Ndio nikakuachia,Mimi si makamo yake
Kwako amekimbilia,kiruka njia mwenzake
Sasa unajisifia,eti Mimi nishituke
Ni radhi nimekuachia, chukua kwangu atoke
Unipunguke udhia na we pia yakufike
Vitamu ulivyotoa shubiri kwako na kwake
Huna haja kuchunguwa, Nayaelewa bayana
Kwangu hadhi hana tena,Chukua ufaidike
Chukua japo mchana,wala usipaparike
Mbele yangu nikiona,bure usifadhaike
Kwangu Mimi hakuhama,vizuri ifahamike
Lakini ameparama,kwa hivyo vituko vyake
Kama kwako bado nyama,kwangu Mimi ni matoke