#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 21
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana jela)
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuwa maafisa Magereza. Wanapaswa kukagua barua inayotoka ndani au kuingia ndio inapaswa kusomwa.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Soma kifungu cha 46 Cha Sheria na kanuni ya 10 na 11 ya kanuni za Magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Anahangaika haoni.
Mhe. Lissu: Sasa wambie majaji kama kanuni ya 10 na 11 inahusu barua wanazoandika na wanazoandikiwa wafungwa.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na wanaosoma ni wewe au maafisa wako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe, Lissu: Ukiikataa barua unamrudishia na kumwambia sababu. Na kama ikikataliwa kwa aliyemletea pia unamrudishia na kumpa sababu. Na kama barua ni ndefu sana na huyapendi ni sahihi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama nje ya barua kwa wafungwa au kutoka kwa wafungwa una mamlaka ya kukagua na kusoma nyaraka nyingine yoyote.
Ntamamiro (Bwana jela) : Naomba soma Section 12 ya Prison Act.
Mhe. Lissu: Kwa kanuni hizi unaruhusa ya kusoma nyaraka nyingine.
Ntamamiro (Bwana jela) : Soma kifungu cha 12 cha Sheria ya Magereza
Mhe. Lissu: Unauwezo wa kusoma nyaraka za mawakili wanaokuja nazo magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sipaswi kusoma.
Mhe. Lissu: Hicho kifungu cha 12 unachosema kinahusiana na upekuzi wa magari na kumkagua mtu sio nyaraka ndio maana sitaki hata kukisoma. Hakikusaidii chochote.
Mhe. Lissu: Kisabo alisema wakiwaambia muondoke ili azungumze na mimi mteja wake mnakataa. Kweli au sio kweli.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Na mimi nimesema kwenye viapo vyangu kuwa alikuja Wakili Alute Lissu. Na kusema nina ujumbe muhimu kutoka serikali nataka niongee nae Faragha. Mkamkatalia. Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana jela): Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Umekuwa unaendeshwa na rimoti na Kamishna Mkuu na wanasiasa walioko serikalini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kuna siku umeniita ofisini kwako kuwa kuna ujumbe wa jumuiya ya madola napaswa kupelekwa mjini? Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sina Jibu.
Mhe.Lissu: Siku hiyo aliyekuja kunichukua ni Mangara?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: sio kweli nini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hujawahi kupelekwa.
Mhe. Lissu: Siku nyingine ulinifuata na kusema Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge Duniani amekuja kuniona anaitwa Martin Chungong na nikapelekwe mjini na Senior Mangara.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Kuna siku Heche, Amani na Mnyika uliwaruhusu kutokana na kulikuwa na maelekezo kutoka juu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kabla hujaja walikuwa wanaruhusiwa na ulipokuja ukawazuia hayo mamlaka ulitoa wapi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nimeshajibu.
Jaji: Ulijibuje
Ntamamiro (Bwana jela): Sikuwakataza.
Mhe. Lissu: Alipokuja Lema Godbless, wewe ulipokuja na kutukuta ulimfukuza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kama sio kweli kwanini haya yote hukuyajibu kwa nyaraka wakati mimi nimeyasema kwenye nyaraka zangu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Sasa kama umewazuia walalamikaji watatu, mashahidi wangu, umewazuia mawakili wangu. Unanitakia nini kwenye kesi ya uhaini inayonikabili ambayo adhabu yake ni mimi kunyongwa?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nilishajibu.
Jaji Mruma: Umejibu nini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sijamzuia mtu yeyote kuja kuonana na Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Sina swali lingine.
Majaji wanamuuliza Wakili wa Serikali.
Anasema naomba tuahirishe tuendelee kesho.
Wakili John Seka: Naomba tuendelee bado muda tunao.
Jaji Mruma: Sasa hoja ya kuahirisha na logistics zilivyo, TLS nao kupewa nafasi wamuhoji shahidi. Sisi tunaomba kusema yafuatayo.
Leo tutaahirisha kutokana na sababu kama za jana, tunaamini leo tumefanya kazi kubwa, kesho tutasema mengine.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 15
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Mkuu wa Gereza, Ntamamiro (Bwana Jela)
Mhe. Lissu: Je askari magereza ambae hasikii au hauoni atashuhudiaje mazungumzo ya mfungwa na ndugu zake watakapokuja kumtembelea
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hayo ni masuala ya kidaktari.
Mhe. Lissu: Sasa Bwana Jela hujui kama wasaidizi wako wote hao kuwa hujui kama wanasikia au hawaoni wewe ni mkuu wa gereza wa aina gani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sik daktari.
Mhe. Lissu: Wewe ni Mkuu wa Gereza wa aina gani? Usiyejua afya za wasaidizi wako?
Ntamamiro (Bwana Jela): Nastahili kuwa kwenye nafasi hii.
Mhe. Lissu: Ndio maana nchi imekwama. Kama watu wenyewe ndio nyie na akili hizi
Mhe. Lissu: Umekuwa Officer incharge tangu lini pale Ukonga?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sept. 2025.
Mhe.Lissu: Ulihamishiwa Ukonga ukitokea gereza kuu la maweni Tanga?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio.
Mhe.Lissu: Ulikuja ukonga kuchukua nafasi ya Juma Mwaibaku?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli.
Mhe. Lissu: Ulipohamishiwa Ukonga mimi tayari nilishakuwa mahabusu ukonga toka April 2025?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Wakati unahamia Ukonga ulikuta nakaa kwenye special wing pale ukonga?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli
Mhe. Lissu: Wakati unahamia pia ulinikuta naishi huko pamoja na wafungwa wa adhabu ya kifo 100?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sikuwakuta.
Mhe. Lissu: Je ulinikuta nakaa peke yangu au sio peke yangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio peke yako.
Mhe. Lissu: Wafungwa gani hao?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mmoja.
Mhe. Lissu: Je kwa miezi 5 ambayo hukuwepo nilikuwa naishi na wafungwa wa kifo takribani 100?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sifahamu.
Mhe. Lissu: Umeona record ya maandishi ya waliokuwepo special wing umeiona au hujaiona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijapitia hiyo records.
Mhe: Lissu: Hili suala nilishalilalamikia na lipo kwenye nyaraka za mahakama.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sifahamu. Tuendelee na maswali mengine.
Mhe/ Lissu: Utaratibu wa wageni kuja kuniona ni weekend?
Ntamamiro (Bwana Jela) : kweli
Mhe. Lissu: Utaratibu wa wageni wangu kuja kuniona weekend ni kwamba siku moja wanakuja ndugu zangu na siku nyingine wanakuja viongozi wa Chama.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sifahamu.
Mhe.Lissu: Wakati unahamia Ukonga ulikuta utaratibu wa kutembelewa na mawakili wangu ilikuwa nimepeleka orodha kwa mkuu wa Gereza kwa mkuu wa gereza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Orodha ya kwanza uliiambatanisha kwenye hati yako ya kiapo kinzani ile ambayo nilikuwa na mawakili 10.
Ntamamiro (Bwana Jela): Orodha hiyo hiyo moja.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hakukuwa na orodha yenye jina la Deogratias Mahinyila, Paul Kisabo na Dickson Matata na Mary Stephano.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna hiyo.
Mhe. Lissu: Angalia kielelezo SUPP 1. Ukishakiona niambie.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Anapekenyua hapa..
Mhe. Lissu: Jina la Nashon Nkungu limo kwenye hiyo orodha lipo au halipo? Ambae ni mleta maombi wa pili.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio lipo.
Mhe. Lissu: Je jina la Kisabo na Maduhu mawakili wangu yapo au hayapo kwenye hiyo SUPP 1
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawa hawapo kwenye hii orodha.
Mhe. Lissu: Sasa hao wawili wamesema kwa kiapo na kusema hapa Mahakamani kuwa kabla hujahamia ukonga walishaingia gerezani kuonana na mimi walishaingia karibia mara tatu. Wewe unasemaje? Yaani wakati ACP Juma Mwaibako akiwa Mkuu wa Gereza walihudhuria
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama ulikuwepo wakati huo?
Bwana Jela: Sikuwepo wakati huo. Ila nyaraka zinasema.
Mhe. Lissu: Nenda kielelezo ambacho ni SUPP 2 hapo.
Jaji: SUPP 2 ni nini?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hiki ni kiambatanisho na. 2 kinahusu orodha ya wageni na mawakili waliotembelea gereza la Ukonga.
Part 16 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 195
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi
Mhe. Lissu: Kwanini umepewa Jina la P7?
Shahidi wa kificho P7 : Kwasababu ya usalama wangu.
Mhe. Lissu: Si umesema hakuna aliyekutishia.
Shahidi wa kificho P7 : Ndio hivyo sasa.
Mhe. Lissu: Sina Maswali mengine.
Jaji: Karibu upande wa Serikali kwa Re Examination.
Wakili wa Serikali: Hatuna maswali kwa shahidi huyu.
Upande wa Serikali walisema wana shahidi mmoja tu kwahiyo kesi itaendelea kesho saa tatu asubuhi bila shaka.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Wakili wa Serikali: Renatus Mkude anasimama anasema kama tulivyosema asubuhi naomba tuahirishe hadi kesho asubuhi.
Jaji: Tafadhali tukutane hiyo Kesho Tarehe 19 saa tatu asubuhi.
Inapigwa high court
Watu wote tunasimama,
Majaji wanaondoka,
Watu wanaanza kutawanyika.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 191
Jaji Ndunguru anawaita upande wa Serikali kwa ajili ya Re-Examination
Wakili wa Serikali anasema hawatakuwa na maswali.
Jaji Ndunguru : Shahidi sasa uende tumemalizana.
Shahidi anasepa.
Renatus Mkude: Tunae shahidi P7 tunaomba yeye aendeleee kesho asubuhi.
Majaji wanaandika kidogo pale juu.
Kesi inaahirishwa hadi kesho asubuhi maana muda umeisha inakaribia saa 11 jioni.
So tutaendelea kesho, Mungu akitujalia uzima.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 174
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji hawako serious hawa kwanza ukisoma D4 kila kitu chake kipo hata jina lake hawajaficha lipo na taarifa zake zote zipo, hawajielewi hawa.
Katuga: Anasimama anasema Mh. Sisi ni maafisa wa mahakama aonywe mshitakiwa kwanini anasema hatuko serious.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji ni kweli hayupo serious ila nataka niliondoe neno hilo lakini kama anasema nionywe siko tayari kuonywa naomba nifanye submission ya kuonesha ni kwa namna gani hawako serious?
Jaji Ndunguru: Basi Mshitakiwa tuishie hapo kama umesema umeliondoa.
Watu wanacheka sana. 😂😂😂
Mhe. Lissu: je umesema kokote kuwa uliwahi kutishiwa maisha?
Shahidi wa kificho P6: Sijawahi kutishiwa maisha mimi.
Mhe. Lissu: Kuna mwanachadema au kiongozi amewahi kukutishia kukupiga au kukudhuru kwa wewe kwenda kutoa maelezo haya Polisi?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo kabisa.
Mhe. Lissu: Je kuna ndugu yako ametishiwa pia?
Shahidi wa kificho P6: Hayupo hata mmoja.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Majaji wanaandika kidogo pale mbele.
Kwa sasa ni saa 7 na dakika 15 mchana, huu ni huwa ni muda wa kwenda Break, ngoja tusubiri Kitakachoendelea muda mfupi ujao.
Jaji: Re Examination Jamhuri?
Wakili Cathbert: Hatuna swali lolote Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru Kiogozi wa Jopo la Majaji watatu anateta tena ma wenzake kabla hajasema nini kiendelee.
Anawasha kipaza sauti.
Shahidi umemaliza sasa unaweza kwenda.
Renatus Mkude tunaomba ahirisho tukawaandae mashahidi, lisaa limoja.
Mhe. Lissu: Sawa sina pingamizi.
Jaji Ndunguru: Basi tukutane baada ya lisaa limoja.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 157
Anamalizia Mhe. Lissu
Vinginevyo haitakuwa Mahakama ya Haki na kanuni zinataka usikilizwaji wa mashauri haya uwe wa haki kwa pande zote.
Ni hayo tu waheshimiwa majaji.
Anamaliza Mheshimiwa Lissu hapa.
Majaji wanateta huku wakiandika kidogo.
Mheshimiwa Lissu anakusanya makabrasha yake taratibu hapa. Bila shaka kesi itaahirishwa leo. Watahitaji kuandika uamuzi wa hoja zilizowasilishwa.
Anawasha kipaza sauti Jaji Ndunguru hapa akiwa serious sana na kama amechoka. Anaonesha hana nuru kabisa. 😂
Naomba niseme yafuatayo kabla sijaahirisha shauri.
Mtakumbuka leo tumevumiliana sana kuhusu simu zinazopiga kelele kama tunashindwa kukaa na simu basi kwenye ukaguzi tutaomba mziache.
Naomba mtambue uvumilivu wa leo hautaendelea kuwepo kuhusu masuala ya simu.
Shauri linaahirishwa hadi Tarehe 11/02/2026 saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 150
Anaendelea Mhe. Lissu
Hivyo naomba sheria hii kama Jaji Mtembwa aliitumia, naiomba Mahakama hii isiendelee kukosea, isiendelee kuitumia.
Waheshimiwa Majaji mkiangalia sheria namba 7 ya 2018 utaona imeandikwa kwenye header note kuwa sheria hii imetolewa kwenye gazeti maalum la Serikali la tarehe 15 Septemba 2018, waheshimiwa majaji huo ni uongo.
Uthibitisho kuwa ilichapishwa kwenye gazeti la serikali ni kulitoa gazeti lenyewe, proof sio what the law says, bali ni physical existence or electronic existence.
Nawaomba waheshimiwa majaji msiitumie hii sheria, msipoitumia maana yake mashahidi waje watoe Ushahidi hadharani, hii ya kufichaficha mashahidi gizani haitakuwepo kabisa na haitakiwi kabisa kuwepo.
Anasimama Wakili wa Serikali Nassoro Katuga yupo kama amechanganyikiwa au ametoka kubeba gunia la mchanga ni mdogo kama Pilton.
Amesimama akiwa amenywea sana na kusema,
Kwa hoja nyingi zilizoletwa tunaomba muda wa kujiandaa kujibu hoja nyingi sana ambazo mshtakiwa amezisema.
Tunaomba tarehe ambayo tutapangiwa kwaajili ya kuja kujibu.
Lissu hajapinga ila ameomba tarehe ya karibu zaidi wapewe.
Kesi imeahirishwa kwa muda usiojulikana hadi pale ambapo Mahakama itatoa Notisi ya siku ya kusikilizwa kwasababu notisi ya awali ilionyesha mwisho wa kusikiliza kesi hii ni leo Novemba 12, 2025.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 148
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja yangu ya nne Waheshimiwa Majaji ipo kwenye kanuni ya 6(2) ambapo Mahakama inaweza kutoa amri bila kuathiri haki ya kusikilizwa kwa usawa.
Waheshimiwa majaji naomba hiyo kanuni isomwe pamoja na kanuni ya 5(2)(f) ambayo inasisitiza kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kwamba kuna effective cross examination.
Waheshimiwa Majaji naomba mtafakari hayo maneno ya mahitaji ya fair trial, kutohatarisha maslahi ya haki na kuhakikisha kuna effective cross examination.
Waheshimiwa majaji kwenye kesi ambayo adhabu yake ni kifo, shahidi akatoa Ushahidi ambaye Mahakama haimfahamu, mshtakiwa hamfahamu isipokuwa tu mawakili wa serikali.
Shahidi akitoa Ushahidi bila mahakama kumuona, majaji hawamfahamu, mtuhumiwa atafanyaje effective cross examination? Shahidi asiyejulikana na Mahakama, haonekani kwa mtuhumiwa itatoaje uamuzi ambao hauhatarishi maslahi ya haki?
Waheshimiwa majaji kuruhusu Ushahidi wa namna hii itakuwa ni a mockery of justice and just adjudication of cases by the court, hakutakuwa na haki kabisa.
Waheshimiwa Majaji katika mazingira haya shahidi akiruhusiwa kutoa kinachoitwa Ushahidi wake:
Mahakama itajuaje demeanour of the witness?
Hii haitakuwa fair hearing, hakutakuwa na usawa mbele ya sheria, mtahakikishaje waheshimiwa majaji kuwa kutakuwa na usawa mbele ya sheria kama ambavyo Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya JMT inasema.
Tunapozungumzia usawa mbele ya Sheria hatuzungumzii kanuni zilizotungwa na Jaji Mkuu tu peke yake, tunazungumzia kanuni za kikatiba pamoja na Ibara ya 107A ambayo inaweka sharti kwamba Mahakama lazima itende haki sawa kwa wote.
Waheshimiwa majaji hili litawezaje kutekelezwa kama mtaruhusu mashahidi msiowajua na msiowaona kutoa Ushahidi? Waheshimiwa majaji nawaomba msije mkakubali kutumika kuharibu utendaji haki katika mahakama zetu, don’t ever allow.
Labda nichomekee jambo hapa kidogo. Ukiachana na Mh. Lissu anaongea Sheria lakini lolote analosema linamuingia kila mtu akilini na moyoni. Ukiwaangalia hata Majaji ni kama wanasema unachokisema tunakuelewa kabisa na ndio ukweli wa Mungu lakini tutafanyaje sasa? Hiyo ndio impression tunayoiona hapa Mahakamani tukiwa tunawatazama majaji na hata mawakili wa Serikali. Ukiwaangalia hata mapolisi waliopo humu nao sura zao zinasema ni kweli hatujui sheria sisi kama mapolisi ila anayosema Lissu yanaeleweka na ni sahihi.😂
Waheshimiwa majaji haya niliyoyasema ya misingi ya haki yamewekwa pia katika mikataba mbalimbali ambayo nchi yetu imeridhia.
Naomba niwape mifano, Ibara ya 2 , 7, 10 and 11 za Tangazo la Haki za Binadamu of UDHR 1948, Ibara ya 14(1) , 14(3) (e ) na 26 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kirai na Kisiasa wa Mwaka 1966 (ICCPR) zote zinazungumzia usawa mbele ya Sheria, ulinzi sawa mbele ya sheria.
Waheshimiwa majaji naomba kuwasomea Ibara ya 14(3)(e) of ICCPR inasisitiza kuhusu in full equality, mkiruhusu shahidi ambaye hamumjui, hamumfahamu, mimi simuoni na wala simfahamu, hiyo in full equality itatoka wapi?
Vilevile Ibara ya 3 na 7 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu, ibara ya 6(d) na 7(2) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rules of Procedure International Residual Criminal Procedure Mechanisms hizi zimeweka gold standard na best practices za umoja wa Mataifa hivyo mahakama zetu zinaweza zikazitumia hasa kanuni ya 75A, 75C, 86A na 86B.
Waheshimiwa Majaji hizi kanuni 4 ndio best standards za kulinda mashahidi, hivyo utaratibu huu upo sio kwamba umegunduliwa na mawakili wa serikali na hazina hii darkness tunayotaka kuletewa hapa (Lissu anaonyesha kizimba alipojificha shahidi wa leo),😂😂
Utaratibu huu hauwezi kuleta fair trial, mkiruhusu huu utaratibu unaotaka kuletwa hapa then we must forget about fair trial.
Part 149 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 147
Anaendelea Mhe. Lissu
Waheshimiwa Majaji,
Hoja yangu ya pili ni kwamba, huyo shahidi ni shahidi wa namna gani?
Kwa mujibu wa kanuni ya 3 lazima awe yuko chini ya amri ya ulinzi.
Sasa Mahakama hii inawezaje kujua shahidi kama yuko chini ya amri ya ulinzi?
Naomba kuwarejesha kwenye Kanuni ya 5(1) ambayo inasema mtu huyo lazima awe amebainishwa katika maombi.
Maana ya haya maneno ni nini?
Maana yake rahisi ni kwamba mtu ambaye jina lake lilipelekwa kwa jaji likaombewa ulinzi.
Jaji awe anamfahamu kwa jina na kuwa maisha yake yako hatarini.
Naomba niwarejeshe kwenye hati ya maombi ya tarehe 14 Julai 2025, hiyo application ina viapo viwili, ina kiapo cha SSA Mose Kaima na ACP Amini Mahamba.
Waheshimiwa majaji kwenye hiyo hati ya maombi, hivyo viapo viwili hakuna kiapo hata kimoja chenye jina la shahidi hata mmoja.
Katika orodha ya mashahidi wanaoitwa wamepewa ulinzi, hakuna hata jina moja la shahidi ambalo lilipelekwa kwa Jaji Mtembwa.
Hiyo amri ilitolewa on insufficient ground na ilitolewa kwa concealment (kwa kuficha Ushahidi kwa mahakama) na mawakili wa serikali.
Walipaswa kupeleka majina kwa jaji lakini hawakufanya hivyo, hivyo Jaji Mtembwa hawafahamu na nyie waheshimiwa majaji hamuwafahamu, wanajulikana tu na waliowaleta, hivyo sitaki kusema kuwa amri ya ulinzi ilipatikana kwa fraud but by concealment by the State Attorneys.
Waheshimiwa majaji kama hiyo ni haki then tunahitaji tafsiri mpya ya haki huku Duniani.
Waheshimiwa majaji sio tu kuwa hakuna majina ya mashahidi ila hakuna hata majina ya wanaowatishia ni maneno tu, maneno matupu kabisa.
Hata nature ya vitisho haijaelezwa kwamba wanatishiwaje, kivipi na nani anawatisha? Haipo kabisa.
Waheshimiwa majaji, sasa niende kwenye hoja yangu ya tatu ambayo ni kuhusu amri ya Mahakama Kuu;
Mahakama kuu ilitoa ulinzi upi? Ili kujibu hilo swali sawasawa naomba nitangulize kanuni ya 7(1) ya Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi.
Kanuni inasema kwamba hatua za ulinzi wa shahidi zitadumu kwa kipindi cha usikilizwaji wa kesi isipokuwa kama amri husika itaashiria vinginevyo.
Kwenye uamuzi wa Jaji Mtembwa maombi ya Jamhuri yalikuwa kutokuonyesha utambulisho wa mashahidi wanaotarajiwa kwa kutokuweka wazi nyaraka zinazoweza kupelekea shahidi kujulikana, matumizi ya majina bandia, amri nyingine yoyote kwaajili ya usalama wa mashahidi wa Jamhuri wakati wa mwenendo wa ukabidhi au wakati wa kesi kusikilizwa.
Naomba waheshimiwa majaji pia muangalie kanuni ya 6(1) ili muone ni maombi gani mengine ambayo kama upande wa mashtaka wangetaka wangeyaomba.
Kanuni hii imetaja orodha ya amri zinazoweza kuombwa na kutolewa na mahakama. Zimeelezwa kwa uwazi kabisa kwenye kanuni husika hii itatusaidia kuelewa ninachotaka kukisema.
Waheshimiwa majaji, katika kanuni hiyo ya 6 kuna amri 16 ambazo zinaweza kuombwa na hiyo ya kutumia kizimba maalumu hawakuomba mawakili wa serikali.
Katika dunia hii waheshimiwa majaji, usipoomba hupewi, hili sio takwa la kisheria tu ni takwa pia la kibiblia kuwa ombeni nanyi mtapewa.
Jamhuri walipewa amri nne walizoomba lakini amri ya kutumia kizimba maalum hawakuomba, hivyo hawawezi kupewa kitu ambacho hawakuomba katika lugha ya kisheria, they are estopped.
Waheshimiwa majaji kwa maoni yangu kanuni hizi zilitungwa kuwafurahisha waendesha mashtaka na watu wao. They are totally one sided.
Waheshimiwa majaji kwa mujibu pia wa kanuni ya 8 kama Jamhuri wangeona amri za Jaji Mtembwa haikulinda mashahidi sawa sawa walikuwa na fursa ya kuleta maombi mbele yenu kwa mfano kuwa tunaomba kutumia kizimba maalum, hawajaleta maombi hayo.
Now it is late in the day to sneek in today kuleta hao mashahidi. Wameleta wakijua kanuni hizi hamtazisoma au mshtakiwa atanyamaza. Wamelalia haki yao, waachwe waendelee kuilalia.
Part 148 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo November 12, 2025.
Last time tuliishia part 145, Leo tunaendelea na-;
Part 146
Mheshimiwa Lissu ameingia Mahakamani kama kawaida akiwa na vibe amekoroga "amezungusha ngumi" akiwa na morali ya kutosha.
Kama kawaida ameambatana na maaskari magereza wakutosha ambao huwa wanamlinda.
Siku za karibuni tulisema sehemu ya askari hawa wamekuwa ni wapya sio tunaowafahamu wa siku zote.
Inapigwa High Courttttttttt kubwa sana na kali.
Watu wote wamesimama hapa na Majaji wanaingia.
Sauti ya Askari imeendelea hadi Majaji wamefika kwenye viti vyao na kukaa ndio ameacha huyu askari.
Mawakili wa Serikali wamejitambulisha na kusema leo wana shahidi na wako tayari kuendelea na kesi.
Shahidi waliyenae leo ni shahidi wa siri ambae ni P11 kwahiyo wako tayari kuendelea Jamhuri.
Anaulizwa Mh. Lissu kama na yeye yuko tayari.
Mhe. Lissu anasema:
Niko tayari waheshimiwa lakini naomba niseme neno dogo tu sio la kuweka kwenye rekodi.
Jaji anashangaa sio la kuweka kwenye rekodi ni jambo gani hilo na lina umuhimu gani sasa?
Mhe. Lissu anajibu ndio waheshimiwa majaji sio la kuweka kwenye rekodi na neno langu sio lingine bali ni kwamba,
Nimefurahi kuwaona maana huko nilikokuwa hizi wiki mbili hakukuwa kwa kawaida.
Watu wote wameangua kicheko mahakamani hadi Majaji wamecheka.😂😂😂
Anaendelea Mh. Lissu
Mh. Jaji hapa Wakili wa Serikali Nassoro Katuga ameiambia Mahakama kuwa kuna mashahidi wengine wa Siri na hivyo leo tutakuwa na Shahidi P11.
Huyo Shahidi wa siri ameingia na Mahakama haijamuona.
Sasa nina pingamizi, waheshimiwa majaji huyo shahidi wa siri anatakiwa asimame kwenye kizimba na sio huko ambako haonekani.
Napenda kuwafahamisha kwamba hili suala la ulinzi wa mashahidi, nimelitafakari kwa zaidi ya miezi 6 sasa na nimeliangalia kwa makini sana.
Naomba kutoa hoja kwamba, hakuna shahidi yoyote kwa amri iliyotolewa na mahakama hakuna shahidi hata mmoja ambaye anatakiwa kutoa Ushahidi akiwa hapo kwenye kificho, anatakiwa akae hapo kizimbani.
Naomba nianze na sheria kwamba inasema nini? hapa Lissu ameandaa nondo za kutosha naona yuko imara kuanza pambano hili la kisheria.
Mahakama imejaa utulivu na kamvua kameanza kunyesha kwa mbali.
Watu wametulia utafikiri wanasubiri kuchomwa sindano au wanasubiri kupewa utaratibu wa kuanza kumuaga marehemu. Utulivu ni mkubwa sana.
Naomba nianze na sheria sasa kwamba inasema nini kuhusu hawa wanaoitwa Mashahidi wa siri?
Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za Mwaka 2025, zimeeleza hicho kiboksi hapo ni kitu gani kisheria?
Sasa kisheria kinaitwa kizimba maalum cha shahidi na kwa kanuni hizi kizimba kimetafsiriwa kwenye kanuni ya 3 kuwa ni sehemu ya kusimama au kukaa wakati wa kutoa Ushahidi iliyoandaliwa mahususi ili kutoa Ushahidi bila kuonekana isipokuwa na Jaji au Hakimu.
Nasisitiza isipokuwa kwa Jaji au Hakimu. Sasa swali Je hapo alipokaa shahidi waheshimiwa Majaji mnaweza kumuona huyo shahidi?
Majaji wanashangaa na kila mtu anashangaa, Waheshimiwa majaji kwa macho yangu shahidi hapo haonekani kwa majaji, wala mimi simuoni. Watu pekee wanamjua ni hawa mawakili wa serikali waliomleta akina Katuga.
Mhe. Lissu anaendelea kuweka ngumu kuwa huyo shahidi asiyeonekana kwa majaji, kwa mshtakiwa ni shahidi wa namna gani?
Kwa misingi gani ya haki katika dunia hii? Mhe. Lissu anahoji huyu shahidi anapaswa kusikilizwa.
Labda nichomekee kidogo ili mpate picha. Hicho kibox anachosadikika shahidi kipo sehemu ya juu pembeni kidogo na mlango wanaoingilia majaji.
Ni kibox kimetengenezwa kama kasanduku hakuna mtu unaweza kumuona ukiwa upande wowote maana kimezungushiwa pande zote nne so huwezi kumuona kabisa. Pia hakijawekwa hapa kwa sehemu ya mashahidi wanaposimama siku zote. Kiko kule juu kabisa. Hata majaji hawawezi kumuona aliyepo ndani ya hicho kibox chao. Kwa mbele kina kama kioo kidogo lakini pia huwezi kuona ndani kuna nini kupitia hicho kioo.
Part 147 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 140
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali ya Dodoso
Ulisema Wakati wa kuandaa taarifa yako ya Uchunguzi ni lazima ufanye reference kwenye Police Notebook na huku ukiangalia yale uliyokuwa umeandika kwenye Polisi Notebook, ni sahihi ulisema hivi?
Samuel Kaaya : Nilisema.
Mhe. Lissu: Yako wapi sasa kwenye maelezo?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuhusu covering letter na ukaiambatabisha na taarifa ya Uchunguzi, Je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Ni kweli nilisema lakini hayapo kwenye maelezo yangu yale ya Polisi.
Mhe. Lissu: Hiyo covering letter umeleta?
Samuel Kaaya : sijaleta kwasababu ni internal communication.
Mhe. Lissu: Kwahiyo haiwahusu Majaji?
Samuel Kaaya : Ni kweli haiwahusu.
Mhe. Lissu: Sasa kama haiwahusu uliisema hapa Mahakamani ili iweje?
Samuel Kaaya : Mimi Sijui.
Shahidi hapa amepiga ile tunaita CHAKUFIA NINI?😀😀😀
Mhe. Lissu: Je barua uliyoandikiwa ya kukuomba ufanye uchunguzi umeiwasilisha kwenye kesi hii?
Samuel Kaaya : Hii haina uhusiano na kesi hii.
Mhe. Lissu: Je barua ya pili umewasilisha?
Samuel Kaaya : Sijui wanayo Mawakili wa Serikali.
Mhe. Lissu: Unasema ulifungua mafile mawili ya Uchunguzi baada ya kupata hizo barua kutoka requesting authority. Je hayo mafile umewasilisha mahakamani kama kielelezo?
Samuel Kaaya : Sijawasilisha.
Mhe. Lissu: Mahakama sasa itajuaje kama wewe ndio uliombwa kufanya uchunguzi kama hujaleta barua uliyoombwa kufanya uchunguzi na pia hujaleta ripoti wala video itakuaminije?
Samuel Kaaya : Itaniamini kwa maneno yangu hapa Mahakamani na hayo maelezo ya Polisi.
Mhe. Lissu: Umewahi kusikia msemo wa Kiswahili kuwa maneno matupu hayavunji mfupa?
Samuel Kaaya : Sijawahi kuusikia.
Mhe. Lissu ; Je mkono mtupu haulambwi?
Samuel Kaaya : Sijawahi sikia.
Mhe. Lissu: Je Mali bila daftari hupotea bila habari?
Samuel Kaaya : Huo nao sijawahi kuusikia.
Mhe. Lissu: Sasa maneno yako na wewe hapa Mahakamani yamepotea bila habari.
Watu wanacheka 😂
Mhe. Lissu: Ulisema habari ya kitabu cha Laboratory Boom Register, Je nayo umeileta hapa Mahakamani?
Samuel Kaaya: Sijaleta pia.
Mhe. Lissu: Hivi ili uwe assigned kufanya uchaguzi utararatibu ukoje?
Samuel Kaaya : Zipo minutes pale kwenye file la Ofisi ndio anaandika huko.
Mhe.Lissu: Hiyo ndio tunaita kwa lugha za ofisi ni Dokezo 70 kwamba inaandikwa kazi fulani aifanye fulani?
Samuel Kaaya : Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa umeleta hiyo dokezo 70 hapa Mahakamani?
Samuel Kaaya : Sijaleta.
Mhe. Lissu: Nisaidie ulisema kulikuwa na majalada mawili la kwanza ni taarifa za uongo na la pili ni uhaini. Hayo maneno yako wapi kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Hayapo sikuandika.
Mhe. Lissu: Katika uchunguzi wako ulisema hiyo video ilikuwa uploaded kwenye channel ya youtube ya JAMBO Tv ni sahihi?
Samuel Kaaya : sio sahih, mimi nilisema video imepatikana kwenye youtube kupitia account ya Jambo Tv.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hiyo video ilipatikana kwenye account ya Jambo TV?
Samuel Kaaya : sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze kama uliweza kubaini mtu aliyeiweka video clip kwenye hiyo account ya Jambo Tv?
Samuel Kaaya : Mimi experts sijibu facts najibu kama mtaalamu.
Mhe. Lissu: Sasa mimi ndio nashitakiwa kuwa nimeiweka huko Jambo TV na wewe ni mtaalamu umekuja leo nataka utusaidie, nani aliweka?
Samuel Kaaya : Account ya Jambo Tv ndio iliweka hiyo account.
Jaji Kalyamaahe: Kwahiyo ulibaini mtu au hukubaini mtu aliyeweka hiko youtube?
Samuel Kaaya : Mimi sikubaini mtu.
Mhe. Lissu: Mimi nashitakiwa kwa kuweka hiyo video huko Jambo Tv basi na mimi nitumie fursa kusema Mwenyezi MUNGU akurehemu na kukubariki sana maana kama mtaalamu umesema mimi sijaweka huko hiyo video nani mwingine atakuja kusema mimi niliweka hiyo video. Ahsante sana.
Part 141 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 138
Mhe. Tundu Antipas Lissu akiwa anaendelea kumsomea Shahidi maelezo yake.
Anasema naomba tuelezane yafuatayo.
Majaji watatu ambao ni Dunstan Ndunguru-Mwenyekiti wa jopo.
James Karayemaha – Jaji mjumbe wa jopo.
Ferdinand Kiwonde – Jaji mwingine wa jopo.
Wameingia kwenye rekodi ya kusikiliza shauri hili la Uhaini linalomkabili Mhe.Tundu Lissu na kwakweli kwa hatua ya sasa ya wao kukataa kupokea hivi vielelezo viwili kwa maana video pamoja na report ya mtaalamu nafikiri hata kama wamefanya kwa mujibu wa sheria na kweli.
Mungu atawabariki kwa hilo kwasababu kwa Mahakama zetu na namna tulivyowazoea hawa Majaji wangeweza kuamua vinginevyo na tusingekuwa na la kusema.
Nafikiri katika hili na sisemi wamefanya kwa nguvu zao ila ninachokisema lolote walilolifanya angalau rekodi zitawatambua kuwa kuna maamuzi ya msingi waliyafanya katikati ya kesi hii.
Kazi kwao huko mbele kama hawatajidharirisha.
Kwa hatua ya sasa nafikiri WATANZANIA hawawadai chochote hawa Majaji.
Wamejitahidi kutenda haki na Mimi binafsi nawaombea kwa Mungu kila la kheri kwasababu tunafahamu wanaafanya kazi kwenye utawala ambao professionalism hakuna kabisa pongezi sana kwao kwa hatua ya sasa.
Mara baada ya pongezi hizo, Mheshimiwa Lissu anamueleza shahidi maeneo ambayo anataka kum contradict shahidi kutokana na kilichopo kwenye maelezo yake Polisi na alichosoma hapa Mahakamani.
Ameshafika eneo la 30 kwa sasa ambayo yanatofautiana na maelezo yake hapa Mahakamani. Ikiwa ni pamoja na Elimu yake ya Upolisi, Masomo aliyosoma nyakati tofauti tofauti, vyuo na course mbalimbali za kipolisi alizosoma South Africa, India na maeneo nengine.
Mhe. Lissu alikuwa anasoma maeneo ambayo amefikisha maeneo 75 anayotaka kwenda kumcontradict shahidi.
Mhe. Lissu amemuuliza Shahidi je ungependa maelezo yako sasa yapokelewe kama ushahidi Mahakamani?
Shahidi: Waheshimiwa Majaji naomba yapokelewe kama ushahidi.
Jaji Ndunguru anasema maelezo hayo yamepokelewa kama kielelezo cha Mshitakiwa na nitayapa alama Exhibit D2 ya upande wa Mshitakiwa.
Kwa kifupi kwa msio elewa hadi sasa Jamhuri hawana kielelezo chochote kilichopokelewa kuunga mkono kesi yao.
Ila upande wa Mshitakiwa Tundu Lissu hadi sasa amefanikiwa kuingiza vielelezo viwili yani Exhibit D1 na Exhibit D2 ambavyo vyote lengo lake ni kuonesha mashahidi wa Jamhuri ni waongo na wanatunga mambo.
Waliyosema hapa Mahakamani ni tofauti na walichokiandika kule Polisi nako ni tofauti kabisa.
Kwahiyo kwenye vielelezo hadi sasa ni mbili bila. 😂
Mhe. Lissu anaanza sasa kuendelea na maswali yake.
Kwenye ushahidi wako ulisema wewe ni mtaalamu wa picha na uliteuliwa kwa kazi hiyo naomba angalia maelezo yako uliyotoa polisi kama ulisema kuwa wewe ni mtaalamu wa picha kwa mujibu wa GN NO. 725/2020.
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: ulisema hapa Mahakamani Kati ya 2003 na 2004 ulihudhuria mafunzo ya Polisi Moshi CCP sasa angalia kwenye maelezo yako kama mambo hayo yapo?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Hapa Mahakamani ulisema ulisomea Criminal Law, Singe, Judo na Karate na masomo mengine sasa waeleze majaji kama yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: je kuhusu ulipandishwa cheo na kupata cheti cha umahiri nayo yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuwa ulifanya mafunzo ya upigaji picha je yapo hayo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Part 139 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 23, 2025
Jana tuliishia part 136 so leo tunaendelea na-;
Part 137.
Mh. Lissu ameingia ila leo amekuja na ujumbe anasema kuwa yatakwisha tu.
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.
Karani anasoma namba ya shauri
Wakili wa Serikali Renatus Mkude anatambulisha jopo la Mawakili wa Serikali na anasema yuko tayari kwa ruling kwa upande wao wa Jamhuri.
Mshitakiwa nae anasema yuko tayari.
Anaanza kusoma Jaji Kiwonde kwa niaba ya Majaji watatu.
Mshitakiwa alipinga shahidi Na. 3 kutoa report kwani ilipaswa kuwa ni certificate lakini pia mshitakiwa alisisitiza kuwa shahidi huyu ni mtaalamu wa picha na sio video.
Lakini pia Mr. Job Mrema yeye alijibu pingamizi hilo na kusema pingamizi halina mashiko.
Alisema Mahakama hii haibanwi na maamuzi yake aliyoyatoa siku ya jana kuhusu flash na memory card.
Na mshitakiwa alienda mbali kuingia kwenye content za report wakati Mahakama ya Rufani ilishazuia jambo hilo.
Mr. Mrema anasema kwa mujibu wa kifungu cha 216 cha CPA shahidi anaruhusiwa kutoa hiyo report.
Kwasababu ina uhusiano mkubwa na kesi na hata yeye ndio aliandaa basi ni yeye ndio anaweza kuitoa.
Na katika rejoinder mshitakiwa anasema taarifa hii au report vina uhusiano mkubwa kama hizo device zimekataliwa hivyo hata report haina miguu ya kusimama.
Mahakama inapaswa kuamua kama shahidi Na. 3 yuko competent kutoa hicho kielelezo.
Sisi tunaona shahidi Na. 3 ni mtaalamu na kwa mujibu wa kifungu 216 kimeeleza majukumu ya mtaalamu na GN Na. 799/2020 inasema kinagaubaga wajibu na kazi ya shahidi.
Hakuna ubishi aliteuliwa na DPP na Attorney General na hicho kilichopo hapa Mahakamani ndio kipo kwenye kifungu hicho.
Kwetu sisi tunaona kazi yake ni kuzichunguza zile picha na baada ya kufanya huo uchunguzi yeye analo jukumu la kuandaa certificate.
Hizo ndizo kazi aliteuliwa kufanya.
Tunakubaliana na Mshitakiwa kuwa shahidi alipaswa kuandaa Certificate badala ya kuandaa Report.
Angekuwa ameteuliwa kama Forensic expert basi tungekubaliana na nyaraka yake.
Kwenye kesi hii shahidi Na. 3 aliteuliwa kushughulikia picha mnato ambazo zinapelekwa kwake na hilo tulisema jana pia na mwishoni anaandaa certificate.
Kwa maana hiyo hatukubaliani na Mr. Mrema kuwa kuna mtego na sisi hatuko tayari kuingia kwenye mtego alitupatia Mrema na kumuamini.
Hii taarifa inalenga kwenda kuelezea nini kama tutaipokea?
Hicho kinachoelezewa kwenye taarifa kama hakipo tukiipokea tunaopokea ili kije kutusaidia nini kama Mahakama.
Huyu Shahidi hana uwezo wa kutoa hiyo taarifa bali alipaswa kutoa CERTIFICATE.
Tunaona pingamizi lina Mashiko. Na tunakubaliana na Mshitakiwa na tumeamua hivyo.
Leo tena wamepigwa na kitu kizito hawa ndugu zetu wa Jamhuri. Wamechanganyikiwa tena kwa mara nyingine. 😂😂
Jaji amesema haya sasa muendeleee.
Anasimama Thawabu Issa Wakili wa Serikali anasema Mhe Jaji.
Jaji anamwambia subiri kwanza Wakili,
Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo.
Ukiwa unaendelea kutoa ushahidi wako.
Shahidi sawa Mhe. Jaji.
Thawabu Issa anasema Mhe. Jaji hatuna kingine cha zaidi kwa Shahidi huyu.
Tunaomba kuishia hapa
Watu wanacheka.😂😂😂
Anaitwa Lissu kwa ajili ya Maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu: Shahidi uliandika maelezo yako Polisi tarehe 08/04/2025 kwenye ofisi za Polisi Forensic Bureau?
Samweli Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu ; Je ukiyaona hayo maelezo yako utayatambua.
Samweli Kaaya: Ndio nitayatambua. Ni maelezo yangu.
Anasomewa hapa Maelezo yake na anapatiwa.
Mhe. Lissu ananendelea kumsomea Maelezo yake Polisi huyu shahidi ambae ni Samweli Elibariki Kaaya.
Part 138 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 116
Anaendele Shahidi Samuel Elibariki Kaaya
Tunafanya huu uhakiki kwasababu programu endeshi ndiyo inayoendesha hardware computer, kwa maana nyingine kama programu linzi isipokuwa compatible / isipoendana na hardware kwa maana ya compute hiyo, it cannot execute any task.
Sambamba na hilo programu chunguzi lazima iwe compatible na programu endeshi ili iweze kufanya majukum yake mahususi.
Waheshimiwa majaji hali ya programu kwa siku hiyo ya tarehe 08/04 ilikuwa timilifu kwa maana programu zilikuwa updated/zilikuwa salama kwaajili ya kufanya majukumu yake mahususi.
Waheshimiwa majaji baada ya kufanya uhakiki wa vifaa nilifanya uchunguzi wangu wa awali kwa maana ya preliminary examination.
Nilifungua computer yangu maalum kwa maana ya kuiwasha, nilichukua flash disk aina ya XIOXIA kwaajili ya kuifanyia uchunguzi.
Baada ya kufungua computer yangu niliiweka kwenye universal serial bus (USB).
Baada ya kuiweka kwenye USB niliifungua ili kutazama kilichopo ndani ya flash.
Baada ya kuifungua nilikuta ina nywila yaani passwords hivyo niliwasiliana na mamlaka iliyoleta vielelezo kwa ajili ya kupata nywila.
Baada ya kupata nywila niliendelea na uchunguzi wangu wa awali na nilikutana na video mjongeo moja ilikuwa na heading Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia majimboni, no reforms no election njia panda.
Na hiyo Video ilikuwa na urefu wa masaa matatu na dakika 38 na ilikuwa katika mfumo wa MP4 file format.
MP4 inatokana na neno MPEG part 14 (kirefu cha MPEG ni Movable Picture Expert Group).
Huyu Bwana Samweli Elibariki Kaaya nae miongoni mwa kitu anatufurahisha hapa Mahakamani ni kujifanya anapenda vingereza fulani kutaja misamiati yake ya kitaalamu.
Sasa anakosea sana kutamka hayo maneno Mh. Lissu kuna muda anauliza mara mbili mbili kuwa umetamka nini?
Akirudia anawaambia tamkeni vizuri jamani kingereza cha wapi hicho, Nafikiri kama Taifa hili swala la kizungu ni ugonjwa mkubwa, inafaa utafutiwe dawa halafu huu ugonjwa kwa mapolisi unaweza kuwa ni mkubwa sana kuliko makundi mengine yote. 😂😂😂
Thawabu Issa: Kingine nini uliona:
Shahidi: Waheshimiwa majaji pia niliona maudhui yafuatayo:
Wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi ni kweli maana tutazuia uchaguzi hivyo tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna pekee ya kuapata mabadiliko, tunakwenda kukinukisha sana sana tunaenda kuuvuruga uchaguzi huu, tunaenda kukinukisha vibaya sana.
Waheshimiwa majaji maudhui haya yanapatikana kwenye lisaa la pili na dakika 58.
Pia nilibaini mwendelezo wa matukio kwa maana ya continuity, pia nilibaini jup shoot kwa maana ya kuwa hakukuwa na kukatika kwa picha.
Nilibaini pia necessary or unnecessary movements, kulikuwa na movement za watu mbalimbali au mtu mmoja mmoja kutoka sehemu moja Kwenda sehemu nyingine.
Nilibaini pia uwepo wa rangi halisi na mwanga halisi wa picha mjongeo.
Naomba nifafanue kuhusu rangi na mwanga halisi.
Waheshimiwa majaji unaporekodi picha au picha mjongeo kuna kitu kinaitwa white balance.
White balance kazi yake ni kuseti mwanga na rangi asili ya vitu vinavyorekodiwa.
Hii white balance ina component chache kwa ajili ya kufanya hayo.
Mfano kama unarekodi wakati wa mvua utaiseti camera yako kwenye cloud setting, kama ni kwenye kivuli utaseti camera yako kwenye shadow, kama ni majira ya kawaida ya jua utaseti kamera yako kwenye day.
White balance ilituonyesha kwamba video hii ina mwanga halisi.
Waheshimiwa majaji pia nilitazama mstari mshazari na ninaomba nizungumzie hapa ili pakae sawa.
Katika mizania ya informatics object near the length of the camera is much greator than the object far from the length of the camera.
Mfano mzuri ni mtu anapojipiga selfie, sehemu ya Kichwa itakuwa ni kubwa kuliko sehemu ya miguu ambayo iko mbali na camera.
Kwa maana hiyo waheshimiwa majaji focal length is the basic attribute in this fact.
Part 117 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 115
Anaendelea Shahidi namba 3 wa Jamhuri Samuel Elibariki Kaaya
Baada ya hilo kutokea nilienda maabara kwa ajili ya kuandaa vifaa vya uchunguzi.
Barua zote mbili tukianza na ile ya FB/PH/LAB/106/2025 Ilikuwa inahusu jalada la kuchunguza uchapishaji wa taarifa za uongo na lile lenye namba /PH/LAB/107/2025 ikiwa na kosa la uhaini.
Thawabu ; umesema baada ya kuwa assigned ulienda maabara, ieleze mahakama nini ulifanya nini?
Nilifika maabara na kufanya maandalizi ya vifaa vyangu vya uchunguzi.
Maandalizi niliyoyafanya ni kuandaa vifaa chunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya uchunguzi.
Baada ya kumaliza kuandaa computer, printer kwaajili ya uchunguzi.
Tukumbuke kwamba nilikuwa na barua mbili ambazo nilikuwa assigned kuzifanyia kazi hivyo niliamua kusoma barua hizo ili kufaham matakwa ya requesting authority wanataka nini.
Mhe Jaji Barua moja ilikuwa inahusu kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na nyingine ilikuwa inahusu uhaini.
Barua ya uhaini ilikuwa na kumbukumbu namba DA.223/476/01B/169.
Barua hiyo pamoja na muhtasari ilinihitaji kufanya mambo yafuatayo; ilihitaji chanzo cha picha mjongeo inayopatikana kwenye flash disk aina ya XIOXIA, kuchunguza uthibitisho wa uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye flash disk, nichunguze chanzo cha picha mjongeo iliyopo kwenye memory card.
Pia nichunguze uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye memory card aina ya Aldeepo, kufanya ulinganisho wa maudhui ya picha mjongeo iliyoko kwenye flash disk aina ya XIOXIA kama yanafanana na maudhui ya picha mjongeo iliyokuwepo kwenye memory card aina ya Aldeepo.
Kiuhalisia huyu shahidi anazungumza jambo hilo hilo moja na Wakili wa Serikali anarudia kuuliza swali hilo hilo mara tatu tatu mpaka mtu unaona uvivu kuandika.
Mfano hiyo habari ya video ilisema nini au Mh. Lissu alisema nini kwenye mazungumzo yake na watia nia kwa namna kesi inavyoenda hata sio tatizo na amekuwa hapingi kuwa maneno yale sio yakwake. Swali lake na hoja yake ni kwamba je hayo aliyosema ni kosa kisheria? Ni Uhaini?
Sasa hawa mashahidi watupotezea muda wa siku kadhaa kutuambia namna walivyochunguza video wakati hiyo video mtuhumiwa hana pingamizi nayo. Nafahamu zipo hatua za kisheria zinapaswa kufuatwa ili exhibits zipokelewe Mahakamani lakini kwa shahidi huyu nimewauliza hata Mawakili wanasema kwa kiasi kikubwa wanapoteza tu muda. Mengine hata sio matakwa ya kisheria.
Acha tuendelee nae na tunasubiri muda wa yeye kuanza kuulizwa maswali ya Dodoso na Mshitakiwa ndio tutaelewana zaidi.
Samuel Kaaya: Pia niliambiwa nichunguze maudhui yafuatayo kama yanapatikana kwenye flash disk hiyo, maudhui hayo ni haya;
"wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kabisa maana tutazuia uchaguzi, hivyo tutahamasisha uasi, hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko, tunaenda kukinukisha sana sana, uchaguzi huu tutauvuruga maana tunaenda kukinukisha vibaya sana."
Nilifanya uhakiki wa vifaa vya uchunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya kufanyia uchunguzi huo, printer maalum aina ya Epson, nilikagua program endeshi kwa maana ya operating system window eleven, programu chunguzi kwa maana ya forensic software and security software amped five na ampend authenticate.
Waheshimiwa majaji naomba nieleze maana ya amped five na amped authenticate.
Ampend authenticate inafanya basic and advance image analysis, pia inafanya basic and advance video analysis pia inafanya utambuzi wa sura kwa maana ya facial recognition Waheshimiwa majaji nilitazama pia programu linzi kwa maana ya security software.
Hii programu linzi ni Kaspersky antivirus ambayo kazi yake ni kulinda programu endeshi pamoja na programu zote zilizopo kwenye computer hiyo na pia inalinda vielelezo unavyovipokea visiliwe na virus au malware.
Part 116 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 110
Thawabu: Baada ya kuwa Police Constable nini kilifuata?
Samwel: Nilipangiwa kitengo cha picha yani sayansi jinai.
Mwaka 2014 nilianza mafunzo yanayohusu upigaji wa picha zote yaani video na picha mnato. Nilijifunza pia SOP for Photography laboratory.
Mafunzo hayo yalichukua miezi 6 hayo ya SOP.
Mafunzo mengine mwaka 2021 hadi 2022 nilihudhuria mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi kwa maanaa ya ACP niliyachukulia Moshi huko.
Yalikuwa ya miezi minne nilijifunza leadership, criminal procedure na sheria ya ushahidi Evidence Law, Criminal Law na Parade, First Aid, Medani za Kivita, Arresting, Drill Parade. Nilipata cheo cha mkaguzi msaidiz wa Polisi.
Kundi la pili linahusu elimu ya ujuzi yaani professional qualification mwaka 2010 nilihudhuria mafunzo ya stashahada ya teknolojia ya habari na mawasiliano yaani diploma in Information technology
Pia nilihudhuria Mafunzo taasisi ya Uhasibu arusha. Anajisemea hapa alijifunza multimedia, web designing, graphical designing , OOP Object oriented programing language, sema anaongea haraka kama chiriku majaji wanashindwa kumpata vizuri mda mwingine
Anaendelea hapa alijifunza Computer mathematics, business mathematics, communication skills, database management baada ya hapo nilitunukiwa diploma in Information technology.
Anasema pia alihudhuria mafunzo 2015 ya forensic video examination and data dot technology and itching technology katika chuo cha HAMASCRA College , Gauteng Province , South Africa.
Akajifunza video analysis, email analysis, facial recognition, motor vehicle chassis number examination mafunzo yalichukua muda wa miezi 6 na akapata certificate of competence.
Anaulizwa tena kama anaujuzi mwengine?
Anasema 2016 hadi 2019 alihudhuria mafunzo ya shahada ya kwanza ya elimu ya mawasiliano alisoma IFM.
Anaanza kulist masomo alisoma data base management, computer network,object oriented programming language, supply chain management, artifical intelligence technology, development studies😂😂wanatuchosha tuu hawa.
Alipomaliza alipata Bachelor of Science in Information technology 2019.
Mwaka 2024 alihudhuria mafunzo ya CCTV Forensic Gandinaghar, gujarat state India. Sema shahid nae kutamka alikosoma hawezi anataka atuandikie hapa na hakuna ubao.
Anasema alisoma National Forensic Science University alisoma kwa miezi 3 CCTV surveillance au monitoring, NVR technology network video recorder vs digital video recorder baada ya kuhitimu alipewa certificate of attendance.
Anasema Shughuli hizi kazifanya kwa miaka 12 (utaalamu wa picha)
Anaulizwa maabara ya uchunguzi wa picha inafanyaje kazi?
Anasema wanafanya kwa kuzingatia SOP Standard Operating Procedure za maabara
Anakuwa na mtaalam mchunguzi wa maabara anaitwa Photographic Expert majukumu ya huyu mtaalamu ni kupokea barua mbalimbal kutoka kwa requesting authorities na kuhakiki vielelezo mbalimbali vinavyotoka sehemu mbalimbal, kuhakiki kama vielelezo vimekidhi matakwa ya kiuchunguzi.
Baada ya kuridhika vile vielezo vimekidhi matakwa hayo vinasajiliwa kwenye laboratory register book yaani PF113 akimaliza kusajili anatoa namba ya usajili kwa ajili ya ufuatiliaji
Akishatoa hio namba anafungua jalada la uchunguzi wa kimaabara kwa kurejea zile namba alizoziandika
Baada ya kusajili namba hio mchunguzi atapeleka jalada kwa mkuu wa kitengo kwa ajli ya assignment
Mkuu wa kitengo akishapelekewa ataasign mchunguzi ni kwa ajili ya kumantain chain of custody baada ya mkuu wa kitengo kumuassign mchunguzi ataondoka na jalada na vielelezo hivyo.
Mchunguzi akiondoka na vielezo hivyo vinaenda kufanyiwa kazi anasema hapa ofisi yao inafanya kazi mtindo wa FIFO First in First Out yaani kilichoanza kuja ndiko kitafanyiwa kazi
Kanuni ya FIFO ikizingatiwa mchunguzi ataanza kuja na ataendelea na uchunguzi wake uchunguzi unafanyika katika njia kuu 3
Wakipokea kielelezo cha picha mjongeo au video utaratibu unakuwa hivi
Part 111 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 105
Mhe. Lissu: Kwahiyo wewe hufahamu mtu anayeteua Mawaziri nchi hii wewe humfahamu?
Kaaya: Mawaziri wanateuliwa na Rais.
Mhe. Lissu: Kwahiyo Mohamed Mchengerwa ni mteule wa Rais Samia? Huyo ni waziri wa TAMISEMI.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli au sio kweli ni Waziri ambae anatoa tangazo la uchaguzi na ratiba yake ya huo uchaguzi wa serikali za mitaa?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo ambao ni returning officer ni wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali?
Kaaya: Sijui.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli Wakurugenzi wote wa halmashauri za Wilaya ni wateule wa Rais?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu ; Askari Polisi mwenye cheo cha Inspector hafahamu wakurugenzi wanateuliwa na nani? Vituko na aibu. (Nimechomekea mimi hii)
Mhe.Lissu: Ni kweli kwamba watumishi wote wa serikali za mitaa wanaohusika na uchaguzi wa serikali za mitaa wanafanya kazi kwa niaba ya Rais au maelekezo ya Rais?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kwa maelfu walienguliwa na kuzuiwa kugombea?
Kaaya: Sina uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli baada ya kuenguliwa kelele ikawa kubwa hadi Dr. Nchimbi katibu mkuu wa CCM alielekeza pia warudishwe?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: Ni kweli baada ya kelele zote hizo Waziri wa Tamisemi Mchengerwa aliomba muda uongezwe na kubadili ratiba ya Uchaguzi?
Anasimama Renatus Mkude anasema Mheshimiwa Jaji imefika saa tano kamili naomba turuhusiwe kwenda msibani na tutafikisha salamu za rambirambi pia za Mshitakiwa.
Jaji Ndunguru: Shahidi tukutane kesho saa tatu asubuhi.
Tunaahirisha shauri hili.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 103
Mahakama imetulia sana hata hakohoi mtu baada ya hiyo speech ya Mhe. Lissu.
Watu wameingiwa ubaridi ni kama maneno yamewaingia kila aliyepo hapa.
Jaji amewasha kipaza sauti na kumwambia shahidi uko chini ya kiapo.
Endeleeni.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli hiyo video ya Tarehe 03/04 ilichapishwa kwenye Jambo Tv na mitandao mingine na walichapisha Jambo Tv wenyewe?
Kaaya: Aliyechapisha sifahamu.
😂😂😂 kumbukeni kosa la Lisu ni kuchapisha na kusambaza.
Mhe. Lissu: Ni kweli Mkutano wangu wa tarehe 03/04 ulirushwa mubashara na Jambo Tv?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na ni kweli au sio kweli mimi sina uhusiano wowote na Jambo TV?
Kaaya: Mimi sikufanya upelelezi wa kuhusu wahusika wa Jambo TV ni akina nani.
Mhe. Lissu: Ile Flash Disk XIOXIA yenye rangi nyeupe unaikumbuka ulisema.
Kaaya: ndio nakumbuka
Mhe. Lissu: Je uliandika aina hiyo ya Flash na rangi yake kwenye maelezo yako Polisi?
Kaaya: Sikuandika.
Mhe. Lissu: Umezungumza sana kuhusu video na kuwaonyesha wakubwa zako na kuipakua na kuweka kwenye flash disk umezungumza sana asa waeleze majaji kama umewasilisha hiyo flash disk au hiyo video mahakamani hapa.
Kaaya: Bado sijaiwasilisha.
Mhe. Lissu: Ni sahihi nikisema hakuna mtu aliyeiona isipokuwa wewe hiyo video, Majaji hawajaona, Mawakili hawajaona na mimi sijaona.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu au hufahamu hiyo video vilevile haikuwasilishwa wala kuonyeshwa kwenye committal Kisutu?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi unakumbuka kwenye ushahidi wako ulieleza jinsi ulivyoona hiyi video na kutoa taarifa kwa mkuu wa kitengo?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kwenye maelezo yako Polisi au hapa Mahakamani ulimtaja huyo Mkuu wako wa kitengo kwa jina?
Kaaya: Sikumtaja.
Mhe. Lissu: Unakumbuka nilikuuliza maswali mengi juu ya kesi mbalimbali zilizofunguliwa na watu tofauti tofauti kuhusu masuala ya Katiba na mabadiliko yake.
Kaaya: Nakumbuka.
Mhe. Lissu: Waelelze majaji kama unafahamu au hufahamu kwamba tarehe 13/06/2023 Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Wananchi ilitoa uamuzi kwamba Serikali ya Tanzania ibadilishe sheria ya Uchaguzi ili kuhakikisha sheria za uchaguzi zinakuwa za haki kwenye kesi ya BOB CHACHA WANGWE.
Ni kesi ya Bob Chacha Wangwe akiwa na Legal and Human Right Center wakiwashitaki AG, Tume ya Uchaguzi. Alikuwa anawapa full citation hapo majaji anawatajia na namba ya kesi hiyo.
Mhe. Lissu: sasa kuzuia uchaguzi ni uhaini mnasema hivyo kwenye ushahidi wako ulieleza kuzuia uchaguzi bila kufuata utaratibu wa kisheria kama vile kupata amri ya mahakama ni kuitisha serikali.
Kaaya: Nakumbuka.
Mhe. Lissu: Utaratibu huo wa namna ya kuzuia uchaguzi upo katika sheria gani?😂
Kaaya: Sifahamu.
Ushahidi ni kazi sana jamani.
Leo kumbukeni kuna ile kesi yetu pia niliyofunguliwa na Viongozi wa Chama ndio inaanza muda huu ila Mimi siendi wataingia Mawakili wetu kwa niaba yetu.🤦🏾♀️
Mhe. Lissu: Katiba unaifahamu shahidi?
Kaaya: Ndio naifahamu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama upo utaratibu wa kuzuia uchaguzi mkuu?
Kaaya: Haupo. Haujaanishwa kwenye Katiba.
Mhe. Lissu: kwahiyo utaratibu haupo?
Kaaya: Zipo sheria zingine lakini.
Mhe. Lissu: Hivi unaelewa swali langu au unatuchelewesha kwenda kwenye mazishi?
Kaaya: haupo
Mhe. Lissu: Je ni kweli Uchaguzi mkuu wa Tanzania unaendeshwa na inayoitwa Tume Huru ya Uchaguzi?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je ni kweli Katiba inasema tume ni chombo huru na haitakiwi kuingiliwa na Mamlaka au mtu yeyote?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Anasomewa Katiba hapa ibara ya 74(11) kuhusu Tume na uhuru wake na pia anasomewa sheria ya Uchaguzi kuhusu wajibu wa Tume.
Kwamba tume haitakiwi kupokea maelekezo yoyote kutoka serikali wala chombo chochote cha serikali.
Kaaya: Ni sahihi.
Part 104 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 15, 2025.
Last time tuliishia part 101 so leo tunaendelea na
Part 102
Leo Tarehe 15/10/2025.
Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia Mahakamani.
Amesimama Kizimbani anauliza Polepole amepatikana na Mama anasemaje si Balozi wake?
Majaji wameingia na Shahidi nae kama kawaida ameingia yupo hapa. Inspector wa Polisi John Kaaya.
Karani anasimama Criminal Session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Iwapendeze naitwa Renatus Mkude Wakili wa Serikali niko na Job Mrema, Ignas Mwinuka, Harrison Lukosi, Winiwa Kasawa tunaiwakilisha Jamhuri. Na Mshitakiwa yupo. Lakini pia tuna jambo tunaomba kuiambia Mahakama.
Mhe. Lissu anasema na mimi niko tayari na pia nitakuwa na jambo la kuieleza Mahakama.
Renatus Mkude, tulipokea taarifa ya Msiba wa Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga.
Tumekuwa na utaratibu wa kwenda kushiriki matukio kama haya na tulipanga kuhudhuria kwenye msiba huo kwa vile ni jambo la kibinadamu ilikuwa na rai yetu itakapofika saa tano twende tukamuage huyu ndugu yetu ili tuendelee kesho tena. Ni hayo tu.
Mhe. Lissu anasimama kwenye hilo mimi sina pingamizi lolote na ikiwapendeza wakienda kwenye huo msiba wanipelekee salamu zangu za rambirambi kwa wafiwa.
Lakini pia niwaeleze kuhusu watu waliokuwa wanazuiwa kuingia Mahakaman, nimesema sana jambo hili.
Kasoro juzi Jumatatu sikulizungumzia kwasababu niliambiwa wangeruhusiwa siku hiyo lakini walikuja wakazuiliwa hapo getini.
Kwa taarifa nilizonazo walichukuliwa na maafisa wa uhamiaji na baadae wakafukuzwa nchini ili wasiweze kuingia Mahakamani kushuhudia kesi hii.
Sasa waheshimiwa majaji hii ni mara ya tatu kwa watu wanaotaka kuja kuhudhuria mahakama hii kufukuzwa nchini.
Walianza na Ujumbe uliotoka Kenya ukiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Kenya, Willy Munyoki Mutunga.
Wakafuata Boniface Mwangi na Agatha Atuhire walikamatwa na kuteswa na kupelekwa mipakani na kutupwa.
Na sasa hili limetokea kwa raia wa Ujerumani na Marekani walioingia nchini kihalali kuja kutaka kuona kinaendelea nini.
Hii ni kesi kubwa kuliko zote ndivyo inasema Katiba yetu ni kesi inayo draw Regional and International attention.
Haya yaliyofanyika Kisutu tayari yapo kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa yapo katika mahakama za haki za binadamu na watu Afrika.
Kwahiyo haya sio mambo madogo kabisa. Mahakama inapoingiliwa inasababisha sintofahamu kwenye mfumo wetu wote wa haki jinai ndani ya Taifa letu.
Mwaka 1958 kulikuwa na kesi kubwa sana katika Mahakama ya Wilaya Dar es salaam Kivukoni ambayo ni Regina Vs Julius Nyerere na wenzake wawili mmoja wapo Robert na mwingine Rashid baldell.
Wakoloni wa kingereza did not dare kuzuia watu kwenda kushuhudia kesi ya kiongozi wao na wanaofahamu historia ya nchi hii Mwalimu alitetewa na Wakili kutoka Wingereza.
Wakoloni hawakukataza pia hawakupiga watu wasiingie Mahakamani.
Kesi ya Jommo Kenyata pia ilikuwa kubwa sana ambayo ilifanyika katikati ya Vita vya Maumau, Waingereza did not dare kuzuia watu kwenda kusikiliza the trial of Jomo Kenyata ilifuatiliwa.
Mwaka 1956 mpaka 1961 tulikuwa na kesi ya Uhaini Afrika Kusini imeelezwa kwenye Long Walk to Freedom, Kesi ya Nelson Mandela hakuna mtu aliyepigwa wala kuzuiwa kwenda Mahakamani, hakuna watu walioteswa ili wasiingie Mahakamani.
Sasa nchi hii baada ya miaka 64 ya Uhuru Serikali yetu na vyombo vya Ulinzi na Usalama inazuia watu wasiingie Mahakamani kwenye nchi ambayo sheria zinasema mahakama ni ya wazi.
Tunafanya mambo ya hovyo kuliko wazungu waliotutawala sisi hapa Tanganyika, walioitawala Kenya na wale wa Afrika Kusini sasa mimi niko Gerezani na Mahakama imeshindwa kufanya lolote.
Sasa ili isije kuja kusemwa baada ya mimi na nyie majaji kutoweka hapa Duniani kuwa nilikuwa kwenye dhambi ya watu ambao walinyamaza kimya mambo haya kutokea. Nimesema kutimiza wajibu wangu na sitaki dhambi ya kunyamazia uovu au maovu, naomba kumalizia hapo.
Part 103 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 101
Kaaya: Sijaidentify kama ni kosa la uhaini.
Mhe. Lissu: Pia unasema nilisema mkutano wetu unasema NO reforms no election na tutahamasisha uasi ili kuzuia uchaguzi ni uhaini?
Kaaya: Ni kosa.
Mhe. Lissu: Mtu anayetaka kuzuia uchaguzi kwa maandamano au migomo au njia nyingine yoyote isipokuwa kumuua Rais. Je ni kosa gani?
Kaaya: Tuzungumzie maelezo yote kwa pamoja.
Mhe. Lissu: Kuzuia uchaguzi ni kosa?
Ngoja nikutaftie sheria hapa unadhani kuwa mwanasheria ni miezi 6 kama ya CCP Moshi kile Chuo cha Polisi. Sheria sio rahisi hivyo.?
Sasa nimepata sheria ya wabunge na madiwani isome sheria hiyo.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa kesho ni sikukuu na imeshafika saa 11 na jioni kwahiyo naomba tuishie hapo.
Mhe. Lissu: Kesho ni Sikukuu gani mimi sifahamu niko jela.
Jaji: Nyerere Day na tunaahirisha hadi tarehe 15/10/2025 kesho kutwa, naomba tukutane saa tatu asubuhi.
Mhe. Lissu: Shahidi nakusubiri sana kesho kutwa hiyo.
Courtttttttt tumetoka!
Tutaendelea kesho kutwa!
Naomba Repost yako