Ifahamike kwa watanzania kwamba; kinachothibitisha UMILIKI wa nyumba, SIYO HATI PEKEE, bali ni MCHAKATO HALALI WA UPATIKANAJI WA HATI HIYO. Kama HATI ilipatikana KIMAGUMASHI, umiliki wa nyumba HAUWEZI KUWA HALALI.
Magari waliyopewa vyama vya mfukoni kufanyia kampeini ni rushwa..
Lengo ni kujaribu kuhalalisha uchafu huu unaoitwa uchaguzi.
Bajeti ya serikali inapitishwa na bunge, Tume waseme wametoa hizo fedha wapi?
Ni fungu gani la bajeti lilitengwa kununulia vyama vya mfukoni magari, kulipia madereva na gharama nyingine zote.
Ni wajibu wa kila chama kugharamia kampeini zake, sio wajibu wa tume kugharamia kampeini za mtu fulani kwa pesa ya umma.
Huu ni uchafu mwingine mkubwa na wakati muafaka watu watatakiwa kujibu.
Watu hawana maji, madawa wala barabara kwa haraka haraka magari 17 kwa kwa sh milioni 500 ni zaidi ya bilioni 8.5 hivi ni vituo 17 kwa kata 17 katika nchi.
Miradi ya maji inayosumbua na wilaya ikapata maji ya uhakika mingi ni chini ya bilioni 1.5.
Mwanza ziwani hakuna maji unaambiwa matenki madogo, mradi huo unahitaji pesa kidogo zaidi ya hizo watu wapate uhakika wa maji.
Barabara za lami za kawaida ni milioni 500, ina maana ni KM 17 za barabara za mitaa ukiweka pale Mwanza karibia kila mtaa utapata lami..
Kwenye barabara kubwa ina maana ni bilioni 1 kwa km moja hizo ni km 8.5 za lami kwenye barabara kuu.
Kwanini mali za Watanzania zinachezewa kiasi hiki? Kwanini watu wanateseka kulipa kodi alafu pesa ya umma inachezewa kama hakuna mwenyewe?
Watanzania amkeni.