Niwape story nyingine ya Nabii AYUBU? ๐
Ukisoma Biblia AYUBU 1:1, Biblia inasema Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyoofu. ๐
Unajua kuwa mnyoofu wewe! Mungu alikuwa proud naye sana. Lakini kulikuwa wanoko ๐ wakasema, Mungu huyu unamuona yuko hivyo kwa sababu umempa kila kitu.
Chukua hivyo vitu vyake uone kama bado atakuwa mwaminifu kama unavyosema, Mungu akaona isiwe kesi ngoja tuone
Ghafla utajiri ukaondoka, mali zikapotea, watoto wakafa, na Ayubu akapata maradhi makali ya mwili.
Halafu wale wale Ma snitch wakaanza kusema, Hapana, lazima huyu kuna dhambi kubwa amefanya, Lakini pamoja na yote hayo, Ayubu aliendelea kushikilia imani yake.
Ndipo katika AYUBU 1:21 tunapata maneno haya
โBwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana libarikiwe.โ ๐๐พ
Guess what ๐ Baada ya kipindi chote cha mateso na maumivu, Mungu alimrudishia Ayubu kila kitu, tena zaidi ya alichokuwa nacho mwanzo. Hapo ni AYUBU 42:10.
Wakati mwingine hali ngumu tunazopitia kwenye maisha yetu si kwa sababu tunastahili, hapana. Wakati mwingine ni kwa ajili ya kutujenga, kutufundisha, na kutuandaa kwa kile kinachokuja mbele yetu.
Usikate tamaa katikati ya story yako. Mungu bado hajaandika mwisho wake. โบ๏ธ
Nisikie Amen kutoka huku nyuma.
Mwaka 2008 Wasabato Masalia walitinga Airport Dar wakitaka kwenda ng'ambo wakaeneze injili bila kuwa na documents yoyote kama visa, passport, tiketi nk
IMANI BILA ELIMU NI USHIRIKINA
#ElimikaWikiendi