@Elparton112 Vipi pale kipande cha man dojo na Domo Kaya wanaimba, na sometimes nawaza mengi juu yako, natamani nibusu tena lips zako???... Hii ni bonge moja la ngoma ya kuombea msamaha kwa dem kama unezingua.
@cleansheet_1 Ww Jamaa bhana, 2011 nikiwa darasa la tano nilishuhudia barca akibeba ubingwa dhidi ya Manchester na 2015 nikiwa form two nilishuhudia barca akibeba ubingwa dhidi ya Juventus.
Eeh Mwenyezi Mungu,asante kwa yote uliyonitendea, kwa yale ninayoyaona na yale nisiyoyaona.
Asante kwa uhai, kwa ulinzi, kwa riziki, kwa watu ulioweka katika maisha yangu na kwa neema ya kusonga mbele.
Nisaidie nisizisahau fadhili zako hata ninapopitia nyakati ngumu.
Amina 🙏🏼
Kitu chochote kikizidi kiasi unachohitaji kinakuwa sumu, inaweza kuwa mali, uhuru, hasira, kiburi au chochote kile
Kila kitu kinapaswa kuwa kwa kiasi unachoweza kumudu
Kuna mtu mmoja kanipa tafakuri moja anasema “Ukiona unampigia mtu simu hapokei halafu baadae hakurudishii simu hadi umpigie wewe tena na pengine asipokee mara mbili mara tatu, bado thamani yako ni ndogo sana, unatakiwa kupambana kujiongezea thamani manake heshima huja palipo na thamani.” Mpaka sasa naitafakari sana sijajua ina ukweli kiasi gani?
Watu wengi hawataki kuwa sehemu ya mchakato wa mapambano, bali wanataka kuwa sehemu ya matokeo na mafanikio.
Wasichojua ni kwamba, mchakato huo huo ndio unaotufundisha nani tutaendelea naye baada ya mafanikio.