@Royaltv_plus Kwani Rais alipomjibu Nchimbi kwamba ameridhia kujiuzulu kwake huyu Yeriko alikuwa wapi? Na lipi lilitangulia kati ya Rais kuridhia na CCM kumfuta uanachama?
Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge. Mwaka 2017 alitoa kauli kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya ili hatua nzuri zinazochukuliwa na serikali zizingatie misingi ya katiba badala ya kutegemea uamuzi wa mtu. Rais Magufuli akasema kuwa katiba mpya si ajenda yake.
Haikuchukua muda mrefu, idara ya uhamiaji ikaanza kuhoji uraia wa askofu huyo. Bado pasipoti yake imeshikiliwa. Anachunguzwa uraia.
Abdul Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alitoa taarifa kupitia simu yake kuhusu watu waliomteka usiku, wakamsafirisha usiku kucha kutoka Dar es Salaam hadi Iringa.
Kwa kuwa โwatu wasiojulikanaโ ambao wamekuwa wanateka na kupoteza watu wanahusishwa na vyombo vya dola, yalitoka maagizo mengi ya kisiasa yakitaka kijana huyo ashughulikiwe. Serikali imemfumgulia kesi mahakamani. Amesimamishwa masomo chuoni. Anachunguzwa uraia.
Padri Saba, Askofu Kakobe, Eyakuze, na Nondo ni wazaliwa wa Kigoma. Askofu Niwemugizi ni mzaliwa wa Kagera. Orodha ya wanaoshughulikiwa โkimfumoโ ni ndefu.
Chanzo maalumu cha SAUTI KUBWA kinaeleza kuwa miongoni mwa waathirika wa mkakati huu ni viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya upinzani, na wafanyabiashara wasiopenda kuunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Miezi kadhaa iliyopita, mke wa kiongozi mmoja wa dini hapa nchini alizuiwa na maafisa usalama na wa uhamiaji katika uwanja mmoja wa ndege akiwa safarini kuelekea Ulaya. Alikaguliwa kwa saa kadhaa akidaiwa kuwa yeye ni raia wa nchi moja ya ulaya. Kama hawa wengine, naye anazaliwa katika mkoa mmoja wa mpakani.
Idara ya uhamiaji katika viwanja vya ndege inathibitisha kuwa viongozi wengine wa dini wamekuwa wanatiwa msukosuko katika viwanja mbalimbali, wakiwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa uraia. Wapo ambao kutokana na misukosuko hiyo wameachwa na ndege. Wote waliohojiwa wanatoka mikoa ya mipakani.
Wimbi hili limechochea hisia mbaya kutoka kwa raia wanaoishi mikoa ya mpakani, wakidai kete ya uraia inatumika kuwanyima haki zao za msingi.
Habari za uhakika zinasema unyanyasaji huu umekuwa unaendeshwa chini ya usimamizi wa rais mwenyewe. Lakini baadhi ya viongozi hawa wanapomuuliza anakana kuhusika, huku kwa siri akihimiza idara ya uhamiaji โkukaza kambaโ hata kuwanyangโanya pasipoti zao.