Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu
Hospitalini baada ya kuugua ghafla.
Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015
hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu
HABARI ZOTE KUHUSU VIWANJA VILIVYO ENEO LA ISAMILO KARIBU NA DARAJA LA JP MAGUFULI NI LEO NDANI YA DRIVE MIX
Unajua ardhi inaweza kuwa mtaji wako mkubwa wa mafanikio?
Usikose #DriveMix Jumanne hii π»
π July 08
β° Saa 10 Jioni hadi Saa 1 Usiku
π Jembe FM
Wenyeji wako:
ποΈ Albert G Sengo
ποΈ George Kivumbi
ποΈ Asha Swaleh
π Fuatilia kupitia @jembefmtz na tembelea tovuti yetu ya https://t.co/qGDv5Ra6Oc
#ArdhiMtaji #DriveMix #JembeFM #RealEstate #Investment #MafanikioNaArdhi
RAIS MWINYI:TUDUMISHE AMANI KUELEKEA KATIKA UCHAGUZI MKUU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Waislamu na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuiombea nchi amani na kudumisha mshikamano, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 4 Julai 2025, alipotoa salamu zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu mara baada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Sunna Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Katika hotuba yake Rais Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuwa na dhamira ya kweli ya kudumisha na kuiombea nchi amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa maendeleo yanayoendelea kupatikana hadi hivi sasa yametokana na matunda ya kuwepo kwa amani hapa Nchini.
Rais Dkt. Mwinyi amebainisha kuwa kuirudisha amani inapopotea ni jambo gumu ikilinganishwa na urahisi wa kuitunza na kusema kuwa kuna mifano halisi ya mataifa yanayoendelea kukumbwa na migogoro mikubwa kutokana na kuvunjika kwa amani.
Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwaasa waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi wote kwa ujumla kuendeleza moyo wa mshikamano na kudumisha amani kama msingi wa kila hatua ya maendeleo ya taifa.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa jumla ya wanachama 4,109 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania kugombea ubunge katika majimbo yote 272
ya Tanzania kwa tiketi ya chama hicho.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa
CCM, Amos Makalla, kati ya waliochukua fomu, 3,585 ni kutoka Tanzania Bara huku 524 wakitoka Zanzibar.
Baada ya Miaka 15, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametangaza rasmi kupumzika Ubunge na kuacha kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, mkoani Lindi.
Juni 26, 2025, Kassim Majaliwa alitangaza kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.
Kwa mujibu wa DW, Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha mabilioni ya dola ya ruzuku zinazotolewa kwa kampuni za Tesla na SpaceX zinazomilikiwa na bilionea Elon Musk kufuatia mvutano unaoendelea kati yao ambapo hii ni baada ya Musk kukosoa vikali mswada mpya wa kodi na matumizi ya Serikali unaolenga kufuta ruzuku za ununuzi wa magari ya umeme hatua inayotajwa kuathiri moja kwa moja kampuni ya Tesla.
Trump amenukuliwa akisema kuwa bila ruzuku hizo, Musk atahitaji kufunga biashara na kurudi nyumbani Afrika Kusini, kauli iliyozua mjadala mpana nchini humo na kwa upande wake, Musk hakusita kujibu kwa maneno makali akisema, βZuia kila kitu sasa.β
Aidha mabishano haya yameibuka wakati ambapo Seneti ya Marekani imepitisha mswada huo kwa kura chache tu huku soko la hisa la Tesla likiripotiwa kushuka kwa asilimia kubwa ambayo ni ishara ya wasiwasi kwa wawekezaji kuhusu mustakabali wa kampuni hiyo.
Baada ya Jembe Fm kuripoti kero ya vumbi Barabara ya Kenyata eneo la Chakecheke maarufu kwa mchina.
Afisa Mahusiano wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tano Mwanza-Isaka Bw. Gasper Matumbi ametolea ufafanuzi kero hiyo.
Na @mustaphakinkula
π TZS 3 MILLION WINNER! π
One lucky player just won big in LOTTO PLUS 1 from one of our retailers! π°
Check your ticket now, it could be YOU!
Play now via *149*88# or visit your nearest National Lottery retailer.
π
MSHINDI WA TZS MILIONI 3! π
Mwamba mwenye bahati ameshinda kupitia LOTTO PLUS 1 kutoka kwa wakala wetu! π°
Cheki tiketi yako sasa, unaweza kuwa WEWE!
Cheza sasa kwa kupiga *149*88# au tembelea wakala wa Bahati Nasibu ya Taifa aliye karibu nawe.
Kushiriki ni kuanzia miaka 18 na kuendelea. Cheza Kistaarabu. ITHUBA ni mwendeshaji rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa.
#AminiChezaUshinde #BahatiNasibuYaTaifa #NationalLotteryOfTanzania
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Abdulazizi Abubakar Chende maarufu kama Dogo Janja, amejiunga rasmi kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya Udiwani Kata ya Ngarenaro jijini Arusha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dogo Janja ambaye amezaliwa, kulelewa na kuishi katika kata hiyo amesema sasa ni wakati wa kuwatumikia wananchi kwa kushirikiana nao kuleta maendeleo jumuishi kwa vijana, kina mama, wazee, walemavu na makundi yote maalum yanayohitaji msukumo wa kiuchumi na kijamii.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Abdulazizi Abubakar Chende maarufu kama Dogo Janja, amejiunga rasmi kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya Udiwani Kata ya Ngarenaro jijini Arusha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dogo Janja ambaye amezaliwa, kulelewa na kuishi katika kata hiyo amesema sasa ni wakati wa kuwatumikia wananchi kwa kushirikiana nao kuleta maendeleo jumuishi kwa vijana, kina mama, wazee, walemavu na makundi yote maalum yanayohitaji msukumo wa kiuchumi na kijamii.
Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kada wa chama hicho Esther Bulaya amerejea Chama Cha
Mapinduzi (CCM), na kutangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara kupitia CCM.
Bulaya ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kupitia
CHADEMA amesema alikuwa ndani ya chama hicho kwa mkopo na sasa anarejea nyumbani na kwamba furaha yake ni kuwatumikia wananchi akiwa ndani ya CCM, ambayo ameitaja kama chama chenye dira, maono na dhima ya kweli ya kuwatumikia wananchi.
Esther Bulaya ni miongoni mwa wabunge 19 wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao chama hicho kilitangaza kuwavua uanachama, lakini walisalia bungeni hadi kuhitimishwa kwa Bunge la 12 kwa amri ya mahakama.
Jumanne hii inaweza kuwa siku yako ya bahati! Cheza jakpoti ya LOTTO inayokadiriwa kuwa TZS MILIONI 45 na LOTTO PLUS 1 ya TZS MILIONI 3 kila siku.
Nunua tiketi zako sasa kupitia Wakala aliye karibu nawe au piga *149*88#.
Kushiriki ni kuanzia miaka 18 na kuendelea. Cheza Kistaarabu. ITHUBA ni mwendeshaji rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa.
#AminiChezaUshinde
#BahatiNasibuYaTaifa
TAARIFA RASMI: KUSTAAFU KUGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA KYERWA
Kwa moyo wa dhati kabisa, napenda kuwataarifu kuwa nimeamua kustaafu rasmi kugombea Ubunge wa Jimbo la Kyerwa katika Uchaguzi ujao wa ndani ya Chama na Uchaguzi Mkuu wa Taifa unaotarajiwa kufanyika Oktoba.
Uamuzi huu umetokana na maono mapya niliyonayo juu ya maisha na mchango wangu kwa jamii nje ya siasa kwa sasa. Kwa zaidi ya miaka 10, nimepata heshima kubwa ya kuwatumikia Wanakyerwa kama Mbunge wenu. Nawashukuru kwa imani, ushirikiano na upendo mkubwa mliouonesha katika kipindi chote cha utumishi wangu.
Ninawaomba radhi kwa mapungufu yoyote yaliyojitokeza kama binadamu. Mliniongoza, mlinisahihisha kwa hekima na kunitia moyo kila nilipopitia changamoto β na hilo siwezi kulisahau.
Nawashukuru sana familia yangu kwa kuwa nguzo yangu kuu β kwa ushauri, maombi na faraja. Pia nashukuru kwa dhati Viongozi wa Serikali Wilayani Kyerwa, hasa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri, kwa ushirikiano mkubwa tuliokuwa nao katika kuleta maendeleo kwa wananchi wetu.
Siwezi kuhitimisha bila kukishukuru Chama changu cha Mapinduzi (CCM), chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa miradi mikubwa ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya Jimbo letu β hususan katika sekta za maji, afya, elimu, umeme na barabara.
Nawatakia kila la heri wote mnaotarajia kuchukua fomu za kugombea Udiwani na Ubunge. Ni matumaini yangu kuwa mtaendeleza mema yote ambayo tumejenga pamoja kwa miaka hii.
Mungu ibariki Kyerwa. Mungu ibariki Tanzania.
Asanteni sana.
Mhe. Innocent Bilakwate
Mbunge wa Jimbo la Kyerwa (2020β2025)
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Ally Haji @arafat__ah amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la shauri moyo visiwani Zanzibar leo Juni 28,2025 kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM)
Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, leo Juni 28, 2025, amechukua rasmi fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde
amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Mtumba
Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya
Dodoma Mjini Sophia Kibaba.