#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo tena Tar. 08/09 kesi ya Mhe. Tundu Lissu Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ya Dar es salaam.
Mheshimiwa Lissu alishafika mapema sana asubuhi ya leo. Na hapa katika Ukumbi No. 1 wa mahakama hii pia viongozi mbalimbali wa Chama na mabalozi wameshafika.
Ukumbi umetapika watu na wanachama wengi wamezuiwa huko nje ya mahakama.
Viongozi wa Chama waliofika hadi sasa hapa Mahakamani.
1. Makamu Mwenyekiti, John Heche
2. Katibu Mkuu, John Mnyika.
3. Godbless Lema, Mjumbe wa Kamati Kuu
4. Boniface Jacob, Mwenyekiti Kanda ya Pwani.
5. Joseph Haule "Prof. Jay" Mbunge mstaafu wa Mikumi.
6. Wapo wakurugenzi mbalimbali wa Chama na maafisa mbalimbali hapa.
7. Wapo wafuasi mbalimbali wa Chama kutoka mikoa mbalimbali.
Ngoja nijaribu kuwaandikia Mawakili waliofika kumuunga mkono Mhe. Lissu pia. Najaribu kukusanya majina yao yote.
Hatuoni dalili kwamba kesi hii itarushwa live. Hatuoni vitendea kazi hapa mahakamani vya kutuaminisha kuwa kesi itakuwa Live streamed.
Tutajitahidi kushare hapa chochote kinachowezekana au kitakachoendelea mahakamani.
Tukumbuke leo kesi ya Uhaini inakuja kwa mara ya kwanza na zoezi litakalofanyika kwa mujibu wa summons ya Mahakama ni pamoja na Mhe. Tundu Lissu kusomewa Shtaka lake pamoja na kusomewa hoja za awali (Preliminary hearing, PH)
Jambo lingine tunalotegemea linaweza kuibuka leo ni kwamba je Mhe. Lissu ataendelea kujiwakilisha mwenyewe au atawakilishw na Mawakili wake? Jibu la swali hilo pengine tutalipata leo baada ya kesi kuanza.
Hatujui pia kama inaruhusiwa kwa Mheshimiwa Lissu kujiwakilisha na wakati huo huo na mawakili wake wawepo. Mimi natamani iwe hivyo. Wapigwe mande. Wachangiwe na Lissu na mawakili wake kwa pamoja.
Sasa hatuwezi jua ngoja tusubiri wataalamu wa sheria watasema nini? Muda sio mrefu tutapata majibu ya masuala hayo.
VIDEO:
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amechangia shilingi milioni 50 Suzana John Pombe Magufuli ambaye amezindua taasisi yake ya Ndoa na Malezi ijulikanayo kama MAPCO.
Akizungumza jana Jumapili ya Julai 13, 2025 baada ya kumwakilisha Rais Samia kwenye uzinduzi wa taasisi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert John Chalamila amesema “ndugu yangu dada yangu Suzan Mheshimwa Rais anasema atakuchangia wewe shilingi milioni 50 na mimi kama Mkuu wa Mkoa nitakuchangia wewe milioni 10”
Suzana amezindua taasisi yake pamoja na kitabu chake cha Ndoa ni Paradiso akilenga kwenda kusaidia jamii kuboresha malezi na kuimarisha ndoa.
Msanii kutoka Nigeria akielekea Tanzania amepost “Guess the country” akiwa KIA … kajaziwa comments zinasema No Reforms, No Elction.
Msanii huyu ameingia hofu na ame-record video akiuliza what’s No Reforms, No Election?
Anasema “I’m scared my comment section a lot of No Reforms, No Election”. What’s #NoReformsNoElection ?
Msanii Chella ameshtushwa na COMMENTS za “NO REFORMS NO ELECTION” kwenye post yake kuwa anakuja TANZANIA kufanya Show.
Wabongo wamechafukwa, sio IG, sio TIKTOK.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Haya aliyasema MEKO hakuna takataka ilinyenyua mdomo kutoka kwenye CHAMA CHA WAKOLONI WEUSI.
Leo GWAJIMA anaongea haya haya wanaibuka na kuanza kumshambulia. Hii inamaanisha UTEKAJI unakibali kutoka kwa WAKOLONI WEUSI.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Yani watoto wa KIBAHA SECONDARY wanaakili kuliko “TUME YA UCHAGUZI”.
Huu mfumo ukija kufanya kazi basi hayupo KIBAKA kutoka kwa WAKOLONI WEUSI atashinda hata kijiji kimoja.
Madogo wanaishia kubuni vitu vya maana na kurudi makwao wakakatie NG’OMBE nyasi.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎