Sijawahi kuona taarifa rasmi ya Kipumbavu kutoka Ofisi ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama hii.
1.Taarifa hii haijakanusha badala yake imethibitishia umma kwamba ni kweli Wabunge wamejiongezea mshahara kutoka millioni 12 ya zamani kufikia Tsh million 18,tangu 2023.
2.Kama Mbowe angekuwa ameongea uongo na kulisingizia Bunge kuhusu wabunge kujiongezea mishahara hadi kufikia Tsh million 18,Wangejiamini na kumuita katika kamati ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge ili wamsute au Kumdhalilisha.
3.Mwenyekiti wa CHADEMA anashindwaje kujua mishahara ya Wabunge ikiwa bado ndani ya Bunge Kuna Mbunge wake mmoja wa CHADEMA, Mheshimwa Aida Kenan ambaye Chama kinaweza Kumuhoji lolote na Kumtaka taarifa yoyote kutoka ndani ya Bunge..?
4.Najua bunge wanachotaka kusema kwamba hiyo Tsh million 18 ni makusanyo ya mwezi ya Mbunge ukijumlisha mshahara pamoja na posho yake ya mafuta ya gari la mbunge kwa mwezi.
Kama ambavyo walikuwa wanachukua Tsh millioni 12 kwa mwezi walikuwa wanadanganya ni Tsh millioni 7 ndiyo mshahara na kiasi cha Tsh millioni 5 ni posho ya mafuta ya gari la mbunge ktk shughuli zake Jimboni (ukweli bado zote ni mali yake)
Kama kwa sasa wanapokea Tsh millioni 18 wanaweza kusema Tsh millioni 12 ndiyo mshahara halisi na Tsh million 6 ni posho ya mafuta ya gari ya mbunge jimboni.
Je kayika hali hii kwa mtu timamu anaewezaje Kukanusha ukweli kwamba kwa mwezi mbunge halipwi Tsh millioni 18..?
Sisi wananchi tunachotizama ni kiasi cha pesa Wanachoingiziwa Wabunge kwa Mwezi latika akaunti zao binafsi ambacho ni Tsh millioni 18 tangu mwaka 2023.
HOJA YETU WANANCHI.
kwanini Wabunge badala ya Kupambana kushusha gaharama na ukali wa maisha kwa wananchi wote badala yake wamejiongezea wao wenyewe mishahara kwa kisingizio hichohicho cha kupanda kwa gharama za maisha ambapo kila Mtanzania anapata maumivu sawa na wao.
Je sisi wananchi gharama za maisha kwetu hazijapanda.?
Mbona hawajatuongzea walimu,madaktsri,manesi,askari na wengineo mishahara kama wao..? Au sisi wananchi tumewaambia maisha siyo magumu na vitu havijapanda bei kama ilivyo kwao.?
Au tuone ongezeko hilo ni kama rushwa na kufumbwa mdomo na serikali katika kuibana serikali ndani ya Bunge na nje ya Bunge..?
Samia, tumekuonya sana. NEVER MESS WITH CATHOLIC CHURCH. Andika kwa wino mwekundu. Umemwaga petrol kwenye moto. Haumalizi muda wako. Hakuna mtawala amewahi kupambana na kanisa katoliki akashinda. Kama ni washauri wamekuingiza choo cha kiume. "The Holy Alliance" is on your tail.
Kesi mbili za jinai zinazomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu zinatarajiwa kusikilizwa leo kwa njia ya mtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
Kesi ya kwanza, ya uchochezi, yenye namba 202504102000008606, inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini ambapo imepangwa kwa usikilizaji wa awali leo, Aprili 24, 2025 saa tatu asubuhi
Kesi ya pili, ya uhaini, yenye namba 202504102000008607, inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Franco Kiswaga na imepangwa kwa kutajwa leo saa tano asubuhi, pia kwa njia ya mtandao.
Moja ya Kesi iliyotikisa Fani ya Sheria, katika utoaji Haki, ni Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Tabora (2006) Bw. Ditopile Mzuzuri (60), kumpiga risasi dereva wa daladala, Bw. Hassan Mbonde (33) maeneo ya kawe jiji Dar es salaam.
kugongwa kwa nyuma na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu.
Marehemu ambaye alifariki dunia papo hapo, alikuwa akiendesha gari aina Isuzu Journey, linalofanya biashara ya daladala kati ya Ubungo na Tegeta na lilikuwa likitokea Ubungo kwenda Tegeta.
Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa baada ya gari hilo kugongwa, dereva wa Ditopile, alishuka na kwenda kukagua uharibifu uliotokana na tukio hilo Kwa mujibu wa mashuhuda hao, gari hilo lilivunjwa taa moja ya nyuma.
Mashuhuda wa Tukio hilo wanasema wakati dereva wa Ditopile Bwana nasoro akiendelea kukagua gari, Ditopile naye alishuka kuungana na dereva wake kukagua uharibifu wa gari hilo, Ditopile alimfuata Marehemu(Dereva wa Daladala) na kumuamuru ashuke ili aangalie uharibifu aliofanya
na waende polisi, Lakini marehemu alimueleza ditopile amsamehe maana ajali hiyo imetokea bahati mbaya
Bahati Mbaya Ditopile hakukubaliana Msamaha huo na kuendelea kumwambia dereva(Marehemu) ashuke na kumwambia maneno hayo ataeleza polisi
Mashuhuda wanasema Marehemu alipoona ditopile anazidi kutoa maneno ya ukali alifunga kioo cha gari ili kuepuka kuchochea hasira za kiongozi huyo
Jambo hili lilimkwaza sana ditopile na kumfanya atoe bastola yake na kuanza kuitumia kugonga kioo cha gari hiyo