Kuna umri ukifika stress zako zinatakiwa ziwe kuhusu kutimiza ndoto zako, majukumu ya familia yako
Kazi na pesa na sio kwa ajili ya nani anakupenda na nani hakupendi au nani anaongea na nani haongei na wewe. Angalia na zingatia maendeleo na ukuaji wa maisha yako
Good Morning
Kuna wakati inabidi utumie pesa kusave muda, hivyo hvyo,,,kuna wakati inabidi utumie muda kusave pesa. Kwahyo kuwa makini na matumizi ya muda na pesa kinyakati.
Good morning x familia
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 254
Anasimama Wakili wa Serikali Ignas Mwinuka anasema Presidential Affairs Act kifungu cha 9 kinasema wito wa summons maana yake unamlazimisha shahidi kufika.
Kifungu hicho cha 9 kinasema anakisoma. Kwahiyo kwa mujibu wa kifungu hiki Mahakama haina mamlaka kutoa wito wa ku compell Rais kufika Mahakamani.
Naomba kuwasilisha.
Anasimama Wakili mwingine wa Serikali Job Mrema nae, anasema naomba kuunga mkono hoja.
Jaji Ndunguru : achana na mambo ya kuunga mkono hoja, Nenda kwenye hoja
Mrema anasema Section 24 ya TISS CAP 406 kinasema kuhusu protection of source of information.
Yaani usiri wa taarifa kwa kuzingatia mshitakiwa ametaja baadhi ya mashahidi mfano DGIS yaani Mkuu wa Usalama wa Taifa aje hapa Mahakamani. Anataka kupata taarifa kwa mashahidi hawa ili apate kujitetea.
Sasa kwa cheo cha shahidi huyu anafungwa na masharti ya sheria hii hata akija hapa hataweza kusema kila kitu. Na sio sahihi kabisa. Kuna limitation kwa mujibu wa sheria.
Kifungu hicho kimeweka penal sanctions yaani kutoa ushahidi huo ni kosa kubwa la kisheria.
ππ Lissu alisema mmeyataka mtayapata. Ngoja tuendelee.
Job Mrema anaendelea kusema naomba kufanya marejeo kwenye shauri la criminal appeal Jacob Tiifunga vs Republic Criminal Appeal No. 185/1980. HC Tanzania at mwanza. TLR.
Mahakama ilisema a trial magistrate has descretion to call witness yaani Mahakama ina uwezo wa kukataa shahidi kuitwa. Lakini kwa mujibu wa msingi uliotengenezwa kwenye kesi hii ni kuweka sababu. Sasa sisi tunasema sababu tulizotoa kuanzia shahidi namba moja SAMIA hadi namba 7 mashahidi wasiitwe kwenye shauri hili kwa sababu tulizozieleza na ni hoja yetu kuwa mnayo mamlaka ya kukataaa. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama anacho cha kusema
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji kabla sijaanza naomba kidogo kufanya consultation na Mawakili wangu kabla sijaanza, 5 minutes its enough...
Mawakili wa Lissu wakiongozwa na Dr. Nshala, Jebra, Matata, Paul Kisabo, Deogratias Mahinyila, Madeleka namuona Wakili Kisabo amesimama akimuonyesha Mhe. Lissu sheria kwenye laptop, Lissu anasoma na wanaendelea kujadiliana.
Wamemaliza kujadiliana
Mhe. Lissu anasema
Kuhusu hoja ya mimi kuwataja mashahidi wangu ninaotegemea kuwatumia kwenye kesi hii. Katuga amesema hoja hii na ukweli ni kwamba toka Kisutu hoja hii ilikuwa na shida.
Mgogoro specific ni kwamba Hakimu Mkuu Mkazi Franco Kiswaga baada ya mtuhumiwa kumwambia kuwa ana mashahidi na kuanza kuwataja akakataa kuwarekodi hao mashahdi.
Na hoja yake ilikuwa ni hao utaenda kuwataja Mahakama kuu. Mimi siandiki utaenda kuwataja Mahakama Kuu.
Baada ya shauri kuletwa hapa Mahakama Kuu Waheshimiwa Majaji nilileta hoja kwamba utaratibu mzima wa committal proceddings ulivurugwa kwa makusudi na nikawaambia majina ya mashahidi wangu wa utetezi yalikataliwa.
Nililileta mbele yenu na mkasema wenyewe kuwa utakapofika wakati wa kujitetea utaapata fursa ya kuandaa utetezi wako. Na mkasema niawatajie majina mnaotaka niwaite.
Nikawatajia na Mkaandika kwenye rekodi.
Katuga akasema ukurasa wa 186 wa proceedings orodha ipo na mliwaandika wenyewe Majaji.
Jambo hili sio la leo. Lipo kwenye rekodi za Mahakama hii, anachotaka Katuga mfanye ni mjikane wenyewe.
Anataka mjioneshe kuwa hamna akili sasa hiyo ni juu yenu sio kwasababu majina ya mashahidi hayajawahi kutajwa.
Yalitajwa Kisutu, yakatajwa kwenu na leo nimerudia tena.
Amueni mtanipa haki hiyo ya kupata mashahidi au mjikane.??
Mimi napendekeza msijikane, msikubali huo mwaliko wa kujikana. Vinginevyo kosa kubwa kuliko zote Mahakama hii itathibitisha kuwa haina uwezo wa kutenda haki tena kwenye Kesi ambayo adhabu yake ni kifo, mtaonesha kuwa hamna uwezo wa kutenda Haki na mtageuzwa Kangaroo Court. A court of star Chamber Court.
Hoja ya kifungu cha 281 na 314(2) mlishaandika majina ya mashahidi last year. Has already been taken by your own order.
Part 255 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Good morning π
Wapo wanaotuona katika hali tuliyonayo leo na kudhani hiyo ndiyo hadithi yetu yote. Hawajui kuwa nyuma ya mavazi yaliyochakaa kuna mtu anayepambana kimya kimya, anayevumilia uchovu, maumivu na changamoto ili siku moja afikie maisha anayoyaota.