Pichani ni Rais Samia akishiriki Mkutano Maalum wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Dar es Salaam tarehe 07 Juni, 2024.
Mitandao imekua nyenzo muhimu sio tu ya mawasiliano bali kama kifaa cha utendaji kazi. Natamani kuona mikutano mingi zaidi ikifanyika kwa njia hii.
Nimewasili nchini Korea Kusini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Yoon Suk Yeol. Korea ni moja ya washirika wetu wakubwa wa maendeleo tangu tulipoanza nao rasmi uhusiano wa kidiplomasia tarehe 30 Aprili 1992.
Uhusiano wetu na Korea umegusa maisha ya wananchi moja kwa moja na lazima kuendelea kufanya kazi ya kuukuza na kuuongezea tija zaidi. Baadhi ya miradi mikubwa ambayo tumeshirikiana na Korea kuifanikisha ni pamoja na Daraja la Mto Malagarasi, Daraja la Tanzanite na Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila.
Ziara hii ni sehemu ya utekelezaji wa kazi ya Diplomasia ya Uchumi, na baada ya mazungumzo kati yangu na Mheshimiwa Rais, nchi zetu zitasaini makubaliano mbalimbali ya kukuza zaidi uhusiano wetu yakigusa hasa sekta za uchukuzi, uchumi wa buluu, usafiri wa anga, madini ya kimkakati, utamaduni, sanaa na kilimo.
Baadaye nitafanya mazungumzo na viongozi wa kampuni kubwa za Korea kwenye sekta za nishati, miundombinu na uandaaji wa filamu ili kuona namna nchi zetu zinavyoweza kushirikiana kwenye maeneo haya ikiwemo kukuza teknolojia, utalii, kuwekeza katika studio za filamu nchini na ujenzi wa Chuo cha Filamu cha Taifa (Tanzania National Film Academy).
Kabla ya kuhitimisha ziara nitashiriki Jukwaa la Afrika na Korea (Korea-Africa Summit) linalowaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika na Serikali ya Korea. Nitahutubia jukwaa hilo na kushirikishana uzoefu na mikakati katika usalama wa chakula na madini.
On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to His Excellency @narendramodi on being re-elected as the Prime Minister of the Republic of India. I am looking forward to continue working with you in strengthening India-Tanzania relations, and advancing our strategic partnership.
Baada ya mikutano mbalimbali ya kazi katika ziara yangu nchini Korea nilipata wasaa wa kukutana na kuzungumza na ndugu zetu Watanzania waishio nchini humo, baadhi wakiwa na familia zao.
Nimefurahi kuona imani na juhudi zao za kuendelea kuwekeza nyumbani, na kuwahakikishia kuwa tutaendelea kufanya kazi ya kuweka mazingira bora ya wao kufanya hivyo, ili kutimiza nia yao ya kuchangia kwenye maendeleo ya nchi yetu.
TAARIFA SAHIHI KUHUSU MKOPO WA TRILIONI 6.8 AMBAO TANZANIA UMEUPATA KUTOKA KATIKA SERIKALI YA JAMHURI YA KOREA.
Mkopo huu ambao Tanzania imeupata ni mkopo wa Dola 2.5 bilioni ambao ni mkopo wa masharti nafuu ili kufadhili miradi muhimu ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia Mwaka (2024 hadi 2028).
Mkopo huu ni sehemu ya makubaliano katika awamu ya pili ya ushirikiano wa miaka mitano ijayo. Ni mkopo wa masharti nafuu utakaolipwa katika miaka 40 kuanzia mwaka wa 26 kwa riba ya 0.01%.
Faida za mkopo huu kwa Tanzania ni kama zifuatazo:
1. Kufadhili Miradi ya Maendeleo Muhimu. Mkopo huu utasaidia kufadhili miradi muhimu ya maendeleo kama miundombinu, elimu, afya, na nishati. Hii itaboresha huduma za kijamii na kuinua kiwango cha maisha cha wananchi.
2. Kukuza Uchumi: Uwekezaji katika miradi ya maendeleo utachochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza ajira, kuboresha mazingira ya biashara, na kuvutia uwekezaji wa kigeni.
3. Masharti Nafuu: Mkopo huu ni moja katika ya mikopo ambayo una riba ya chini sana ambayo ni 0.01% na muda mrefu wa kulipa ambao ni miaka 40. Hii itapunguza mzigo wa deni kwa serikali na kuruhusu matumizi bora ya rasilimali za kifedha.
4. Kuimarisha Ushirikiano wa Kimataifa: Makubaliano haya yanaimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania na Korea Kusini, ambayo inaweza kufungua milango kwa fursa zaidi za ushirikiano na msaada wa kiufundi.
5. Kuboresha Miundombinu: Miradi inayofadhiliwa na mkopo huu inaweza kujumuisha ujenzi wa barabara, madaraja, na mifumo ya maji na umeme, ambayo ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya taifa.
6. Kuimarisha Huduma za Kijamii: Ufadhili wa miradi ya afya na elimu utaboresha huduma za kijamii, kupunguza umasikini, na kuimarisha uwezo wa kitaalamu wa wananchi.
7. Kuwezesha Ukuaji wa Maendeleo: Mkopo huu utatoa msingi imara wa maendeleo endelevu kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati.
Kwa ujumla, mkopo huu utakuwa na matokeo chanya kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania, na kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu na mkopo huu utamnufaisha kila mmoja.
Muone @jacquemaline kwa pochi kali zenyye quality ya hali ya juu . Leo nimefika na kujipatia yangu . Sasa nipate gigs ili ninunue clutch na Vingine . Duka lake liko Mwenge karibu na KKKT .