Hiki alichokifanya @MariaSTsehai ni Ku raise Global Awareness yaan tunaweza kua tunahoja nzuri lakini watu hawajui nn kinatokea nchini. Alichokifanya ni kupeleka at Global level na ame deliver to the fullest.
Naomba msiaidie kumpa Repost za kutosha.
Thanks @OsloFF
Repost
@Jambotv_ Mpaka uchaguzi upite nadhani tutaona mengi ila CCM nadhani wanachama chenye wanachama wenye nidhamu sana. Ila awa wengine wanachama AKILI KISODA nadhani
BARUA YA WAZI KWA VIONGOZI WA CHADEMA.
Nawafikishia salamu nyingi za mshikamano (solidarity) na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Mwenyekiti kubambikiziwa kesi, wanachama kama Mdude na Soka kutekwa, wafuasi kushambuliwa na kuumizwa, na mengine mengi, ni kipindi kigumu.
Hata hivyo yote haya yanapaswa kutokea kwa sababu ni prerequisite ya mabadiliko. Kama mwenyekiti Tundu Lissu alivyowahi kusema, “kitakuwa kipindi kigumu kweli kweli;’ alimaanisha.
Lakini pamoja na ugumu wa hiki kipindi, kinatoa fursa nzuri pia ya kujifanyia tathmini (reflection) na kufanya marekebisho muhimu for take off.
Kitendo cha kundi la wanachama (viongozi wa zamani) waliokuwa wanamuunga mkono mwenyekiti Mbowe kutangaza kuachana na chama baada ya sarakasi nyingi kinatuma ujumbe muhimu sana kwa chama.
Je, chama kina wanachama waliovutwa na identity ya chama na wenye nia ya dhati ya kupigania cause au ni loyalists wanaokuja kumsifu na kumwabudu aliyepo madarakani?
Kwa mtizamo wangu, chama kilijikita zaidi (iwe kwa bahati mbaya au makusudi) katika kutengeneza au ku-attract kundi la pili badala ya lile la kwanza.
Badala ya kutengeneza vijana jasiri wenye uwezo wa kuwahoji hata viongozi wao, chama kilitengeneza vijana ambao no carbon copy ya vijana wa watawala.
Kilitengeneza vijana wenye sauti ya kukemea uchafu wa watawala halafu wakati huo huo wanakumbatia na kushangilia uchafu wa viongozi wao ndani ya chama.
Kilitengeneza vijana wenye ujasiri wa kuwaita wenzao chawa huku wao wakiishi tabia ile ile ya uchawa.
Matokeo yake ndio kama haya. Ilikuwa ni ajabu sana vijana wa chama kuona wazi mwenyekiti wao Freeman Mbowe akitoa tuzo kwa Rais aliyepersecute viongozi wake na wenyewe kunyamaza na kupiga makofi.
Ilikuwa ni ajabu kwa vijana wa chama kumwona mwenyekiti wake akishirikiana na watawala kuhonga viongozi wa dini na wao kupiga makofi tu kama wajinga.
Ilikuwa ni ajabu kwa vijana wa chama kumwona viongozi wake wakijikombakomba kwa mtawala na kumpa platform ya kujiuza kama walivyofanya kwenye lile tamasha la Sugu na wao kushangilia tu kanakwamba kila kitu ni sawa.
Ilikuwa ajabu sana kwa vijana wa chama kuona Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu akipewa akichangiwa pesa na wanachama wa CCM kwa dhihaka na masimango ya hali ya juu na yeye kukubali kuzipokea kisha wao wakampigia makofi kana kwamba ni hapo ya kawaida.
Ilikuwa ajabu kwa vijana wa chama kusikia viongozi wao wanajihusisha na pesa haramu za Abdul na Mama yake tena mpaka kufikia hatua ambayo viongozi wao wanatoka wazi na kukiri mahusiano hayo pasipo tone la regret na wao wakawanyamazia na kuwapigia makofi kana kwamba kila kipo sawa.
Ilikuwa ajabu sana kwa vijana wa chama kinachojipambanua kupigania demokrasia kusikia viongozi wake wakisema “mwenyekiti tuliyenaye ni wa milele” au “tunamtaka kwa sababu ana hela,” na wao wakanyamaza na kupiga makofi.
No no no, hii ni tabia ya unyumbu isiyopaswa kuonekana hata kidogo kwenye chama kinachojipambanua kama chama mbadala.
Mjumuiko wa kukosekana ujasiri wa vijana kuhoji na kuwajibisha viongozi wao, ujasiri wa kuangalia ndani kwa jicho lile lile unalotumia kuangalia nje matokeo ndio haya.
Hivi sasa chama kimepewa nafasi ya kujitakasa na kurudi kwenye mstari, ni jukumu lake kutengeneza watu wenye misingi thabiti na wanaoamini kweli katika cause.
Ni wajibu wa viongozi kuangalia upya mtaala na ideolojia zinazotumika kulea vijana wa chama ili kuhakikisha vijana wanaotengenezwa kweli wanakuwa na uwezo wa kusimama and kupotray identity ya chama ambayo kila mmoja atajivunia.
Huu ndio mtaji pekee utakaovuta sehemu kubwa ya umma na kuufanya ukiamini chama.
Umma ukiona yale yale ya CCM ndani ya CHADEMA, utakata tamaa kabisa na kuona “wote ni wale wale.”
Yours in solidarity
Onesmo Mushi
@ChademaTZ2