Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa onyo kwa Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya kufuata utaratibu wa Bunge wa kuacha kuzungumza bungeni bila kibali cha spika.
Mwanamuziki wa bendi ya FM Academia, Malu Stonch aliyefariki baada ya kuanguka ghafla jukwaani, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, atazikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kwa Kondo yaliyopo Ununio.
Mwaka wa fedha 2022/23 imetoa Sh Bil16.5 kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali kongwe 19 ambapo kwenye mwaka wa fedha 2023/24 kiasi cha Sh Bil 27.9 kilitengwa kukarabati hospitali kongwe 31 zilzobaki ikiwemo Hospitali ya Magunga Mji wa Kongwe ambayo imetengewa Mil 900.
Kutoka Nigeria Rema aliamua kususia tamasha la Dreamville la 2024 ambalo limefanyika huko North Carolina siku ya jana Jumapili baada ya kuchukizwa udhaifu wa sauti(Sound) hivyo akaamua kuondoka jukwaani.
Bondia matata Kanda ya Ziwa kutoka Manispaa ya Kahama, Shinyanga, Issa Salum James [Issa Simba], amepanda viwango na kuwa bondia namba pili Tanzania kwenye uzito wa Super lightweight, nyuma ya kinara Tony Rashid wa Dar es salaam.
Rapa kutoka Marekani, J. Cole amemuomba radhi rapa Kendrick Lamar kwa kum-diss kwenye β7 Minute Drillβ.
J. Cole alilazimika kukatiza kutumbuiza kwenye onyesho lake kwenye Tamasha la Dreamville la 2024 huko North Carolina siku ya jana Jumapili ili kumwomba Lamar msamaha.
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo ambaye kwa sasa ni RC mpya wa Arusha, Paul Makonda tayari amepokelewa Jijini Arusha mapema leo hii anarajiwa kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Ndg. John Mongella ambaye kwasasa ni Naibu Katibu Mkuu CCM.
Watu zaidi ya 90 wamepoteza maisha nchini Msumbiji, baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama hapo jana kwenye mkoa wa Nampula, wakielekea katika kisiwa kilichoko karibu na mji wa Lumbo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limethibitisha kuwakamata watu 17 raia kutoka nchini Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila ya kufuata utaratibu ikiwemo kutokuwa na vibali.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza kuwa mchezo kati ya Yanga na Simba maarufu kama Kariakoo Derby utapigwa ifikapo Aprili 20 mwaka huu ndani ya dimba la Mkapa majira ya saa 11:00 Jioni
Msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Malu Stonch amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi.
Malu alianguka ghafla jukwaani katika ukumbi wa Target uliopo Mbezi Beach wakati akiimba pamoja na bendi yake anayofanya nayo kazi ya FM Academia.