Yajuwe Mafanikio Yenye Ulemavu.
Ni mafanikio yenye upungufu hasa katika suala zima la Afya. Hela unazo lakini hiki usile na kile usile tena vile vitu vitamu. Sehemu kubwa ya hela uliyoitafuta kwa shida inaishia Hospitali za nyota 5. Hali hii inawatesa wengi katika matajiri.
Maisha ni uwiano wa kazi na kula bata.
Unapotafuta maisha usisahau kuishi.
Kutafuta ni vizuri na kutojisahau ni vizuri zaidi. Kula vizuri na kuishi pazuri ni sehemu ya maisha. Wakati ukitafuta maisha ya watoto wako usisahau kuishi. Kujipenda sio ubinafsi bali ni kujithamini.
HIZI NDIZO BIASHARA UNAZOWEZA KUFANYA KWENYE MIKOA 26 YA TANZANIA.
Pia nimeunganisha na mawazo 190 ya biashara
Kupata hii PDF yenye Pages 10.
commment "nahitaji"
"Repost" hii post
Na, hakikisha umenifollow ili niweze kuingia kwenye inbox kukutumia.
📌
Usipoiheshimu pesa leo kwa kuitumia vizuri na ukafuata kanuni zake na nidhamu zake kesho lazima ikuadabishe na kukudhalilisha.
Ukiipata hela iheshimu.
Shikamoo pesa.
Philosofia ya kuja kuwa tajiri siku zijazo ni kuwekeza kwanza uje kutumia baadae.
Philosofia ya kuwa maskini ni kutumia kwanza ili uwekeze kitakachobakia.
Uamuzi ni wako.
Wakati ukiwa unazisoma historia za wenzako kumbuka nawe kuna siku itasomwa historia yako.
Jifunze kutoka kwenye historia za uliowasoma ili usifanye makosa waliyoyafanya.
Kuna Umri Ukifika Kama MWANAUME Hutakiwi Kabisa Kuteswa na Mapenzi...Unatakiwa Kuteswa na MALENGO Yako Tub
Mwanaume Hatafuti Kupendwa...anatafuta HESHIMA!
P. S. Ukiwa na Miaka 30-47 Halafu unateswa na Mapenzi... You're a FINISHED Man!
Ukiitafuta hela/pesa utakufa hujazipata. Chukuwa SIRIi hii tengeneza mkondo uanzie kwenye kichuguu au juu ya mlima. Weka chombo cha kuzikinga kule bondeni taratiibu zitamiminika na utajaza. Hakikisha chombo chako hakivuji. Unataka kujuwa jinsi ya kutengeneza Mkondo wa pesa?
Kuna wakati Mungu anakupitisha kwenye matatizo ili uje kuwa na ushuhuda. Ukiona hakuna mtu anaekuchukia jikaguwe mara mbili. Usiifurahi kuona huna maaduwi, kama huna maaduwi ujuwe huna vita kwa sababu huna matokeo.
Biashara nyingi hufa wakati zinapokuwa kwenye mafanikio, kwa kuanza kujisahau na kupuuzia mambo ya Msingi yaliyowafikisha hapo wallipo. Usishangilie unapokuwa umepata mafanikio ni wakati muhimu kusimamia Mara mbili zaidi yale yalliyokufikisha hapo.
Pesa haiwezi kukaa kwa mtu ambae hawezi kumudu kuitunza.
Kuishi kwa Bajeti ni msingi wa mafanikio.
Je wewe unaishi kwa Bajeti? Niambie umetumia kiasi gani kwa nauli, chakula, vocha, umeme, maji n.k?
Furaha ya kweli haipo kwenye uwezo na namna unavyotumia, Bali Furaha ya kweli na yenye kuendelea ipo kwenye kuweka Akiba na kuiweleza pia.
Jenga utamaduni wa kuweka Akiba na Kuwekeza.