Kwa ambao mlikuwa hamjaona hii video ya Mwaipopo akimshutumu Mwigulu, hii hapa.
Sasa jiulize ni Mtanzania gani unamjua wewe ana pumbu la kuita press na kumwanika Waziri mkuu??? Hii inakuonyesha Mwigulu hana nguvu tena ndani ya serikali, kabaki na title tu ya kuuzia sura na pia inakuonyesha kwamba huyu Mwaipopo ana back up ya vyombo vyote vya usalama Tanzania, na nikisema vyombo vya usalama namaanisha Abdul.
Huu ndio mwanzo wa project ya kumpoteza Mwigulu Nchemba, msaliti namba moja wa Watanganyika.
Sitokaa nisahau maneno ya Mwigilu just 1 month baada ya Watanganyika kuuliwa kama mbwa. Mwigulu alisema Gen Z walikuwa na silaha na wakaua askari, akimaanisha kwamba Watanganyika elfu 10 walistahili kuuawa sababu waliua askari. Aliongea haya akitegemea ndio yatafanya Samia na Kikwete wampe Urais 2030.
Kwa mnaojiuliza uadui na kimama unatokana na nini? Uadui umetokana na Mwigulu kutaka Urais 2030, yani yale yale ya January Makamba, Mwigulu alisherehekea Makamba kutolewa akidhani urais wa 2030 sasa ni wake. Mwigulu kajipanga kuwa Rais 2030 hata Baada ya mauaji ya October 29. Mwigulu anaseti mambo ya Urais mpaka huko kanisani kwake.
Kimama Urais wa 2030 anautaka yeye mwenyewe sababu kaua Watanganyika so anaogopa akiachia madaraka atapigwa kitanzi kwa mauji aliyoyafanya, and more so anaogopa mwanae atapigwa kitanzi, hawezi kuachia nchi kwa just anybody, eti kapigiwa kura na kamati kuu ili aibuke Magufuli mwingine, either abaki yeye mwenyewe, ampe mtoto wa kumzaa au akikosea sana sababu kabanwa basi ampe mtoto wa Kikwete yule Ridhwani sababu mauaji aliyafanya kwa backup ya Kikwete so chance ya mtoto wa Kikwete kumgeuka na kutaka uwajibikaji wa October 29 wakati na baba yake alishiriki yale mauaji ni ndogo sana.
Kama Watanzania tutakuwa maboya na waoga na tukashindwa kutumia 2 BIG opportunities za kuandamana kwa amani mbele ya dunia,MUNGU katupa bila kupigwa risasi au kutishiwa kwa wanajeshi na polisi kuwekwa barabarani in 2027, AFCON na Miss World 2027, basi tunastahili maumivu haya ya roho na 2030 ni mtoto wa Kikwete pekee mwenye nafasi ya kuwa mgomboea wa CCM , mbali Samia mwenyewe kubaki madarakani.
Sababu ingine ni kwamba hawa kina Mwigulu wanaweza kuja ku turn state witness against Kimama na mwanae kwa ku cut deals na serikali ijayo ili kujipunguzia wao adhabu. Lazma wapotezwe. Kama kwenye mafia movies inavyokuwaga, wakiona dalili za mmoja wao kuja kuwa shahidi wa serikali baadae huwa wanamalizana nae mapema.
Yani hao kina Angela Kizigha, Kina Katambi wote wakimaliza kutumika hawatoachwa salama maana hawa wote watakuja kuuza mechi ili kujiokoa.
Huyu Mwaipopo ndio Musiba wa serikali ya 6. Kama mnakumbuka Magufuli alipotaka kushughulikia mtu Musiba ndio alikuwa anaanza attacks, this time ni Mwaipopo ndio anafanya ile kazi ya Musiba.
Mwigulu kidogo afe huko Europe, alitibiwa karibia 1 month huko Europe sababu ya sumu. Ni vile @MariaSTsehai hakuandika ile habari kwa confidence zote so haikuchukuliwa seriously but she was 100% correct na mimi nikagoma kui-confirm ili nisimuokoe Mtanganyika aliehalisha vifo vya vijana wetu. You have no idea watu waliotaka niiongelee ile habari ya Mwigulu kupewa sumu Europe. Wazito!!!! Na niliwajibu honestly, I DON’T GIVE ONE FUCK!!!!!!!!
PS: Second photo: Familia ya former president, JAKAYA KIKWEYE ikifurahia ubunge, NA HIGH HEELS JUU, less than 30 days after 10,000 Tanzanians were murdered in cold blood for fighting for justice. Wanafurahia UBUNGE WA DAMU!!!!!
Watanganyika tukishashinda hii vita hawa watu lazma wa stand trial for their crimes!!!!!!! fair trial, sio hizi sham trial za kina LISSU, Tutawaonyesha what a fair,
Legal, just trial looks like. Hatutolipa kisasi ila tutawaonyesha haki inafananaje. HATUTAKI KUOMBA MSAHAMA!!! They will stand a fair trial,
One they didn’t afford our Mandela, @TunduALissu
We will live what we preach. I WILL SEE TO IT!!!!!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 13
Anaendelea Mhe. Lissu
Upande wa mashitaka unalazimisha kuipa mamlaka Kisutu ambayo haikuwa na hayo mamlaka, wao wanasema inayo mamlaka mimi nasema haina.
George Abdon Kilinga mahakama inasema walikubaliana.Totally wrong. It is distinguishable.
Joseph Mkenda vs Ladislaus...... tulipewa kesi hiyo nyingine....kesi inahusiana na mauziano ya ardhi na mnunuzi aliuziwa ardhi na mtu ambae sio mmiliki kwahiyo mahakama ilishughulika na jambo kama kesi ya mkataba na sio kesi ya ardhi.
Jaji alitoa Obiter dictum kwamba Jurisdiction of the court is the creature of the law.
Obiter dictum maana yake ni maneno yaziada kwenye hukumu sio yanayoamua kesi husika.
Sasa hata ingekuwa sio ibiter dictum mimi sina pingamizi mambo yaliyosemwa hapo na mimi nasema hii kesi inaunga mkono ninachosema nashukuru sana kwa wao kuniletea hii kesi.😂
Kesi ya tatu Commisioner General TRA na wenzake.
What was the issue before the Court of appeal? Whether the High Court has the jurisdiction to assume its revisionary jurisdiction. Ilifanya review ya mambo ya kodi kwenye mgogoro mwingine.
Nani atakayebisha msimamo huo baada ya kusoma aliyosoma? Mimi sibishi.
Hoja ya msingi the question of jurisdiction ambayo kisutu iliendelea na shauri ambalo haina mamlaka kulisikiliza.
Je mnatakiwa kuendelea na hilo kwa mtindo huo. You should not condon such illegality.
Na hii kesi ya Job Mrema nayo pia inaunga mkono hoja yangu ndio maana niliwashukuru kwakweli.
Kuhusu kesi ya Elias John.
Kesi hii ii ilikuwa ndio Climax ya hoja za wakili wa serikali mwandamizi alileta kwa mbwembwe sana.
Kwamba huyu mshitakiwa angejua wala asingeleta haya mambo alisema hivyo.
Hii kesi ilikuwa ni kesi ya mauaji na wakata rufaa Elias , Daniel, Dotto walikuwa convicted of murder and sentenced to hell the committal proceedings were conducted to Chato District Court where they have arrested.
In the High Court ilisema kulikuwa na makosa mengi mahakama ya Committal kule chini.
Mahakama kuu iliona hii committal haikuwa halali ikaifutilia mbali na kuamua committal ifanyike de novo. Ifanyike upya. Hiyo committal denovo haikufanyika.
Mahakama kuu ikaendelea na kesi bila committal kufanyika na mahakama kuu ikaendekea na kesi na kuwahukumu kifo washitakiwa wote wawili.
Kesi ikaenda mahakama ya rufaa mtaona majaji kuanzia ukurasa wa 6 mpaka wa 9 mahakama ya rufani inazungumzia jinsi mahakama kuu ilikosea kuendesha kesi bila committal order.
Mahakama ya rufani kwa kutumia revisionary power ikafutilia mbali proceedings za mahakama kuu na mahakama ya Chato.
Halafu mwisho kabisa mahakama kuu baada ya kuwa imefuta proceedings zote watu wamehukumiwa kifo, ikasema sasa hawa waliohukumiwa kifo waendelee kukaa gerezani meanwhile the Appellant shall remain in custody for afresh new committal.
Ndio maana wakili Job Mrema alikuwa anasema tutarudi Kisutu, tena alikuwa anasema kwa mbwembwe kabisa.
Sasa naomba niseme yafuatayo.
1. On its facts Elias Dotto case is completely distinguishable with the case at hand in other words is completely irrelevant here. Kwenye facts zake. Kesi ilisikilizwa na sentenced to death.
Mimi I'm a mere accused. Charge yangu inahusiana na mambo ya kisiasa tu je inafananaje na convicted murderers.
2. Committal ilifanyika vibaya na mahakama kuu ikaifuta na wakaendelea na kesi.
Hapa kwangu bado hamjasema kuwa committal ilikuwa ni mbovu, hoja yangu hapa ni kwamba toka jumatatu nawaambia msiendeleee na kesi hii kutokana na makosa yaliyofayika kisutu.
Sasa hizi kesi zinalinganaje?
Mfanano wake ni upi?
I'm asking the court not to follow in that trap. Msifanye kesi iliyotoka committal Court unlawful inalingajaje na hii?
Hata hii kesi is totally irrerelevant to this case.
Part 14 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 12
Anaendelea Mhe. Lissu
Tatu. Mahakama ya Rufaa kwenye kesi ya Dodoli Kapufi ilisema nini kuhusu kifungu cha 183?
Jaji Chande alisema in essence that section is deal with trial not deal with Committal. Section inayodeal na committal ni S. 261.
Nimemaliza na hiyo niendeleee na kesi yao nyingine.
Hii nayo imeletwa bure kabisa.😂
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nishughulike na JOB MREMA.
Huyu Katuga nimemaliza nae.
Anasimama Katuga anasema kifungu cha 187 hajakisemea.
Mhe. Lissu anasema nawashukuru sana Katuga. Ngoja nije hapo.
Hicho cha 187 trial at a place where act done.
Hii section is about trial na section about committal is 262, 263 hadi 265.
Hivyo basi kama ambavyo sect. 183 ilivyo irrelevant basi hata section 187 nayo ni hivyo hivyo haihusiki hapa tunazungumzia committal. Tofautisha Committal na trial.
Sasa nirejee kwenye suala la Mashahidi. Nalo lilizunguzwa na Mrema na nimesema naanza kushughulika nae.
Suala la Mashahidi wangu kutokuandikwa. Walilizungumza.
Katuga anasema hawakuitwa na kuandikwa wanaweza kuandikwa baadae hakuna tatizo. There is no prejudice.
Wakili Mrema pia alisema Mshitakiwa alishauriwa kuwa majina ya mashahidi atakuja kuwasema mahakama kuu. That one was premature kwahiyo hamna shida.
Waheshimiwa majaji naomba niwaonyeshe jinsi ambayo hii nayo ni shida kubwa.
Mashahidi kutokuandikwa kwenye commitall proceedings.
Ipo hivi Waheshimiwa majaji, Mshitakiwa ana haki ya kutamka majina na anuani ya mashahidi wake wakati wa committal maana asipoitumia inabaki fadhila ya mahakama.
Kwenye committal nilikuwa na haki ya kusema mashahidi wangu na anuani zao. Kwenye mahakama hii ni descretion yenu sio haki yangu tena.
Mnaweza kuamua au msiamue sasa niwapeleke kwenye sheria.
Kifungu cha 264 cha CPA ndo kinatoa haki kwa mshitakiwa kutaja majina ya mashahidi wake wote.
Nikisema nina mashahidi wewe Hakimu KISWAGA huwezi sema nitawasemea mahakama kuu, unapaswa kuandika.
Hilo halikufanyika.
Mawakili wa serikali wanasema ni premature, unaweza kuita baadae, sasa hiyo baadae iko kifungu cha 281 na 314 ya CPA. (Kumbukeni CPA ni Criminal Procedure Act - Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
S. 281 inasema hivi msajili wa mahakama kuu ataandaa wito kwa mashahidi wote ambao orodha yao ipo. Registrar/ msajili anatoa summons/wito kwa hao uliowataja. Kinasema hivyo.
Sasa kama hujataja nini kinapaswa kufanyika ndio S. 314 inaingia hapo. Kinasema hivyo mtuhumiwa hawezi kuwa na haki ya kuita mashahidi wake ambao hawakuwa kwenye orodha yake labda mahakama ijiridhishe kuwa kuna umuhimu wa mashahidi hao kuitwa.
Sasa hii ni fadhira ya majaji haki yangu nimesema ilikuwa Kisutu.
The accused person shall not be entitled to call witness without approval au consent ya majaji sasa kuna prejudice kubwa kuliko hiyo kunyang'anywa mashahidi wangu.
Haya maneno ya kwamba naweza kuwaita baadae ni maneno ya watu wenye nia mbaya sana na mimi.
Wanasema mambo ambayo sheria haiyatambui na kuyakubali, naomba waheshimiwa majaji msikubali jambo hili.
Sasa Job Mrema alisema majaji mnapaswa mjiulize hili pingamizi kama liko sawasawa mbele ya mahakama hii.
Na alilisema jambo hili kwa mbewembwe kabisa.
George Abdon Kilinga na wenzake vs Anna na wenzake ni mashauri ambayo aliyaleta hapa.
Kwanza hii ni kesi ya mirathi ilianzia mahakama ya mwanzo, ikaenda mahakama ya wilaya ya Babati ambayo iliamua kwamba wadaaawa wataamua watumie sheria gani? Mahakama kuu rufaa ya pili sasa Madam Justice alisema parties can not by agreement confer jurisdiction to a Court.
Wadaawa hawawezi jiamulia kuipa mamlaka mahakama hii kwasababu suala la jurisdiction (mamlaka) ni suala la Jaji.
Kwenye kesi yangu sasa Mshitakiwa anasema alikuwa committed na mahakama ambayo haikuwa na mamlaka.
Part 13 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 11
Anaendelea Mhe. Lissu
Walinipa uamuzi wa kesi ya Ishengoma na wenzake sita.
Kesi ya Mahakama ya Rufani hiyo Kesi ya Donatus Ishengoma ukurasa wa 15 umecite kesi ya Mbogo niliyoitaja hapo awali.
Anasoma hiyo kesi hapa ilichosema. Maelezo marefu hapa.....
Waheshimiwa majaji nani anauwezo kuwa na ubishi na hili, Mimi sina.
Sina ubishi na superior Court can do on interference to surbodinate court.
Kifungu cha 265 hakina descretion kihivyo wanavyodhani. Its only partially decretion. Naomba nikisome hicho kifungu.
Anakisoma sasa hicho kifungu hapa.
Descretion nimeambiwa hapa kwamba ni kumpeleka mtuhumiwa gerezani. Hiyo ni 265(1).
Ukianza kusoma vifungu vingine ikitaka kuahirisha iandike sababu za hayo maahirisho.
Mamlaka haina option ya kutokuandika sababu na haina option ya kutokutoa reason hizo.
Naomba niendleee hiyo kesi ya ishengoma imeenda kwa kiwango hicho.
Naendelea na kesi zao zingine.
Waheshimiwa majaji wakili Kasuga aahhh samahani Katuga aliuliza a very rhetorical question kwamba sasa turudi kisutu?
Hili nitalijibia lamwisho.
Twende kwenye improper dating kubadilisha proceedings na kubadilisha tarehe za matukio mahakamani.
Tuliambia hiyo ni amere sleeping of the pen na tukapewa Kesi ya Baraka Mashaka Kesi ya Mahakama kuu PC Civil appeal/2023.
Hoja yangu ni kwamba kukiwa na kosa moja au mawili kwenye kurasa 101 unaweza kusema ni sleep of a pen.
Sasa ukiwa na makosa mia kwenye nyaraka hiyo hilo la kukosea tarehe haliwi kosa dogo kabisa lazima yaangaliwe kwa uzito.
They are part of the designing kwangu mimi na naomba hayo makosa ya kuteleza kwa mkono naomba yachukuliwe kuwa sio kuteleza kwa mkono yachukuliwe kama sehemu ya uchafu mwingi uliopo humu na niliousema toka siku ya kwanza.
Kwenye hiyo kesi hiyo mshitakiwa alihukumiwa maisha kwa kumfanya kinyume na maumbile mtoto lakini mahakama ikamfunga kwa kosa la armed robbery.
Mahakama ya rufaa ilisema kwa vile adhabu ni ileile kwa makosa hayo basi ni sleep if a pen.
Sasa huwezi kuleta kesi ya namna hii itumike kwenye hoja za kesi tuliyonayo leo hapa.
Kuna kitu amekisema sana Katuga kwamba malalamiko yangu ni kutaka huruma amekisema toka kisutu.
Sympathy..!! Ilianzia Kisutu imekuja hadi mahakama hii.
Pamoja na kwamba sidhani kama itaamua one way to other naomba niweke for the record kupata huruma unapoonewa sio jambo baya.
Kuomba huruma unapokuwa kwenye matatizo sio jambo baya.
Kama anadhani ukipata matatizo unahitaji huruma.
Sasa la msingi ni nini? Siwaombi Majaji chochote mtakachoamua msiamue kwa huruma. Muamue yote kwa haki na kwa mujibu wa viapo vyenu. Msinihurumie na sihitaji huruma yenu nahitaji muamue kwa haki.
Nayasema haya for the record nimeona Katuga anayarudia rudia sana.
Kuna hoja ilitolewa na Katuga na imerudiwa na Mrema kuhusu kifungu cha 183 cha CPA.
Job Mrema anasema inapaswa kusomwa na 187 pia za CPA izo zote zinazungumzia mamlaka ya mahakama.
Mahakama ya Kisutu. CPA ni sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
S. 183 inazungumzia general authority of Court in Tanzania. Kwamba mahakama yoyote ina mamlaka ya kuamrisha mtu kwenda mahakamani ndani eneo la mahakama hiyo kama mtu huyo amefanya kosa ndani ya eneo la utawala wa mahakama hiyo.
Sasa wameleta hii ili waseme kwamba uliletwa kisutu kwasababu ulifanyia kosa Dar es salaam hicho kifungu walichotaja cha 183 kinazungumzia tayari ameshashtakiwa kinaipa mamlaka amri aletwe kwenye mahakama husika.
Mimi nilikamatwa Mbinga na wakati nakamatwa sikuwa mshitakiwa.
Mimi nimekuwa mshitakiwa baada ya kupelekwa Kisutu na kusomewa mashtaka.
Sababu ya pili ni kwamba kwani nilipelekwa Kisutu kwasababu mahakama iliamua nipelekwe kisutu? Hakukuwa na order hiyo.
Kwahiyo S. 183 haiwezi ku apply kabisa.
Part 12 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 11, 2025
Jana tuliishia Part 9 so leo tunaendelea na
Part 10
Hali ya hewa ya mahakama ni nzuri na imetulia.
Askari magereza wameingia hawa wawili watatu ambao wamekuwa wakivaa haya madude usoni ingawa wengi wao siku hizi hawajifichi sura zao kama walivokuwa wanajificha wakati tupo Kisutu.
Imesikika sauti ndogo ya askari High Courtttttttttt.
Kinyonge sana ni kama jamaa hajapata breakfast.😂
Majaji wanaingia na watu wote wamesimama.
Mheshimiwa Lissu ameingia na style yake mpya anakunja ngumi na kuizungusha kwa vibe sana kama kwenye ile video mliyoiona juzi.
Majaji wanaandika andika muda huu.
Wameingia kwa tabasamu kubwa sana leo Majaji wote watatu.
Wamevaa haya magauni yao mekundu na hivi vitai vyeupe shingoni kwao.
Jaji Nduguru kiongozi wa jopo anateta jambo na Kalani wa mahakama.
Sasa Jaji anataka kuongea hapa huku anamuangalia Mh. Tundu Lissu.
Karani anaita kesi Criminal Case No. 19605/2025.
Jaji: Jamhuri Karibuni.
Katuga: Nipo na Misieh Kahima, Thawabu Issa, Harrison Lukosi, Cathbert Mbirnge hawa wote ni Mawakili wa Serikali ambao ni 6 tunaiwakilisha Jamhuri katika shauri hili na mshitakiwa yupo Mheshimiwa Jaji.
Katuga: Tunaendeela na usikilizaji wa mapingamizi na mwenzetu mshitakiwa kama yupo tayari aendeleee. Sisi hatuna shida.
Jaji: anaandika. Anamuuliza Mh. Lissu vipi uko tayari.
Mhe. Lissu: Niko tayari na imara kabisa.
Jaji: anaandika na kuteta kidogo na wenzake.
Sasa unaweza kuendelea ndugu Lissu.
Mhe. Lissu Waheshimiwa Majaji nimefurahi kuwaona na niwapongeze kwa kazi kubwa mliyofanya toka jumatatu.
Lissu anaendelea sasa.
Jana niliomba ahirisho ili nikasome kesi walizonipa hawa jamhuri naomba niseme hiyo kazi nimeifanya vizuri sana.
Niwashukuru mawakili wa serikali kuleta hizo kesi kwasababu zitanisaidia sana kuja kusema nitakachosema siku ya leo.
Ni kesi wamezileta wenyewe sio mimi.
Wakili wa serikali Katuga na Mrema walitoa hizo kesi wenyewe kwahiyo nitaonesha namna hizo kesi kama ni relevant au sio relevant kwa kesi tuliyonayo.
Kwa kuanzia naomba nizungumzie kauli ambayo ilitolewa juzi na wakili wa serikali Mkuu Katuga kwamba committal proceedings lengo lake ni kuhakikisha fair trial.
Hiyo position ipo kwenye maamuzi mengi ambayo yametajwa toka jumatatu mimi nakubaliana na msimamo huo ni kuhakikisha kuna fair trial katika kesi zinazosikilizwa mahakama kuu. Na kesi hizo ni kesi kubwa.
Kama lengo ni kuhakikisha fair trial/hearing hivyo basi committal Court is responsible to make sure the accused person is given full opportunity
Huwezi kumpa nyaraka nusunusu mtuhumiwa kwenye kesi yake, huwezi kuacha makosa mengi yote kama yaliyopo.
Ni lazima mshitakiwa apewe nafasi ya kusema maelezo yake yote. Apewe hiyo fursa na ipo hoja ya whether nilipewa fursa ya kutoa maelezo yangu kwenye committal Court (mahakama ya ukabidhi)
Mahakama ya ukabidhi ilipaswa pia kunipa nyaraka zote zilizopatikana kwenye committal processes.
Hayo yote yakitimizwa kutakuwa na fair trial na yasipotimizwa hayo hakutakuwa na fair trial kabisa.
Waheshimiwa Majaji Wakili wa Serikali Kiswaga watu wanacheka.😂😂😂
Anasema Waheshimiwa huyu Kiswaga amenikaa sana kichwani. Samahani ni Katuga.
Sasa anasema lengo la niliyosema ni kuupotosha umma na nyie majaji kwa hayo ambayo nimeyasema tangu jumatatu mimi binafsi siamini kama kuna chochote nimesema cha kuipotosha mahakama.
Nafikiri nimewezesha mahakama hii na umma kuwaleeza mambo mengi ambayo yalikuwa yamefichwa.
Katuga anasema kuhusu S. 265(1) of CPA anasema hayo mamlaka ya kuahirisha kesi na kutoa sababu za msingi za kuahirisha na kuandika sababu hizo alisema all that is descretion..
A superior court like this should not interfere that power.
Nikapewa kesi ya MBOGO and ANOTHER 1993 kwamba inaunga mkono msimamo wao huo.
Waheshimiwa majaji hiyo kesi ya Mbogo vs Shah sina library yangu ningeipata hiyo kesi yote.
Part 11 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako kwenye tweet hii.