KABLA YA KUNUNUA KIWANJA AU NYUMBA AU SHAMBA FANYA UHAKIKI/UCHUNGUZI ILI KUJUA YAFUATAYO;
1)UMILIKI HALALI wa kiwanja hicho, ni vema kujua kama anae kuuzia ndio mmiliki halali wa kiwanja husika. Je ni cha urithi au sio..? Hakina wamiliki zaidi ya mmoja..? Kina hati miliki au hakina..? Je hakina wofia..? Kama upo unasemaje kuhusu hilo eneo..? Je hakina pingamizi lolote la mahakama au lililosajiliwa na wizara (caveat)..? Je hakina mkopo..? Hii itakusaidia kujiepusha na kutapeliwa.
Mfano,watu wengi waliotapeliwa na kubomolewa katika maeneo ya mapinga,vikawe,mbweni,bunju,mabwepande,mbopo nk wameuziwa viwanja kwenye mashamba ya watu au taasisi za serikali hivyo basi wangefanya uhakiki wa umiliki wangebaini umiliki halali na kutonunua maeneo hayo.
2)MATUMIZI sahihi yaliyoidhinishwa na serikali kama ni makazi,barabara,biashara,eneo la wazi nk. Kabla ya kununua ardhi hakikisha umejua matumizi yaliyopangwa kwenye hicho kiwanja na kama kimepimwa je kimepimwa kwa kuzingatia matumizi yake kama ilivyooneshwa kwenye mchoro wa mpango mji. Je huo mchoro wa mpango mji umeidhinishwa na wizara ya ardhi..? Hii itakusaida kujiepusha na kubomolewa. Mfano, watu waliobomolewa kimara walijenga kwenye maeneo ambayo yalipangwa kwajili ya barabara ya morogoro road,hivyo ni muhimu sana kuangalia matumizi ya ardhi kabla hujanunua.
3)KUTAMBUA MCHORO HALALI WA MPANGO MJI NA RAMANI HALALI YA UPIMAJI. Watu wengi sana hawajui kutambua mchoro wa mpango mji na ramani ya upimaji halali. Sio kila mchoro au ramani ukioneshwa ya viwanja ni halali zingine sio halali. Ili uwe mchoro halali wa mpango mji au ramani halali ya upimaji ni lazima iidhinishwe na wizara ya ardhi. Je unajua kutambua mchoro na ramani iliyoidhinishwa na wizara..? 😄 ramani ikiwa haijaidhinishwa na wizara eneo bado litaendelea kutambulika kuwa halijapimwa. Watu wengi kwa kutokujua hili wamenunua viwanja ambavyo havijapimwa ila wanajua vimepimwa ndio maana hawapatu hati miliki au hati miliki zinachukua muda mrefu kwasababu ulinunua kiwanja kwa kuoneshwa ramani ambayo haitambuliki na wizara lakini wewe unajua eneo limepimwa😄. Nicheck inbox au nipigie nikufundishe jinsi ya kutambua ramani halali.
3)BARABARA ya kufika na kutoka kwenye kiwanja, hili ni jambo muhimu sana kabla hujanunua ardhi hakikisha umejua barabara au njia za uhakika na za kudumu zinazoenda kwenye kiwanja unachotaka kununua, wengi wamenunua viwanja kwa gharama kubwa lakini wamejikuta hawana njia ya kufika kwenye maeneo yao😄. Epuka pia kuambiwa jirani ataacha njia ili hali huyo jirani hayupo na wala hajakubali mwisho wa siku jirani anazungusha fensi eneo lake unaendelea kutokuwa na njia.kama jirani anaacha njia ni vema akubali kwa maandishi au mbele ya majirani wote na viongozi wa mtaa au kijiji pamoja wewe ukiwepo usipewe tu taarifa,mara nyingi ukipewa taarifa inaweza kuwa ni katika kukufurahisha ili ununue eneo.
4)MIPAKA ni vema kukagua na kuthibitisha mipaka ya eneo unalotaka kununua kwa kushirikisha majirani wanao zunguka eneo pamoja na viongozi wa serikali za mtaa hasa kwa maeneo ambayo hayajapimwa ili uweze kujiepusha na migogoro ya mipaka, mfano, ile migogoro ya jirani kujenga kwa kuzidisha hatua au kujenga mpaka kwenye njia inaweza kutatuliwa kama mtajua mipaka yote kwa pamoja.
Zoezi hili linaweza kuwa ngumu kwako kwasababu linahitaji muda na utaalamu hivyo ni vema ukatafuta mtaalamu hasa mpima ardhi au afisa mipango miji au hata mwanasheria au ukaenda kwenye ofisi za ardhi zilipo karibu yako.
Pichani nikiwa 📍bagamoyo zinga, nikifanya uhakiki wa eneo kabla boss hajanunua. Baada ya kumaliza uhakiki niligundua eneo ambalo boss anataka kuuziwa lipo ndani ya EPZ hivyo haliwezi kupimwa wala kupatiwa hati miliki.
Ripoti yangu pia ilimsaidia boss kufanya maamuzi ya kununua au kutokununua kwasababu nilimpa ripoti yenye kila kitu nilichokibaini kwenye kiwanja husika.
Imeandikwa na;
Thom Mnkondya
(Mpima ardhi,mshauri na mtaalamu wa masuala ya ardhi kutoka LAPEX)
0744336336
Mwaka mwingine wa kuendelea kunukia Vizuri matumaini yangu wote mpo salama na leo Nawaletea list ya Perfume zilizofanya vizuri 2023.
10. Rave: Moja Kati ya perfume iliyopendwa sana 2023 inavutia Sana na harufu yake, nzuri sana kwa watu ofisini
Elfu 40 bei yake.
☎️0678213259
Sharing is caring:
Nilipoenda na mke wangu clinic kwa sababu ya mtoto wetu mchanga, tulifundishwa haya; waBABA tuna jukumu la kuwasaidia wake zetu kuyafanikisha⬇️
1. Jitahidi mara nyingi mtoto mchanga apate joto la wazazi. Mvue nguo mara kadhaa kisha hakikisha unamkumbatia na kuwa na skin contact.
2. Hakikisha mtoto ananyonya/anapata formula kila baada ya masaa mawili mpaka matatu, sio zaidi ya hapo. Hata kama amelala, mwamshe mtoto anyonye.
3. Hakikisha mtoto ananyonya ziwa moja la mama kwa dakika 20 kisha mhamishie ziwa jingine kwa dakika 20 hivyo hivyo mpaka ashibe.
4. Hakikisha mama anakula balanced diet, mbogamboga na matunda kwa wingi. Chakula kikiwa balanced na maziwa yatatoka kwa wingi, mama hahitaji chakula special anahitaji chakula balanced.
5. Kama mtoto ananyonya ziwa moja kisha analala, hakikisha mama anakamua ziwa jingine. Hii inasaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa sababu kadiri mtoto anavyonyonya zaidi ndivyo mwili wa mama unavyozalisha maziwa zaidi.
6. Mtoto ameshamyonya akashiba, msaidie acheue kwa kumlaza begani au mapajani na kumsugua juu ya mgongo taratibu. Ni vizuri mtoto akacheua mara kadhaa kabla hajalala.
7. Hakikisha mtoto analala kitanda chake au baby crib. FANYA VYOVYOTE UNAVYOWEZA MTOTO ASILALE NA WATU WAZIMA (IKIWEMO MAMA YAKE) au NA WATOTO WENGINE. Kumuua mtoto ni kitu Cha sekunde na usingizi hauna adabu.
8. Hakikisha mtoto analala sehemu plain isiyokuwa na kitu chochote karibu yake. Toys, vitambaa, etc., viondoe kabisa Karibu na mtoto.
9. Mtoto asifunikwe kwa blangeti wala shuka. Mviringishe kwenye kiblangeti au shuka lake vizuri huku mikono ukiibana ndani, hapo atalala mwororo kabisa.
10. Hakikisha mtoto anabadilisha diapers kila masaa mawili mpaka matatu, haswa anapokuwa mchanga.
11. Kwa angalau mwaka mzima, usimpe mtoto maziwa ya ng’ombe wala asali. Madaktari wanasema maziwa ya ng’ombe yana protein nyingi sana kiasi ambacho figo za mwanao haziwezi kuprocess lakini pia hayana nutrients anazozihitaji mtoto.
12. Jitahidi kuhudhuria clinic na mkeo.
13. Msaidie mkeo, haswa usiku; wanachoka sana.
HILI NI SOMO KUTOKA KWA PROF JANAB - HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI LINALOANGAZIA MASUALA YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA HASA LISHE.
- Elimu muhimu sana kwa kila mmoja wetu.
Kila mmoja wetu aone, madini adimu sana.
Video credit: @MuhimbiliTaifa
Karibuni sana katika Utumishi wa Umma, tunatarajia kupata changamoto mpya kutoka kwenu.
Mkafanye kazi kwa weledi na kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma
@George_Ambangil Chelsea Kwa kweli wanacheza kizembe sana, sio wazuri kwenye ulinzi, viungo Wala safu ya ushambuliaji, ni kama wachezaji wameokotana kijiweni, mimi sio kocha wala si mtaalamu sana lakini ukizama sana kwenye fikra hii timu haifundishiki.