Tusimsahau Niffer kwenye maombi ashinde kesi
Huyu dada ni mjasiliamali mkubwa sana
Ana influence kubwa sana mitandaoni kuliko wasanii wengi bongo
Na bado hakuogopa kusimama na wengi kipindi hiki
Tusimsahau Niffer kwenye maombi ashinde kesi
Huyu dada ni mjasiliamali mkubwa sana
Ana influence kubwa sana mitandaoni kuliko wasanii wengi bongo
Na bado hakuogopa kusimama na wengi kipindi hiki
Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Banson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
_______
Leo 8/5/2025, Papa wa 267 (Papa Leo XIV) amechaguliwa. Ni Mwana Chicago mwenzangu; Mwana CTU mwenzangu (CTU ni chuo kikuu cha Theolojia cha Kanisa Katoliki ambapo Bagonza kasoma hapo pia). Na ni Mwana Augustino mwenzangu (Msisahau Martin Luther alikuwa Padre wa O.S.A). Kwahiyo imekua siku njema kwangu.
Lakini pia imekua siku ngumu kwa sababu nimepokea taarifa kuwa โWASIOJULIKANAโ watakuja kunimaliza. Hivyo nimeambiwa niishi kwa tahadhari. Sishangai maana ukimfuga mbwa ukamwachia aonje damu za watu, huwezi kumdhibiti tena na hawezi kuacha mwenyewe.
1. Kama kweli wanakuja; WAMEKOSEA. Wanaichafua serikali na taifa kwa jumla.
2. Kama hawaji, pia WAMEKOSEA. Bado Wanaichafua serikali na taifa kwa kuwaza kuja.
Kama wakija, nawaomba wasiharibu milango ya nyumba yangu na kuwafanya wanangu nitakaowaacha yatima waanze kufikiria kuitengeneza upya. Waniite nitatoka nijikabidhi.
Kama hawaji; namshauri mfuga mbwa awafungie mbwa wake ndani. Si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya usalama wa mfunga mbwa mwenyewe na usalama wa kijiji chetu.
Huu ni mwaka wa uchaguzi. Hekima ni kutengeneza marafiki wapya kuliko maadui wapya. Usimuue mtu aliye tayari kufa. Hayo ni matumizi mabaya ya mauaji.
Awamu ya tano walikuja. Si lazima waje awamu ya sita hata kama awamu ya sita ni muendelezo wa awamu ya tano.
Iwe awamu ile au hii, hawa wasiojulikana ni waharibifu wa awamu zote mbili. Serikali makini (kama kweli haiwajui) ijitenge nao.
Wanaweza kufanya (kwangu) kwa sababu wameishafanya pasipotegemewa (TEC). Wakifanya wasijipongeze, wasipongezwe, na adhabu yao iwe ni kufanya MILELE.
Kama wakifanya; mwili utaoza, watu watalia, wengine watashangilia lakini watazaliwa wengine zaidi yangu.
Mungu analipenda taifa hili kuliko mimi ninavyolipenda. Hachelewi wala hawahi. Atasimama kulitetea.
Naishi katika jimbo la Waziri wa Mambo ya Ndani. Nina uhakika hajawatuma. Nawashauri wasitumie rungu kuua mbu aliyekaa kwenye kende za mfalme. Wala jiwe kumtungua kunguru aliyekaa kwenye kichwa cha Malkia.
Nawapenda Watanzania. Wakija kunichukua, tusipoonana tena, basi tutaonana kwa Baba kwa wale mlio na imani ๐๐ฝ
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi @Mwabuk2Boniface , ameonyesha kushangazwa na kimya cha Bunge la Tanzania katika kushughulikia masuala nyeti ya kitaifa, akilituhumu kuwa limekimbia majukumu yake ya msingi.
Akizungumza jijini Arusha hii leo Mei 8, 2025 katika mkutano wa TLS uliojadili hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, Mwabukusi amesema ni aibu kwa Bunge la Tanzania kushindwa kujadili masuala kama ukiukwaji wa haki za binadamu, usalama wa raia, vitendo vya utekaji na kupigwa kwa baadhi ya wananchi, pamoja na kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.
โMambo haya yangepaswa kujadiliwa na bunge letu, lakini leo hii tunaona Bunge la Ulaya ndilo linayajadili. Hii ni ishara kuwa Bunge letu limekosa uthubutu na linaogopa wajibu wake,โ alisema Mwabukusi.
Kauli hiyo imekuja saa chache baada ya Bunge la Ulaya kuketi na kuijadili Tanzania, likitoa wito kwa Serikali kuhakikisha haki inatendeka katika kesi ya Tundu Lissu, na kuweka mazingira rafiki kwa vyama vya siasa, hasa upinzani, kushiriki uchaguzi mkuu ujao kwa uhuru na haki.
Ndugu zangu nimeumia sana ..! Tunaichafua nchi yetu wenyewe . Why tusikae na kuelewana sisi wenyewe ? Please hii mvaya kwetu . Ndugu zangu kweli tunabomoa bchi yetu kwa tamaa zetu . Nineumia sana hii ya kujadiliwa UE .
Martin Masese alikuwa akimnadi Mbowe wakati wa uchaguzi wa chama Wala hakujificha,Baada ya uchaguzi kumalizika aliendelea na kazi ya kupambana na CCM bila kuweka kinyongo,Leo hii wamehama waliokuwa na mapenzi na mbowe yeye amebaki Amechagua uhai wa chama
tumpe retweet 1000
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniphace Mwabukusi, ameikosoa vikali kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Homera, ya kutoa Shilingi milioni tano kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa mwanaharakati Mdude Nyagali, akisisitiza kuwa hatua hiyo inaleta hofu badala ya matumaini, huku akitaka hatua za haraka kufanyika kumrudisha Mdude akiwa hai.
โNinataka kusema Mdude hana thamani hiyo, Mdude siyo mwizi, siyo mhalifu, hadhulumu watu. Mdude ni mkosoaji,โ amesema Mwabukusi siku ya Jumanne, akisisitiza kuwa kukosoa ni haki ya kikatiba isiyopaswa kufananishwa na uhalifu.
Akizungumza kwa niaba ya kundi la Rafiki za Mdude, Mwabukusi ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na kutoweka kwa mwanaharakati huyo wanamrejesha akiwa salama, huku akiweka wazi kuwa utulivu wao si wa woga, bali wa hekima, na hawatovumilia kuvunjwa kwa haki za msingi.
Kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Homera, aliyesema siku ya Jumatatu kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kuongeza nguvu katika kuwasaka waliomteka Mdude, ambaye pia ni kada wa CHADEMA. Alisema serikali imetangaza zawadi ya Shilingi milioni 5 kwa yeyote atakayesaidia kupatikana kwa Mdude, awe hai au mfu โ jambo ambalo limeibua ukosoaji mkali kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu na wanasheria.
Katika hatua nyingine, Dkt. Homera alikutana na viongozi wa CHADEMA kutoka Mkoa wa Mbeya na Kanda ya Nyasa ofisini kwake, akiwatoa hofu kuwa serikali inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mwanaharakati huyo anapatikana. Alisema pia anatarajia kukutana na viongozi wa kimila kujadili hali ya sintofahamu inayozidi kutanda mkoani humo.
Tukio la kutoweka kwa Mdude, ambaye anafahamika kwa sauti yake ya ukosoaji dhidi ya serikali kupitia mitandao ya kijamii, limezua maswali mengi miongoni mwa jamii ya watetezi wa haki za binadamu, huku likichochea wito wa kuimarishwa kwa mifumo ya ulinzi wa haki za raia dhidi ya vitendo vya vitisho na ukiukwaji wa haki.