya fahari na uhuru wa kweli wa jamii yoyote ile ni kujenga uwezo wa kila mwananchi kupata matibabu sahihi, bora, nafuu na kwa wakati pale anapopata changamoto za kiafya.
Nchi yetu inajivunia hatua kubwa tunazoendelea kupiga kwenye eneo hili ambapo pamoja na maboresho na ujenzi, sasa kila Hospitali ya Rufaa ya Kanda inatoa huduma ya MRI na kila Hospitali ya Rufaa ya Mkoa inatoa huduma ya CT scan.
Shukrani hizi toka mkoani Kagera kutokana na maboresho makubwa yanayoendelea katika sekta ya afya mikoa mbalimbali nchini si zangu na Serikali pekee, bali ni za kila Mtanzania popote pale alipo anayechapa kazi kuifanya nchi yetu kuwa bora zaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwania wa Ndlege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, Windhoek chini Namibia kwa ajili ya Mkutano wa dharura wa Troika plus wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Nawatakia kila la kheri wanangu wote mnaoanza mitihani yenu ya Kidato cha Sita kesho. Tunawategemea. Tunawaamini.
Naamini mmejiandaa vyema kwa hatua hii muhimu kwenye safari yenu ya elimu, na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape utulivu na siha njema mkahitimishe salama na kwa mafanikio.
Serikali itaendelea kuhakikisha inaandaa mazingira bora katika safari yenu kuelekea hatua zifuatazo ikiwemo Vyuo vya Ufundi, Vyuo vya Kati na Vyuo vya Elimu ya Juu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kikwete, Ikulu Jijini Dares Salaam tarehe
27 Aprili, 2023. Rais wa Rwanda Me. Kagame amewasili nchini kwa ajili ya ziara ๐น๐ฟ