Kheri ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika.
Kutimia kwa ndoto ya kila mtoto kunategemea maamuzi na hatua tunazochukua leo. Tunapojiandaa kuanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, tumeazimia kujenga Taifa ambalo kila mtoto anapata malezi na makuzi bora, analindwa na anajengewa msingi imara wa maisha yake.
Huu si wajibu wa serikali pekee, bali ni wa kila mwananchi, kwani uhai, ulinzi, usalama na maendeleo ya Taifa letu vinategemea ustawi wa watoto wetu.
@KennedyMmari Ndugu Nehemia Mchechu alijaribu ku-propose project kama hii pale Muheza eneo la Kigombe Beach miaka hiyo, ilikuwa ni project kubwa sana. Wakati watu wanamaliza presentation Madiwani wakataka mgao mkubwa before anything else πππ. Mchechu akala nyoya
Hotuba yangu leo niliposhiriki maadhimisho ya Miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam. Maeneo muhimu niliyosisitiza Benki Kuu kufanyia kazi tunapoelekea kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 ni pamoja na:
1. Kuimarisha uwezo wa kungβamua mwelekeo wa taifa kiuchumi.
2. Kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi za kifedha kwa lugha inayoeleweka.
3. Kuhakikisha taasisi za kifedha zinaacha kutegemea dhamana za mikopo ambazo wananchi wengi hawana.
4. Kuhakikisha mafanikio ya mfumo wa fedha yanaenda sambamba na ustawi wa wananchi.
5. Kuimarisha akiba ya fedha za kigeni.
Mwaka huu Tanzania na Singapore tunaadhimisha miaka 45 ya uhusiano wetu ambapo kwa upekee leo tumempokea Rais wa Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam, Ikulu jijini Dar es Salaam. Hii ni historia na heshima kwa nchi yetu kwani ni mara ya kwanza Rais wa nchi hiyo kutembelea Tanzania, hatua inayodhihirisha dhamira yetu ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya nchi zetu na watu wake.
Baada ya mazungumzo yetu, tumeshuhudia utiaji saini mkataba na hati nne za makubaliano zinazolenga kufungua fursa mpya katika biashara, uwekezaji, kuwezesha vijana kupitia elimu ya ujasiriamali, ujuzi na ubunifu hasa katika uchumi wa kidijitali. Aidha, tumekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo sambamba na kuanzisha mfumo wa pamoja wa mashauriano utakaosaidia kuratibu utekelezaji wa makubaliano yetu na kushughulikia changamoto kwa ufanisi na kwa wakati.
Katika hatua nyingine, nimeikaribisha Singapore kufungua ubalozi wake nchini ili kurahisisha utekelezaji wa makubaliano haya na kuimarisha zaidi uhusiano wetu.
President of Singapore arrives in Tanzania for a three-day state visit
The President of the Republic of Singapore, H.E. Tharman Shanmugaratnam, has arrived in Tanzania for a three-day State Visit from 8β10 June 2026.
Upon arrival at Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam, President Tharman Shanmugaratnam, accompanied by his spouse, Mrs. Jane Ittogi Shanmugaratnam, was received by the Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Amb. Dr. Mahmoud Thabit Kombo (MP), together with other senior government officials, including the Dar es Salaam Regional Commissioner, Hon. Albert Chalamila, and the Managing Director of the Air Tanzania Company Limited (ATCL), Eng. Peter Ulanga.
President Tharman Shanmugaratnamβs State Visit is the first to be undertaken by a President of Singapore since the establishment of diplomatic relations between Tanzania and Singapore in 1980.
The visit marks a significant milestone in strengthening diplomatic relations, trade, and investment cooperation between the two countries.
During his stay, President Tharman will be accorded an official welcome by his host, the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Samia Suluhu Hassan, at the State House in Dar es Salaam. The two leaders are scheduled to hold official talks aimed at enhancing bilateral cooperation in key areas, including trade and investment, the digital economy, port development, education, skills development, tourism, and infrastructure.
The visit will also feature participation in the TanzaniaβSingapore Business and Investment Forum, as well as a visit to Zanzibar for discussions with the President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council, H.E. Dr. Hussein Ali Mwinyi.
The State Visit is expected to create new opportunities for economic cooperation and further strengthen the longstanding partnership between Tanzania and Singapore for the mutual benefit of their peoples.
Kumbe mambo haya ndivyo yalivyo? Sasa LGBTQ Tanzania kivipi yaani? Yaani umepokea hela kutetea mapapai Tanzania au?
Kumbe PANYA BUKU ulipokea hela kwa akili ya kuchochea vurugu wakati wa uchaguzi? Ndiyo maana ulikuwa hutaki hii documentary itoke eeeh
BASI SAWA ITAFAHAMIKA TU ..π
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika Jijini St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026. Kongamano hilo limewakutanisha Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Taasisi za kukuza Uwekezaji kutoka Tanzania na Urusi.
ππππ πππππ πππππππππ πππππππ ππ πππππππ πππππ
Moscow, Urusi | 04 Juni 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN), ikiwa ni kutambua mchango wake katika uongozi, maendeleo ya jamii na kuendeleza sekta ya elimu.
Akizungumza baada ya kupokea heshima hiyo, Rais Samia amesema tuzo hiyo si yake binafsi bali ni ya walimu, wanafunzi, wazazi na wote wanaoamini kuwa elimu ni msingi wa maendeleo ya watu na mataifa.
Rais Samia amesisitiza umuhimu wa elimu katika kuandaa jamii kukabiliana na mabadiliko ya dunia ya sasa, hususan katika maeneo ya sayansi, teknolojia na ubunifu, akieleza kuwa ushirikiano wa kimataifa ni muhimu ili mataifa yaendelee kunufaika na maendeleo hayo.
Hii ni miongoni mwa shahada za heshima ambazo Rais Samia ameendelea kutunukiwa kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani kutokana na mchango wake katika maendeleo, uongozi na ustawi wa jamii.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_______________
#KazinaUtuTunasongaMbele #SamiaSuluhuHassan
#CCMIpoKazini l
#ElimuKwanza