Ni mwaka mmoja umepita Humphrey Polepole ametuachia ujumbe mzito wa mwisho tusisahau kuwa wenye mamlaka ni sisi wananchi na TUNA WAJIBU wa kupinga dhulma, ufisadi na kulinda nchi
Mwezi huu ninaanza mazungumzo ya kitaifa tujadili masuala muhimu kuikomboa nchi
#OngeaNaShangazi itakuwa live kupitia @MwanzoTvPlus na @MwanzoTV na kupitia social media akaunti zangu
Karibuni!
UCHAMBUZI WA KISHERIA KUHUSIANA NA OMBI LA WAKILI KATUGA:
Kwenye hili, nitazingatia mbinu za kisheria (legal tactics) na mchezo wa kisiasa (political chess) tuliouona kati ya DPP na TAL.
Iko hivi:
Katuga amejaribu kutumia tafsiri ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) kama silaha ya kimkakati dhidi ya TAL.
SUALA LA KWANZA - Kwa nini KATUGA anasisitiza "mwanya wa kisheria" (Loophole) ya kifungu kidogo (d)?
Uandishi wa kisheria (legal drafting) wa maneno "shall be liable to", yenye maana ya (atawajibika/atastahili adhabu ya...) Katuga alisisitiza hii 'LOOPHOLE' wakati anamhoji Lissu (cross-examination) na kwenye majumuisho yake ya mwisho (final submission), halikuwa jambo la bahati mbaya. Huu ni mkakati wa kisheria wenye malengo mawili:
A). Kuwajengea majaji NJIA YA KUTOKEA (Soft Landing): Katuga anajua fika kuwa kutoa adhabu ya kifo kwa kesi ya kisiasa na ya "MANENO MATUPU", tena kifungu kikiwa tested kwa mara ya kwanza, itasababisha mtafaruku mkubwa wa kijamii, kulaaniwa & kukosa sapoti kimataifa. Hivyo basi, kwa kusisitiza busara ya mahakama (judicial discretion) kupitia maneno "liable to", Katuga anaiaminisha mahakama kuwa inaweza kumkuta Lissu na hatia lakini ikampa adhabu mbadala (kama kifungo badala ya kunyongwa), na hivyo serikali kuonekana "ina huruma."
B). Kuhakikisha Ushindi wa Kisiasa wa Upande wa Mashtaka: Lengo kuu la kesi za namna hii mara nyingi si kumuua mshtakiwa, bali ni kumfunga kisiasa (political neutralisation). Lissu akipatikana na hatia na kupewa kifungo cha maisha au miaka kadhaa, upande wa mashtaka utakuwa umeshinda kisheria, na Lissu atakuwa amepoteza sifa za kugombea uongozi; na kama atakuwa gerezani kwa muda, maana yake 2030 CHADEMA ipataswa ichague Mwenyekiti mpya.
SUALA LA PILI - Tundu Lissu akauona huu mtego kitambo: "ninyongwe au niwe huru"
Lissu, kama mwanasheria mbobezi na mwanasiasa mwenye mipango na ajenda za kimkakati, ameliona hili na ndio maana amekataa kata kata "adhabu ya katikati" (compromise sentence). Msimamo huu wa Lissu una mantiki kubwa mbili:
A). Kuharibu mkakati wa "kumpunguza kasi" akapendekeza (All or Nothing Strategy): Lissu anajua kuwa kukubali uwepo wa adhabu ya katikati ni kuwapa majaji nafasi rahisi ya kumtia hatiani. Kwa kulazimisha kuwa chaguo ni ama KIFO au UHURU, TAL akaona aiweke mahakama na serikali kwenye kona mbaya sana kisheria. Hapa, mahakama italazimika kufikiria mara mbili: Je, tuko tayari kumhukumu kifo Lissu kwa sababu ya MANENO TU na kukabili gharama za kisheria, kisiasa, kidiplomasia na machafuko ya ndani ya nchi?
B). Kuhifadhi HADHI ya Kesi kama ya Kisiasa: Lissu anataka kuonyesha Umma & Dunia kuwa kesi hii haina nia njema ya kisheria bali ni ya kisiasa. Hivyo basi, Serikali ikishindwa kumnyonga, italazimika kumuachia huru, na hivyo yeye kuibuka mshindi mkubwa wa kisiasa (political martyr).
SUALA LA TATU - Mtazamo wa Kihistoria na Hatma(maamuzi) ya Kesi za Uhaini ndani ya Tanganyika.
A). Jaji Mkuu Philip Telford Georges (1970) katika kesi ya Grey Mataka na Bibi Titi, na Jaji Kiongozi Nassor Mnzavas (1985) katika kesi ya Hatibu Gandhi, Kapteni Eugene Maganga na wengine, walitumia busara hii hii ya kisheria kuepuka KUMWAGA DAMU & KUTENGWA na Dunia.
HITIMISHO:
Hata hivyo, changamoto kubwa ya kesi hii ni kwamba, hii ni kesi ya kwanza ya uhaini inayotokana na MANENO PEKEE, tofauti na kesi za nyuma zilizohusisha njama, silaha, vikosi vya jeshi (JWTZ), au majaribio ya mapinduzi ya kijeshi.
Kutokana na UHALISIA huo & pia kwa kuzingatia udhaifu wa ushahidi wa DPP na dosari za kisheria katika uwasilishaji wa mashtaka, mahakama itapaswa kulinda HADHI yake. Hivyo, kuna uwezekano MKUBWA kuwa mahakama itajiepusha kuingia kwenye historia mbaya.
Kutokana na msimamo wa kisheria, maamuzi ya kihistoria & ufikiri wangu binafsi, niungane na walio wengi kuamini kuwa, majaji wa kesi hii watatumia hekima ya JUU ZAIDI kulinda misingi ya haki na utawala wa sheria nchini.
TUSONGE MBELE & TUSIKATE TAMAA.
#BabaMwita ⚖️
"[kufuatia mauwaji ya Oktoba 29], kuna waliozika ndugu, waliozika nguo badala ya watu.. maana yake unatafuta ndugu humuoni unaenda kuzika kofia yake... jamani mambo ni mabaya! Tukubaliane ndio twende mbele." - Dkt Helen Kijo-Bisimba.
Dola katili la CCM lilienda Kisutu kimyakimya kuomba Edger @Sativa255, Maria Sarungi na Mange wakamatwe warejeshwe TZ. Mliona mbwembwe zao humu!
Sativa alipinga uamuzi huo High Court.
Jana imeamuriwa kuwa mwenendo, uamuzi na amri ya kukamatwa & kurejeshwa TZ Sativa ni BATILI!
𝐀 𝐐𝐔𝐈𝐂𝐊 𝐒𝐔𝐌𝐌𝐀𝐑𝐘 𝐀𝐍𝐃 𝐄𝐋𝐀𝐁𝐎𝐑𝐀𝐓𝐄𝐃 𝐓𝐔𝐍𝐃𝐔 𝐋𝐈𝐒𝐒𝐔’𝐬 𝐂𝐋𝐀𝐒𝐒𝐈𝐂𝐀𝐋 𝐅𝐈𝐍𝐀𝐋 𝐒𝐔𝐁𝐌𝐈𝐒𝐒𝐈𝐎𝐍
Jana, Tundu Lissu alimaliza kutupa karata yake ya mwisho kujinasua na mashtaka ya uhaini dhidi yake kwa a very classical final submission iliyomchukumua muda wa siku nne kuiwasilisha.
HUYU KATUGA NI NGULI WA SHERIA 🙌
Uzi🧵
KATUGA: Sisi kwa pamoja tunaiwakilisha Jamhuri.
Mshtakiwa yupo mbele yenu.
Waheshimiwa Majaji, shauri leo limekuja kwa ajili ya kuleta mawasilisho, specific kwa upande wa Jamhuri kuleta mawasilisho.
Upande wa Jamhuri tupo tayari.”
Jaji Ndunguru:
“Mshtakiwa?”
Lissu:
“Waheshimiwa Majaji, nipo tayari.”
Jaji:
“Tuendelee upande wa Mashitaka.”
Nassoro Katuga:
“Naomba kutoa ahadi, Waheshimiwa Majaji, kwamba tutakuwa na mawasiliano ambayo si marefu.
Tuta-focus na shauri lililopo mbele yetu.
Waheshimiwa Majaji, nitaanza tu submission. Naitwa Nassoro Katuga.
Waheshimiwa Majaji, mshtakiwa ameshtakiwa kwa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, Urekebu wa Mwaka 2022.
Ambapo, Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na taarifa ya shitaka hili, inaelezwa kwamba tarehe 23 Aprili 2025, ndani ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa chini ya utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitengeneza nia ya kuchochea umma kuweza kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa nia ya kuitisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (for the purpose of intimidating the Executive), kwa kudhihirisha nia hiyo kwa kutoa maneno yafuatayo:
‘Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi: Msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli, ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi, hiyo ndiyo namna ya kupata mabadiliko. Kwa hiyo tunaenda kukinukisha, huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana.’
Haya maneno ndiyo Jamhuri imeleta mbele yenu, mbele ya sheria kuyaangalia.
Kwamba maneno haya ndiyo, Waheshimiwa Majaji, tunatuhumu au kutafsiri in favour of the Republic.
Kwamba mshtakiwa alitoa maneno haya kwa nia ya kuitisha Serikali ili apate mabadiliko, ambayo aliyetafsiri ni ‘mabadiliko’.
Waheshimiwa Majaji, kifungu ambacho nimekirejea cha 39(2), upande wa Jamhuri tulikifanyia research kama Mahakama ilishawahi kuki-test.
Tafiti zilionyesha kwamba Mahakama zetu katika mashauri ya uhaini ni mashauri ambayo yalishitakiwa chini ya kifungu cha 39(a).
Waheshimiwa Majaji, samahani, kama itawapendeza, naomba nimuingize Job Mrema katika kolamu ya upande wa Jamhuri. Alikuwa amepata dharura, sasa amefika.
Katuga: Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa tumejiridhisha kwamba haijawahi kutumika katika Mahakama zetu, tuweze sasa kutafsiri hati ya mashitaka pamoja na kifungu kilichotumika cha 39.
Ili kuweza kuona ni vitu gani Mahakama yenu Tukufu ilianza kuangalia ushahidi, basi ni kitu gani upande wa Jamhuri ulipaswa kuthibitisha.
Naomba kwa kuanza kuwaalika katika kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Kifungu chenyewe kinasema:
‘Mtu yeyote ambaye yupo chini ya utii, awe Tanzania au nje ya Tanzania, atengeneze nia either kufanyika au kusababisha kufanyika au kutengeneza nia ya kuchochea.’
Kwa mujibu wa kifungu cha 135 cha CPA, Sura ya 20, Urekebu wa Mwaka 2023, kinaelezea kwamba mashitaka lazima yawe na maelezo ya kosa la shitaka husika pamoja na maelezo ya shitaka.
Ambayo sheria inasema hayo maelezo lazima yatie information ya jinsi shitaka lilivyofanyika.
Lakini kifungu cha 138(a)(iii) kinaelekeza kwamba technical terms hazitakiwi kutumika.
Inatakiwa itumike ordinary language, lugha ya kawaida.
Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, mtaona kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d), kinaelekeza kwamba ili mtu ashitakiwe kwa kosa la uhaini la aina hii:
Kwanza ni lazima awe mtu mwenye utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwetu ilichukua mshtakiwa ni mtu wa Jamhuri ya Tanzania akiwa Tanzania, tukaacha ‘elsewhere’.
Hati yetu ya mashitaka ikachukua ‘forms an intention to instigate’ — nia ya kuchochea.
Tukaachana na maneno ‘forms’ zingine za ‘intention to defect’.
Ikaachana na ‘intention to persuade’, ‘to counsel’, ‘to...’
‘Intention to instigate the public’ — umma kwa ujumla wake, nitaeleza hapa kwa nini.
Hati ya mashitaka ikaeleza watu wamechochewa kufanya nini.
Mshtakiwa akichochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 — General Election, Waheshimiwa.
Waheshimiwa Majaji, hati yetu ya mashitaka imeachana na neno ‘deed’, ikachukua neno ‘for the purpose of intimidating the Executive’.
Na hapa ikaachana na maneno ‘intimidating Legislature’ na ikachukua ‘intimidating the Executive’.
Ukiendelea na hati ya mashitaka, ile nia ya mshtakiwa kudhihirisha nia yake...
"Nimepigania haki kwa sehemu kubwa ya maisha yangu ili kuwe na nchi ya demokrasia, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi. Msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu nitaendelea kuusimamia, kama ikibidi KUFA nipo tayari KUFA".
Tundu Lissu. 28/09/2026.
"Nimepigania haki kwa sehemu kubwa ya maisha yangu ili kuwe na nchi ya demokrasia, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi. Msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu nitaendelea kuusimamia, kama ikibidi KUFA nipo tayari KUFA".
Tundu Lissu. 28/09/2026.
“Nimepigania haki na demokrasia katika nchi hii kwa sehemu kubwa ya maisha yangu. Kuwa na nchi ya kidemokrasia, inayojali haki za watu wake, inayojali utu wa binadamu, imekuwa ni ideal ambayo nimeipigania kwa nchi yangu. Msimamo huo umenigharimu sana. Msimamo huo umeniletea madhila mengi sana. Msimamo huo, kwa siku zilizobaki za maisha yangu kama Mungu akinajalia, ni msimamo ambao nitaendelea kuupigania kwa siku zilizobaki za maisha yangu. Na kama ikibidi kufa, ni msimamo ambao nipo tayari kuufia.” — Tundu Antiphas Mughwai Lissu, Mahakama Kuu ya Tanzania, 28 September 2026
@cw_pedro Huyu Mpumbavu haijui hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Jinga na mkia wake!
Ndiyo maana akili zinamtuma kusema HADHARANI mambo yake ya ndani!
DGIS nao ni 'wajumbe wa kamati kuu ya CCM'. Kinyume kabisa na KATIBA ya Jamhuri. Mwaka jana ndio waliomuweka madarakani Samia. Mwalimu Nyerere afufuke leo, asimuliwe yaliyofanyika kwenye chaguzi zetu tangu mwaka 2016, atarudi kaburini haraka sana.
TUNAFUNDISHWA kufaulu na walimu ambao walifeli.
Walimu wetu wa bishashara kwenye mitandao ya kijamii hawajawahi kuuza hata kijiko.
Wachungaji wanaotufundisa mahusiano? Wao wenyewe ndoa ziliwashinda. Watoto wao hawataki hata kusikia kitu inaitwa uchungaji.
Asilimia tisini ya wanaofundisha "Namna ya Kutunza Ngozi Yako" hawajui hata neno dermatology lina maana gani. Utasikia, "kama ngozi yako ina mafuta, tumia 'selam' au 'krinsa' 😂
Wataalam wa gardening.
Wataalam wa savings.
Wataalam wa investment na government bonds.
Wataalam wa malezi
malezi.
Wataalam wa indoor deco.
Kwenye Neno la Mungu ndo usiseme.
Wataalam wa mapishi.
WALIO WENGI NI WAONGO WAONGO TU.
Wanauza bidhaa tofauti na ile wanayokufundisha.
Cha kushangaza:
Siyo wengi wanafundisha maadili.
Siyo wengi wanaofundisha uaminifu.
Siyo wengi wanaofundisha nidhamu.
Siyo wengi wanafundisha kujituma, kuamka mapema na kuwajibika.
Siyo wengi wanaofundisha professionalism.
Siyo wengi wanaofundisha customer care nzuri na tabasamu kwa mteja, hata kama umeamka vibaya.
Siyo wengi wanaokemea attitudes mbaya-mbaya (mbovu) ofisini, dukani, wala sokoni. Kuna tudada tuna attitudes nyie. Ooh!
Tunafundisha mambo mepesi, tunapuuzia mambo magumu tanayoweza kuleta mabadiliko.
Hii ni kauli muhimu sana, imethibitisha yale ambayo tumeyasema kwa miaka yote.
Leo kiongozi wa juu wa ccm ametibitishia Watanzania na Dunia kwamba . Kwa wale waliokua wanafikiri tunasema uongo au tunawazushia.. polisi, usalama wa Taifa na jeshi la wananchi wamsikilize bwana Chacha.
Vyombo vya ulinzi na usalama ni mali ya ccm na hao viongozi wa vyombo hivyo ni wanachama na makada wa ccm.
Maswali muhimu ya kujiuliza, je vyombo vya ccm, polisi, usalama wa Taifa na JWTZ kama alivyosema bwana Chacha vinaweza kutendea haki wapinzani wa ccm?
Je ni halali kwa Watanzania mamilioni kulipa kodi ambazo zinatumika kuhudumia vyombo vya dola ambavyo ni vya ccm?
Chama chetu kitasema kwa undani kuhusu jambo hili na kutoa msimamo kamili, kwasasa tuelewe.
1. No reforms no Election ilikua muhimu sana ili kubadili hali ya vyombo hivi kuwa mali ya chama kimoja katika Nchi ya vyama vingi..
2. Kesi ya Mwenyekiti wetu ni ya uongo amebambikiziwa na vyombo vya ccm kwasababu ya kulinda chama chao dhidi ya ushindani wa kweli kutoka kwake na chama anachokiongoza.
3. Katika mazingira haya aliyoyasema Chacha haitawezekana kwa Mwenyekiti wetu kutendewa haki, kwasababu hivi vyombo vya ccm haviwezi kumtendea haki mwanachadema..
4.Tuhuma za kuua watu, kuteka, kupoteza zinazofanywa na vyombo vya dola ni kwaajili ya kuisaidia ccm kujitangaza washindi kwa njia ambazo sio halali.
5. Wanachama wa ccm hawafiki hata milioni 5 Nchi hii. Watanzania wako milioni 60, kwanini vyombo vya watu milioni tano vilipwe na kuhudumiwa na Watanzania wote kwa maslahi ya watu million 5.
Lazima tupate katiba mpya sasa.