‼️HABARI MBAYA‼️
Familia ya Jafari Saidi Kahise inaomba msaada wa wananchi katika kumtafuta ndugu yao ambaye hajulikani alipo tangu tarehe 5 Juni 2026.
Kwa mujibu wa familia, Jafari alichukuliwa tarehe hiyo katika eneo la Mtaa wa Madukani, Kihonda, Morogoro, akiwa katika kituo chake cha kazi cha bodaboda. Inadaiwa kuwa alichukuliwa na watu wanne waliojitambulisha kuwa askari polisi waliokuwa wamevaa mavazi ya kiraia.
Tangu siku hiyo, familia haijapata taarifa zozote kuhusu mahali alipo wala hali yake. Juhudi za kumtafuta zimeendelea kufanyika kupitia mamlaka mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi, ambalo familia imesema limekuwa likitoa ushirikiano katika kufuatilia suala hilo.
Mtu yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kufahamu alipo Jafari Saidi Kahise au aliyemuona tangu tarehe 5 Juni 2026 anaombwa kuwasiliana kupitia namba zifuatazo:
0680340487
0654777333
0685574592
"Lissu hana kosa, anachosema ni kwamba rasilimali za Nchi hii zitumike kwaajili yetu sote na ndiyo maana tunakuja tunasema mzizi wa fitna wa mambo yote haya yatakatwa na Katiba mpya. Na tunazunguka sasa hivi kuwaomba watanzania wote mtuunge mkono kwenye suala la kudai katiba mpya na kuwaambia wamuachie Lissu, wasipitusikiliza kwasababu Nchi hii ni ya kwetu sote tutaenda hatua ya pili."
"Huu ndio ujumbe wetu kwenu na tunazunguka kusema, hatuna chuki na mtu, hatuna hasira na mtu lakini tunashida na Nchi yetu inavyoendeshwa." Amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania bara Bw. John Heche, akizungumza na wananchi wa Nachingwea kwenye Viwanja vya Mahuridi, Majengo C leo Alhamisi Juni 18, 2026.
All Scripture is given by inspiration of God, and is profitable for doctrine, for reproof, for correction, for instruction in righteousness, that the man of God may be complete, thoroughly equipped for every good work.
2 Timothy 3:16-17