Tume huru ya taifa ya uchaguzi imeanza rasmi zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kwa awamu ya pili ambapo watendaji wa uboreshaji ngazi ya halimashauri katika wilaya ya kilosa wametakiwa kuzingatia uadilifu na uaminifu katika zozi hilo.
Viongozi wa Vyama vya Siasa Wametakiwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili linalotarajiwa kuanza Mei 16 hadi 22 Mwaka huu ili waweze kuhakiki na kurekebisha taarifa zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imechukua hatua ya kuboresha usimamizi na ufatiliaji wa marejesho ya mikopo inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kwa kununua gari Land Cruiser yenye thamani ya shilingi Milioni 226 kupitia fedha ya marejesho ya 10%.
Katika kikao cha tathmini ya lishe kwa robo ya tatu kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri Wilaya ya Kilosa, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe Shaka Hamdu Shaka, ametoa wito kwa wazazi, walimu, na watendaji wa kata kushirikiana na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana.
Katiak kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa leo Aprili 26, 2025 imeadhimisha siku hiyo kwa kupanda miti 158 katika shule ya Msingi Lamlilo iliyopo kata ya Magomeni
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imepokea miche 16,000 ya karafuu kutoka katika Taasisi ya TAHA na kuisambaza kwa baadhi ya shule ambapo shule hizo zitaanza kuvuna mazao hayo na kupata fedha zitakazo saidi kununua chakula ikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula shule
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. Ismail Ali Ussi akiweka jiwe la Msingi katika barabara kiwango cha Zege kutoka Ruaha Kona Hadi Kilomero ii yenye urefu wa km 0.71 mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi 949,316,350 kukamilika fedha kutoka serikali kuu
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amekabidhi msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum ikiwa ni zawadi maalum ya Eid El Fitr ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo kwa Kilosa imetolewa kwa Shule ya Msingi Mazinyungu na kituo cha watoto yatima Dumila
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeitaka halmashauri ya wilya ya Kilosa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusimamia matumizi ya fedha na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka ameandaa IFTAR maalum Machi 26,2025 nyumbani kwake ambapo viongozi mbalimbali wamealikwa katika hafla hiyo. IFTAR hiyo imeambatana sambamba na Dua ya kuliombea Taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan
Katika kuadhimsha siku ya Misitu Dunuani na siku ya upandaji miti Kitaifa, Wilaya ya kilosa Machi 22, 2025 imeadhimisha tukio la kihistoria kwa kupanda miti elfu mbili katika shule ya sekondari mazinyungu ikiwa ni kuunga juhudi za serikali kuhamasisha jamii kutunza mazingira
Waziri wa Mawasiliano na Technolojia ya habari, Mhe. Jerry Silaa ametoa agizo Machi 14, 2025 kwa makampuni ya Mawasiliano ya Simu Nchini kukamilisha ujenzi wa minara ya mawasiliano 758 inayoendelea kujengwa nchini kote ifikapo Mei 12, 2025.
Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, Wilaya ya Kilosa imefanya maadhimisho hayo Machi 5, 2025 katika kijiji cha Mbwade kilichopo kata ya Madoto ambapo Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu. Shaka .
Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Mhe. Denis Londo, amekabidhi gari la kubebea wagonjwa mahututi (ambulance) katika Kituo cha Afya cha Ulaya kilichopo Tarafa ya Ulaya wilayani Kilosa, akitoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta msaada huu muhimu kwa wananchi wa jimbo hilo.
Katibu Tawala wilaya ya Kilosa Bi. Salome Mkinga ameborsha taarifa zake katika daftari la kudumu la wapiga kura siku ya tarehe 3 Machi, 2025 katika kituo cha shule ya sekondari mazinyungu kilichopo kata ya Mkwatani.
Zoezi hilo litaendelea hadi tarehe 7 machi, 2025