“Ndugu zangu wanachadema hakuna kosa kubwa la kimkakati kama kubadilisha Jenerali katikati ya Vita, niwaombe msibadilishe Jenerali katikati ya Vita” Hotuba ya mwisho ya Freeman Mbowe akiomba Kura kwenye Uchaguzi wa Chadema 2025.
Naungana na watanzania wote wenye upendo wa dhati na nchi yao, kutoa pole kwa familia, ndugu, na marafiki wa wote waliopoteza maisha au kujeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika siku ya uchaguzi October 29.
Ni huzuni kubwa kuona damu ya Watanzania ikimwagika katika kipindi ambacho tunapaswa kutumia sauti na busara kujenga demokrasia yetu. Maisha ya kila mtanzania ni yenye thamani, na kila tone la damu lililomwagika litukumbushe kuwa haki, amani, umoja na mazungumzo ya kijamii ni msingi wa taifa letu.
Kwa heshima tunaomba mamlaka husika kuchukua hatua za haki na za kibinadamu kuhakikisha ukweli unajulikana, wahusika wanawajibishwa na haki inatendeka bila upendeleo.
Kwa familia zilizoathirika, tuko nanyi katika maombi, huruma na matumaini. Mungu awafariji, na taifa letu lijifunze kuthamini uhai na utu zaidi ya tofauti zetu za kisiasa.
Taifa lenye amani ni taifa linalokubali ukweli, hata pale ukweli huo unauma. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
BABA umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza, Imani umeilinda Lala Salama JAKOM. AGWAMBO leo umelala katika makazi yako ya milele, hatuta kuona tena katika Dunia hii, Nenda salama Shujaa, umenitendea mema mengi, vizuri havidumu, FAREWELL TINGA, OSIEPA😭😭
"CCM haimiliki vyama vya Upinzani, Polepole aache upuuzi na asiendelee kuleta upuuzi, asikichafue Chama Cha Mapinduzi" Fadhili Maganya - M/KITI WA WAZAZI, CCM TAIFA.
“Chadema hatujutii kumbadilisha Jenerali Mbowe, Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, chama Kinasonga mbele, maamuzi ya wengi uheshimiwe” Adv. Matata - MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA.
“Hakuna anayeweza kukiua Chadema, hakuna chama cha upinzani zaidi ya Chadema ununu usinune, upende usipende, vingine vyote ni Vyama vya kwenye Flash” YERICKO NYERERE - ENZI ZAKE AKIWA CHADEMA