KATORO – GEITA. Mamma Mia! 🙆🏾
Watu ni wengi kama mchanga.
Kilio cha SHOSTI na wenzake tunakielewa.
Kwa huu mtiti, lazima watoe mlio.
Kazi ni moja. Kuyapelekea moto MaCCM.
Hii inaitwa ‘IGA UFE AU JARIBU UFILISIKE’
#PeoplesPower#StrongerTogether ✌🏾
Hili Dude Linapigwa mnada na TRA, Hii ni Ford F-350 2006 Model
.
Lilikua la Transit naona limefika Mkongo mambo yemekataa akalitelekeza na ni LHD
.
Matumizi yake makubwa ni for Towing kwa Lugha ya Tunguu ni Kuvuta Magari na Kubeba Mizigo
.
Pesa Wanayoitaka sasa ndo utashangaa👇
#Pichani
Huyu aliyeshika 🎤 ndo Shahidi wetu wa leo Coplo Vicent yeye kasema hajui PGO wala sheria yoyote ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kingereza.
Anasema yeye ni mpelelezi, anakamata watu kwa amri ya Polisi tu hata kama hajui wamekosa nini.😂😂😂
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 205
Mhe. Lissu anaendelea na Cross Examination.
Mhe. Lissu: katika maelezo yako kuna sehemu yoyote umesema mwenyekiti Tundu Lissu amesema tufanye vurugu?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana hakuna hayo maelezo
Mhe. Lissu: unafahamu maana ya neno uasi.
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: Ngoja nikwambia, waheshimiwa majaji namsomea shahidi maana ya uasi kutoka katika kamusi ya Kiswahili…swali langu kaka, waeleze waheshimiwa majaji kwa kuwapinga wenye mamlaka au taratibu zilizopo ni uhaini?
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: Shahidi mimi ninasheria ya uchaguzi hapa ya urais, madiwani na ubunge, sheria hiyo haina popote iliposema kuzuia uchaguzi ni kosa la jinai, wewe unasemaje?
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: hapa nina sheria kuu ya makosa ya jinai na hakuna popote iliposema kuzuia uchaguzi ni kosa la jinai, wewe unasemaje?
Shahidi wa kificho P3 : mimi sijui.
Mhe. Lissu: umeeleza mahakama kwamba ulipokamatwa tarehe 4 april 2025 na kwenda kuandikwa maelezo kwa tuhuma za kupanga njama za kuzuia uchaguzi, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P3 : kweli.
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji hizo tuhuma ziliishia wapi?
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama umefunguliwa mashtaka ya jinai ya kupiga watu mawe na kupanga njama za kufanya vurugu
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: ulipaanga njama na mapolisi ujifanye mwanachadema uje kutoa ushahidi hapa?
Shahidi wa kificho P3 : si kweli
Mhe. Lissu: kama si kweli kwanini hujafunguliwa mashtaka
Shahidi wa kificho P3 : sijui
Mhe. Lissu: kwa muda wote wa miezi mitano uliyokua unaenda kuripoti polisi, walikua wanakwambia nini?
Shahidi wa kificho P3 : walikua hawaniambii chochote, wananiambia niende
Mhe. Lissu: waambie majaji kama wakati wote unaripoti polisi waliwahi kukuuliza chochote kuhusu tuhuma zako za kupiga watu mawe?
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: nani alikulipia nauli ya kutoka Mbeya mpaka Dar es salaam
Shahidi wa kificho P3 : nimejilipia mwenyewe
Mhe. Lissu: hapa Dar es salaam umefikia wapi?
Shahidi wa kificho P3 : nimefikia guest
Mhe. Lissu: nani anakulipia?
Shahidi wa kificho P3 : najilipia mwenyewe
Mhe. Lissu: waeleze waheshimiwa majaji kama mpaka leo hii kuna kiongozi au mwanachama wa chadema aliyekutishia chochote juu ya maisha yako
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: waambie washeshimiwa majaji kama kuna kiongozi au mfuasi yoyote wa CHADEMA ametishia familia yako
Shahidi wa kificho P3 : Hapana
Mhe. Lissu: Kuna polisi ameleta kiapo mahakamani akisema kwamba shahidi kama wewe umetishiwa maisha.
Shahidi wa kificho P3 : Hapana mimi sijawahi kutishiwa maisha.
Mhe. Lissu: sina maswali tena kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru : Re-examination upande wa mashitaka.
Wakili wa Serikali: Sasa shahidi umeulizwa swali kuhusu huyo askari Polisi aliyekukamata, mheshimiwa Jaji naomba kielelezo, shahidi Sasa naomba usome kielelezo ukurasa wa mwisho mstari wa tatu.
Shahidi wa kificho P3 : wakati tunaendelea kubishana alikuja mtu aliyejitambulisha kwangu kuwa yeye ni Askari Polisi.
Wakili wa Serikali; kwa hiyo alijitambulisha kwako kuwa yeye ni?
Shahidi wa kificho P3 : kuwa yeye ni Askari Polisi.
Wakili wa Serikali: Shahidi umeulizwa swali na mshitakiwa kwamba kama kuna neno katika maelezo yako ‘kufanya vurugu’ ukajibu yapo, alivyokuonesha ukasema kuzuia Uchaguzi ndiyo kufanya vurugu zenyewe, sasa onesha uhusihano kati ya maneno kufanya vurugu na kuzuia uchaguzi.
Mhe.Lissu: waheshimiwa Majaji Sasa naona Wakili anataka kuelezea mambo ambayo shahidi ameyakataa, anataka kuintroduce kitu kipya.
Kama Mahakama itamruhusu kufanya hivyo nitaomba nimcross examine shahidi upya kwenye suala hilo.
Part 206 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Spare part hazipo huwezi enda ilala ukakutana nazo hapo ni mpaka Kuagiza Dubai au UK wanakoyatengeneza huko.
.
Mafundi wapo kwa hapa DSM wako hapo CMC Automobile, huyu ni official dealer wa gari baadhi za UK.
.
Hizi ndo garage unakuta fundi mkuu ni kama branch manager wa NMB kule Masasi so ujipange..
Inaitwa Forward Collision Warning (FCW) ikiwa na Emergency brake asssit bila kusahau Electronic Stability Control (ESC) na Traction Control (TCS)..
.
Hili kwenye Kona alibinuki labda ubinuke wewe imagine chuma ina ton 2.4, longer wheelbase halafu ina mifumo ya umeme ya stability..
So dude linakimbia [twin turbo] na top speed ni 320Km/hr na inafikika kipengele ni huku Tunguu uje na barabara yako tu ili uwezi kufika 320..
.
Na usalama wake ni wa hali ya juu imagine gari ina airbag 10 mpaka airbag za goti eti, lakini pia ikisense Ajali inaku alert+braking..
Koo lake ni kubwa sana so kuhusu mafuta hii halitumii ila linabugia, imagine within 4 second 0-100km hii hapa na gear number 4 unaitafuta, hii acceleration rate sio ya nchi hii..
.
Full tank linakula 90 Litres na mafuta ni 4-5Km/L na sometime inaweza kuwa chini ya hapo au juu kidogo kutegemeana a uendeshaji wako..
Ziko na hp 680-880 zikiwa linked na gearbox ya 8 Speed AT kutoka Porsche, Hizi ndo GB zenye dual clutch alafu Tiptronic..
.
Yani gear zina shifts extremely fast na unaweza hata usijue kama imebadilika, Imagine Gearbox kubwa kama engine ya Crown wewe ulishaona wapi ?
.
Hapa gear inadakwa kabla haijatoka nyingine ishaingia na inakupa feeling kama ya gari za mashindano na ukilikanyaga linaamka..
Ukienda kwenye engine huko ndio kuna balaa sio la nchi hii kuna engine option mbili 6.0 L W12 twin-turbo hii na 4.0 L V8 twin-turbo.
.
Hizi mbili ni Petrol engine, Yani cc 5998 na CC 3998 Jichanganye sasa Maana hapo machine ni cylinder 8 nyingine cylinder 12 bila kupepesa jicho.
Muonekano wa njee wa kibabe sana kuanzia grilles na taa zake za mbele badge ya gari, exhaust system etc hapa mtu wa Mungu endelea kuangalia picha..
.
Kuna gari uspeciall wake kuzielezea unaishiwa maneno inabidi uwe mtazamaji tu then ujifunze kwa picha..
.
Ndio maana hii machine inaitwa the ultimate driver’s limousine hapa kaiulize AI ina maana gani itakupa majibu..
Hizi situ ndugu yangu zina adjustment mpaka za kiuno [Lumbar support], Sasa kiuno kinakuaje adjusted hilo Daudi anaweza elezea vizuri..
.
Hapo ndani kuna mood lighting yani ukiwa na hasira machine inakuwashia taa za kuku calm, au ukiwa na mbebezi kuna taa zake pia..
Na hata taa za Ibada zipo, Inshort NI taa flani za ku control hisia kizungu wanaita mood lighting na haya mambo ni ya ki-masaki masaki sana kama umezoea balbu na gropu unaweza usielewe hapa, achana napo tu..
.
Music bana upo wa kutosha kwanza kuna speaker 10-20 kutokana na toleo husika zikiwa na watts 1500 to 2200 Yale mambo ya underseat sabufa humu hayafai..
Music uko na mfumo wa Beosonic unaoatoa music ulio sawa [Clear and balanced sound] usioumiza masikio unaoleta utulivu wa moyo na ukipiga singeli humu mfumo unakataa.
.
Infotainment yake ukiweka vents za AC steering dashboard ni za kipekee sana so far zina muonekanano wa kisasa Zaida katika uzao huu..
Nyuma katikati ya siti pale iko na refrigerated bottler cooler kwa ajili ya chupa mbili tatu, massage heating na ventilation unapata pia..
.
Control za ubaridi pia unapata bila kusahau kuna screen za inch 10-12 pale nyuma na vitu kama wireless charging na etc..
Kwa hii chuma huwezi sikia mtumiaji anauliza kama unacharge type C na kina USB iko na wireless charging system..
.
inshort mambo ni mengi siwezi yamaliza ila nimekugusia muhimu upate ka kitu uendelee kupambania katiba mpya.
.
Ina long wheel base kwa ajili ya kuwa na smooth riding lakini pia ina suspension za upepo [air suspension system]..
.
Hizi za upepo kuna raia wa Discovery huwa wanazitoa wanaweka za Tunguu pale Unguja mambo yasiwe mengi..
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 177
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Koplo Michael.
Mhe. Lissu: Kwahiyi P8 alikuwa amefanya kosa?
Koplo Michael: ni kweli alikuwa amefanya makosa
Mhe. Lissu: Kwahiyo maelezo yake hayapo?
Koplo Michael: Sijayaleta
Mhe. Lissu: Je mlifungua kesi?
Koplo Michael: Hatukufungua kesi.
Mhe. Lissu: hadi leo hamjafungua?
Koplo Michael: Sijui kwakweli.
Lissu: RCO ndio alikwambia chukua maelezo ya shahidi kwenye kesi ya Lissu.
Shahidi: Hapana sio hivyo.
Mhe. Lissu: anamsomea alipoandika kuwa shahidi kwenye kesi ya lissu.
Koplo Michael: Ni kweli nilisema kumbe.
Mhe. Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa kesi ya Lissu?
Koplo Michael: Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kwahiyo mlikuwa mnaandaa nini?
Koplo Michael: Ushahidi wa kesi.
Mhe. Lissu: Kesi gani?
Koplo Michael: hii ya kwako.
Mhe. Lissu: Kumbe ni yangu umebana umeachia.
Watu; 😂😂😂😂
Sasa tuendelee na swali lingine.
Mhe. Lissu: Nilitishia Serikali kwasababu nilisema tutazuia Uchaguzi, wambie Majaji ni wapi umesema neno lolote juu ya maneno niliyosema?
Koplo Michael : mimi nilisema aliyoniambia shahidi.
Mhe. Lissu: Umeelewa swali we polisi?
Koplo Michael: Hapana sijasema lolote kuhusu maneno gani ulisema.
Mhe. Lissu: naambiwa nilichapisha maneno mitandaoni sasa sema kama kwenye kielelezo D5 kama ulisema chochote kuhusu maneno yangu niliyochapisha.
Koplo Michael: Hapana sikuandika lolote kwenye hayo.
Mhe. Lissu: Kutaka mabadiliko ya Katiba, Tume Huru ya Uchaguzi ni kosa la jinai?
Koplo Michael: Sio kosa la jinai.
Mhe. Lissu: Kuhamasisha wananchi nchi nzima kupatikana Katiba Mpya na kuzuia uchaguzi ni kosa?
Koplo Michael: ni kosa
Mhe. Lissu: Kosa gani?
Koplo Michael: Mimi sio mtaalamu wa sheria, wanasheria watasema.
Mhe. Lissu: Huna unalojua wewe ni Koplo tu, umetaja Katiba tutajie ibara sasa?
Koplo Michael: Sijui kosa ambalo umeshitakiwa nalo.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru: Re Examination.
Ignas Anasimama anasema nina maswali mawili.
Je uliposema hakuna utofauti ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Nilimaanisha hakuna tu tofauti maana ni ile ile.
Wakili wa Serikali: Je ulisema hujui anashitakiwa na kosa gani? Ulimaanisha nini?
Koplo Michael: Najua ni uhaini lakini uhaini ni mpana unajumuisha uchochezi na kuharibu mali.
Wakili wa Serikali ni hayo tu Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnasemaje?
Renatus Mkude: Tunaomba tuendelee Jumatatu.
Jaji Ndunguru: Kwanini msiendelee na shahidi mwingine atakapoishia ikifika saa 11 tunaacha.
Mkude: Mh. Jaji naomba tuendelee jumatatu tafadhali muda umeenda.
Jaji: Basi jumatatu saa tatu kamili asubuhi tukutane.
Inapigwaa Courttttttt tunatoka.
Naomba Repost yako.