VIDEO:
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema wanaomsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ndio hao wanaoongoza kwa kumhujumu na kufanya uovu.
Mpina ametoa kauli hiyo wakati akiwa ziarani jimboni humo ambapo amebaini ubadhirifu wa fedha za miradi ya ujenzi wa shule ambazo hazionekani kutekeleza miradi, huku kukiwa na udanganyifu katika uidhinishaji wa malipo pamoja na kumsajili mkandarasi hewa, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ndiye anayedaiwa kuhusika katika hayo.
"Huyu mtu kama ni kukamatwa akamatwe atumie mafungu yake alipe hizi fedha za umma jumla ya shilingi milioni 402 ziletwe."
"Huyu Mama Rais wetu Samia Suluhu Hassan watu wanapenda tu kusema maneno, Rais wetu tunampenda, nani kama Samia huku wanamhujumu usiku na mchana, fedha zinaliwa halafu aliyekula hizo fedha ndio wa kwanza kufanya makongamano eti ya kumpongeza Rais na kumwombea ili kuficha uovu, akizungumza neno moja 'Mama Samia' utadhani ni mwema mno, hawa akina Mpina wanaosema wanageuzwa wao ndio maadui wa Rais," amesema Mpina.
VIDEO:
โKuna jambo ambalo limeendelea ambalo limefunikwa kwa kiwango fulani na mjadala mkubwa juu ya uchaguzi wa ndani ya CHADEMA, lazima nilitolee kauli kwa ufupi sana leo, juu ya mchakato unaoendelea kufanywa na Tume ya taifa ya uchaguzi kutunga kanuni za uchaguzi wa Ubunge, Rais na Madiwani wa mwaka 2025. Na sisi walitupa rasimu hizo kanuni na walitupa mpaka tarehe 30 Disemba tuwe tumepeleka maoni kwao.โ
โKatibu Mkuu nimemuandikia Mkurugenzi wa Tume huru ya taifa ya uchaguzi, kumtaarifu kwamba sisi hatukubaliani na huu utaratibu wa kuanza kuandika kanuni kutoa hii kanuni na kutaka maoni ya wadau kabla kwanza hayajafanyika marekebisho ya kikatiba na kisheria.โ โ Mnyika.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Chama hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam, tarehe 7 Januari, 2025.