#TajiriLaKihaya
KUNA MASWALI MAKUBWA YANAYOPASWA KUJIBIWA MUHIMBILI NA JKCI.
Leo familia yetu imepoteza mdogo wetu. Moyo wangu umejaa huzuni, uchungu na maswali mengi ambayo hadi sasa hayajajibiwa.
Siku ya kwanza nilipofanikiwa kumpeleka mdogo wangu JKCI na kupata chumba cha VIP, nilifurahi sana. Niliona kama tumepata mwanga wa matumaini. Baada ya vipimo, tuliambiwa tatizo lake la moyo lilihitaji upasuaji mdogo tu na angeweza kuendelea na maisha yake kawaida.
Tukaahidiwa upasuaji ungefanyika ndani ya siku mbili au tatu.
Lakini siku zikageuka wiki.
Kabla hata ya kulazwa, tulikuwa tumepambana kwa zaidi ya mwezi mzima tukizungushwa kutoka leo hadi kesho. Mara daktari hayupo, mara jopo la wataalamu halijakaa, mara kipimo kirudiwe, mara tusubiri dawa zifanye kazi kwanza. Kila siku ilikuwa ni ahadi mpya na tarehe mpya.
Baada ya kulazwa tuliamini safari ngumu imekwisha. Lakini ndipo mateso makubwa zaidi yalipoanza.
Mdogo wangu aliingia hospitalini akiwa bado anaweza kutembea, kuongea, kula na kujitambua. Kila siku tulisubiri upasuaji ulioahidiwa, lakini haukufanyika. Badala yake hali yake ilianza kuzorota mbele ya macho yetu.
Wiki moja ikapita.
Wiki mbili zikapita hadi wiki tatu
Hakukuwa na upasuaji.
Kulikuwa na sababu mpya kila siku.
Kisha tukahamishwa kutoka chumba tulichokuwa tumepewa kwa madai kuwa kingefanyiwa fumigation. Lakini usiku huo huo mgonjwa mwingine akawekwa kwenye chumba hicho. Hadi leo hatujui ukweli ulikuwa nini- lazima UFISADI ULITUMIKA HAPA!
Tulihamishiwa chumba kingine JAPO kilikua VIP… ila hakikua kwenye standard sawa!
Hata nakumbuka kuna Daktari wa Kihindi alikuja kusoma vipimo akasema ile MONITOR haipo sawa! Mapigo ya moyo na oxygen haisomeki kwa usahihi…
Sasa kwa nn tulihamishwa chumba? Kutoka chumba kizuri kuja hiki?? Kwa nn kile tulichokuwepo alipewa mwingine usiku huo tumehamishwa? CORRUPTION!
Baada ya hapo hali ya mdogo wangu ilizidi kuwa mbaya zaidi. Akapoteza nguvu, akashindwa kuzungumza, akashindwa hata kuwatambua watu waliomzunguka.
Tulikuwa tunauliza maswali. Tulikuwa tunaomba msaada. Tulikuwa tunaomba hatua zichukuliwe haraka.
Lakini muda uliendelea kwenda.
Leo asubuhi mdogo wangu amefariki dunia.
Siandiki haya kwa hasira pekee. Naandika kwa maumivu ya familia iliyokuwa na matumaini makubwa ya kumuona mpendwa wao akirudi nyumbani akiwa mzima.
Kama kweli kulikuwa na uzembe, kucheleweshwa kwa huduma, ukosefu wa uwajibikaji au mifumo mibovu ya utoaji huduma, basi kuna haja ya uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa. Maisha ya Watanzania yana thamani. Wagonjwa hawapaswi kupoteza maisha wakisubiri tarehe nyingine, kikao kingine au ahadi nyingine.
Tunataka majibu.
Tunataka uwajibikaji.
Na zaidi ya yote, tunataka familia nyingine isipitie maumivu tuliyoyapitia sisi.
Kama hapa ni VIP… je wagonjwa wa kawaida wanapata huduma gani???
Pumzika kwa amani mdogo wangu. Tulipambana kwa kila tulichoweza. Mungu akupokee katika makao ya milele. 💔🕊️
#TajiriLaKihaya@TaasisiMoyoJKCI kuna maswali muhimu hamjayapatia Majibu kwenye hili andiko langu!
Mmetoa taarifa ya juuu juu saana!
Kwa nini mlimuHAMISHA CHUMBA??
Kwa nn chumba mlichomhamishia mapigo ya moyo na pressure hayakua yanasoma kiusahihi…??
Hadi yule daktari wa kihindi alipokuja kupima na kipimo chake ndio tukagundua hilo na bado hamkubadilisha??
Mgonjwa wetu alikuja akiwa mzima… ila mlipomlaza tu hali kila siku ikazidi kuwa mbaya???
Kwa nn manesi kuna dawa walikuwa wanaambiwa wampe mgonjwa… ila hawampi kwa wakati hadi tena madaktari watakapopita waulizie kama kapewa ndio wampe???
Maswali ni mengi saaana…
Star Cape Verdean goalkeeper Vozinha and his mother will be reunited in Miami in time for the match on Sunday.
Thank you to Secretary Rubio, U.S. State Department officials, the government of Cabo Verde and FIFA for working together to make this happen.
FOR THE FIRST TIME IN 53 YEARS, THE KNICKS ARE NBA CHAMPIONS 🏆
New York defeats San Antonio 4-1 in the NBA Finals, capturing their third championship in franchise history!
@TheTrueVanguard Plus also you start splitting up the player base even more in a game where we need more players right now will not be good. I run solos with free kits to do objectives but if I'm in a team I take the best gear I got coz I don't wanna be the weak link on the team