#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 1
Maombi haya yanasikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Mh. A. Mruma, Dr. A. Rumisha na Dr. E. Longopa.
Kiongozi wa Jopo hili ni Mheshimiwa A. Mruma.
Nawaona waleta maombi wote wapo. Lakini pia Mawakili wao wapo ambapo jopo la mawakili wao linaongozwa na Wakili John Seka, akisaidiwa na Edson Kilatu na Selemani Matauka.
Lakini pia Chama cha Mawakili Tanganyika kinawakilishwa na Wakili Emmanuel Ukashu.
Namuona Mkuu wa Gereza la Ukonga tayari ameshaingia hapa Mahakamani amekaa nyuma ya mawakili pale. Ni Dingi mmoja mrefu, mweusi amevaa Kaunda Suti na kitambi kile cha maaskari wa magereza.
Maandalizi ya majaji kuingia yamechukua muda mrefu sana.
Wanaingia sasa imepigwa High Courtttttttttt.
Mhe. Lissu hajaingia bado.
Majaji ni kama wanashangaa, mbona Lissu hayupo maana hawamuoni kizimbani.
Anatoka karani kwenda kuwatafuta magereza kwasababu hawapo kabisa hapa Mahakamani.
Wameanza kuingia maaskari magereza wa kutosha. Wanajipanga, muda sio mrefu ataingia Mwenyekiti. Tunamsubiri.
Ameshaingia akiwa na na Kombati yake ya Kaki na mifuko yake iliyobeba nyaraka zake, anazitoa taratibu pale anaweka mezani na majaji wanateta.
Anasimama Wakili wa Serikali baada ya jalada kusomwa hapa.
Naitwa Stanley Kalokola, Wakili wa Serikali nitasaidiwa na Francis Wisdom. Mjibu maombi wa nne yupo mbele ya Mahakama yenu na interested party TLS wapo.
Tuko tayari kuendelea na zoezi la DODOSO kwa siku ya leo.
Wamehojiwa waleta maombi na pande zingine wote wako tayari.
Mhe. Jaji Mruma anasema sasa 4th Respondent usikae kwenye kizimba ukae huku kawaida maana hii ni kesi ya Kikatiba.
Mhe. Lissu amesema naomba nikae hapa hapa maana nina meza na nitakaa vizuri nikiwa hapa.
Jaji Mruma akasema hakuna shida kaaa hapo hapo.
Basi ameitwa mleta maombi wakwanza Maduhu William aanze kuulizwa maswali ya Dodoso na Mhe. Lissu.
Jaji anasema ni vema ukaapa kwanza. Wewe ni afisa wa Mahakama unajua kuapa haya apa sasa.
Wakili Maduhu: Nina miaka 36 ya kuzaliwa. Mkristu, na anaaapa hapa tena.
Jaji: Bwana Tundu Lissu karibu.
Mhe. Lissu: shaidi naomba nikuulize maswali kuhusu kiapo ulicholeta mahakamani na kesi uliyoileta Mahakamani dhidi ya sisi walalamikiwa wanne.
Waeleze majaji kama hapo ulipo una nakala ya hati ya madai na kiapo chako.
Wakili Maduhu: Vyote ninavyo hapa.
Mhe. Lissu: Je una nakala ya hati ya viapo kinzani yaani counter affidavit za walalamikiwa wakwanza hadi wanne pamoja na interested party.
Wakili Maduhu: Ninazo hizo nyaraka zote.
Mhe. Lissu: Tuanze na hati yenu ya madai na kiapo chako katika aya ya kwanza ya originating summons na aya ya pili ya kiapo chako.
Angalia Je kwenye hizo aya umesema wewe ni mmojawapo wa mawakili wangu katika kesi ya jinai iliyopo katika mahakama hii. Umesema wewe na wenzako ni mawakili pia wa kesi yangu iliyopo kisutu.
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Naomba uangalie aya ya nne ya hati ya kiapo kinzani ya wajibu maombi wa kwanza hadi watatu na hicho kiapo kilitolewa na Andrew Shaban kilitolewa Tarehe 09/04.
Huyu Andrew anasema wewe hujawahi kutambulishwa kwake kuwa ni mmoja wa Mawakili wangu.
Wakili Maduhu: Ni kweli huyu Andrew amesema mimi sio Wakili wako.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli hii kesi iliyopo Mahakama Kuu ilianzia Mahakama ya kisutu ambako ilikuwa ni (P.I)
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Na hiyo kesi ilikuwa mbele ya Kiswaga pale Kisutu?
Wakili Maduhu: sahihi.
Mhe. Lissu: Angalia majibu yangu kwenye hili shauri lenu, kwenye majibu yangu kuna viambatanisho kadhaa. Angalia annexure A2N24R umekiona?
Wakili Maduhu: Nimekiona.
Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 19 wa hizo proceedings angalia waliokuwepo Mahakamani tar. 06/05 angalia corum kuhusu mtuhumiwa. Je jina la Maduhu lipo?
Wakili Maduhu: Ni kweli lipo.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
@joeselasini Hii nchi bora tungebaki kuwa koloni la uingereza tu maana uhuru huu hauna maana yoyote.
- Mkoloni alijenga shule
- Mkoloni alijenga barabara na reli
- Mkoloni alijenga mahospital
- Aliajiri watu
- Ulinzi wa raia ulikuwa mzuri.
@eastafricatv Anguko la matumizi ya mafuta linakuja. Huu ni mkakati wa kumdhoofisha Mwarabu na mafuta yake kwani mbadala wa mafuta ni umeme. Magari, pikipiki na bajaji za umeme zinanunuliwa kwa kasi!