@Mulastar255 Umetoka nyumbani kwako kwenda Benjamin Mkapa Hospital kurecordi hii video....
Ungefanya jambo la maana ungeingia wodini hapo usaport wagonjwa wenye uhitaji wa gharama za matibabu...
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 10
Wakili wa Serikali Kalokola anaendelea kumfanyia Cross-examination Wakili wa Mhe. Lissu Paul Kisabo.
Wakili wa Serikali Kalokola: Ushahidi wa Lissu na TLS unaunga mkono mambo mliyosema?
Wakili Kisabo: Ni sahihi.
Wakili wa Serikali Kalokola: Mwenye wajibu wa kuthibitisha ni nyie mlioleta kesi?
Wakili Kisabo: Labda kama umekariri lakini inategemea na aina ya kesi.
Wakili wa Serikali Kalokola: Kazi ya ushahidi ni kuthibitisha madai?
Wakili Kisabo: Ni kweli
Wakili wa Serikali Kalokola: Kwenye kupitia kwako sheria za Magereza uliona kifungu ambacho kinazuia idadi ya watu kumlinda askari?
Wakili Kisabo: Soma kanuni ya 33 utaona inasema nini inasema mfungwa wa mauaji ni askari wawili. Sasa Lissu sio amehukumiwa kunyongwa.
Wakili wa Serikali Kalokola : Kuna katazo la mtu kukaa lockup?
Wakili Kisabo: Sikia we Bwana, tunacholalamikia hapa kwamba hatupewi access ya kuongea na mteja wetu kwa usiri kama sheria inavyosema.
Wakili wa Serikali Kalokola: Na tunakubaliana Mkuu wa Gereza anao wajibu wa kulinda.
Wakili Kisabo: Kwa mujibu wa sheria.
Wakili wa Serikali Kalokola : Sasa kile chumba kinakinzana na sheria au vipi?
Wakili Kisabo: Hivi unajielewa kweli? Hapa hatuzungumzii ukubwa wa chumba tunazungumzia kusikilizana.
Wakili wa Serikali Kalokola: Mandela rule imesema ukubwa wa chumba?
Wakili Kisabo: Haihusiani na ukubwa wa Chumba inahusiana na wakili na mteja wake wasisikilizwe. Achana na mambo ya ukubwa hayatakusaidia.
Wakili wa Serikali Kalokola: Nimemaliza.
Anasimama Wakili wa Mhe. Lissu, Advocate Edson Kilatu kwa ajili ya re-examination.
Wakili Kilatu: Umeulizwa kuhusu afya za masikio za maaskari unasemaje?
Wakili Kisabo: Walikuwa wananisikia ndio maana kuna mambo wanasema usiongee nae jambo hilo maana yake wanasikiliza. Wangekuwa hawasikiii wasingekuwepo kazini.
Wakili Kilatu: Vipi kuhusu kile chumba na ukasema hujui kama kuna kifaa kinachorekodi. Ulikuwa na maana gani?
Wakili Kisabo : Ukiongea na simu maana yake mazungumzo ya simu yanarekodiwa. Lakini pale Ukonga kwenye kile chumba kuna control room.
Wakili Kilatu: Waheshimiwa Majaji Inatosha, nimemaliza maswali yangu.
Jaji anasema sasa mleteni shahidi mwingine.
Jebra unasemaje? Ahhhh samahani ni Seka unasemaje?
Seka: Sisi tuna nguvu tunaomba tuendelee.
Jaji: Lissu unasemaje?
Mhe. Lissu: Na mimi naomba niendeleee nae huyu Mkuu wa Gereza kuanzia sasa hivi.
Kuhusu suala la Jiografia ya barabara za Dar es salaam, naomba kuwapeni taarifa kuwa mimi huwa sikai foleni huwa barabara zinasafishwa na nina magari karibia sita. Ving'ora ni vingi sana kwahiyo mimi msinionee huruma kuhusu barabara.
Jaji Rumisha anasema: Sasa mazingira kama haya wakati mwingine huwa mnasema majaji tunapoteza muda. Lakini kumbe kuna wakati huwa wateja ndio huwa hamtaki kuendelea na kesi. Tutawalazimisha sasa? Kalokola unasemaje kwahiyo?
Kalokola: Ni kweli njia huwa ni nyeupe lakini kuna mambo yanafanyika nyuma ya pazia. Usione tu askari magereza wanatembea.
Jaji Rumisha: Haya tuendeleeni kesho asubuhi na mapema saa tatu.
Mahakama imeahirishwa.
Naomba repost yako.
@HildaNewton21 Wahadhiri wote nchi nzima wasimame nahili nasi wananchi tutawaunga mkono.... Wagomee kuendelea kufundisha, washinikize Serikali kumuachia Prof haraka sana bila masharti yoyote.