🗣️ Tatizo lako unaongea ongea sana kuusema utawala…..
🗣️ 🗣️Wewe ipo watakuteka tu maana unaropoka ropoka sana….
🗣️🗣️🗣️ Oyaa acha kuandika andika mitandaoni kukosoa viongozi utapotezwa
Hizo ndio kauli watu wengi wanaambiwa na wanaamini wanaofanya hayo ndio Target ya watesi.
Sasa nikuulize umewahi kuona Mzee Kibao akiongea ongea mtandaoni kukosoa?
Umewahi kuona akiandika andika mtandaoni kuusema utawala?
Kwanza watu wengi ndio wamemjua baada ya hili tukio.
#NB Hata ukikaa kimya hauko salama
NOBODY IS SAFE!!
Hii imeniumiza zaidi, ni kama moyo wangu umepata ganzi kwa kitendo alichofanyiwa huyu mzee wetu wa Tanga!!
Bado Mtasimama Kwenye Majukwaa Na Kuwambia Wananchi Wasiogope Story Za Kutekwa Ni Drama Tu?
Bado Mtasema Sio Kweli Ni Watu Wanajiteka Tu Wenyewe?
Bado Mtatupa Mifano Na Majibu Mepesi Kuwa Kesi Mnazopokea Ni Za Watu Wamejificha Kwa Mahawara Tu Au Wanajiteka Kupata Ransom?
Au Bado Uchunguzi Unaendelea Si Eti Ee?
Mnaumiza Sana Mioyo Ya Watu!!
Mtatuteka Mtatutesa Mtatuua
“You Can Kill Me But You Wont Kill What Im Standing For”
Ununio Ndio KumbuKumbu Iliyobaki
Rest In Peace Uncle….. My Condolences To The Family💔
Sambaza upendo Mchango wako ni tumaini letu
Kwa pamoja, tunaweza kumrudisha uraiani mpendwa wetu @Eng_Matarra kwenye familia na jamii
Mchango wako ni muhimu sana changia ulichonacho Faini 7M
LIPA NAMBA MITANDAO YOTE 5554323 - MacFoodTz
M-PESA: 0769853711 - Devota Tweve
Rts
Askari Polisi muda huu yupo lindo kuhakikisha fedha benki zipo salama, kuhakikisha documents kwenye maofisi hazipotei! Ulinzi wa familia yake nyumbani alipotoka upo juu ya Muumba wake, furaha ya Mkewe kitandani na baridi ama mvua lipo kwenye tumaini na Mapenzi ya dhati ndio pekee Mlinzi wa kweli kati yao.
Mwanajeshi yupo nchini Kongo muda huu, wengine wapo Somalia wakipambana na missions mbali mbali, wengine wapo mipakani mwa nchi wakiweka rehani uhai wao kwa ajili ya Watanzania wote, hii sio ajira bali ni wito na uzalendo!
Mwanajeshi wakati huu anaitazama silaha yake kama Mkewe na risasi kama maisha yake, hana muda wa Baby umekula bali milio ya risasi, moshi na baruti! Hajui atarudi lini nyumbani, atarudi hai ama amekufa, ila anachofahamu ni kuwa ikitokea hayupo basi mwili utarejea nyumbani na bendera ya Tanzania.
Askari wa Usalama barabarani wakati huu anapambana kuhakikisha magari yanapita salama wakati home sio safi, simu inaita mboga hakuna ila amechagua kuhakikisha V8, Range mpaka Daladala zinawahi maskani mwao, shida zake sio kikwazo cha kufeli kazi yake! Mvua kwake imekuwa mapenzi na jua kwake ndio mahaba.
Wapi Wanangu wa SUMA JKT, wana tumaini kubwa Wanangu! Hawanaga shida ila hawapendi dharau, muda huu kwenye usiku wa matumaini wanalinda wazito na nyadhfa zao ambao wakifika kwenye maamuzi wanawasahau, amani juu yenu Wanangu! Wapi Askari MAGEREZA ni ulinzi kwa Wafungwa bila pingu na amani inatawala, asanteni sana.
Wanangu Makachero, Watalaam wa hizi kazi wa kuitwa USALAMA! Muda wowote kazini, wamekula kiapo kwa ajili ya Tanzania, hawana ndugu zaidi ya bendera yenye rangi nne, kuna wakati wanaweka rehani maisha yao kwa ajili ya usalama wa nchi, wapo waliokubali kuwa vyote kwa ajili ya vyote ili wapate taarifa zote, hakuna mshahara unaotosha na kamari ya uhai, ila kuna uzalendo wa kutosha kuweka kwenye uhai, respect Wanangu.
Heshima kwenu Ndugu zetu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama🫡! Unaweza kuwa usiku ila kwenu ni mchana, inaweza kuwa shwari machoni ila moyoni mnajua nini kinaendelea, hakuna mshahara wala posho ya kutosha bali Uzalendo wenu wa kweli kwa ajili ya Jamhuri.
VISIT MOROGORO🇹🇿
Yule Mwanamke wa ndoto zako kwa Jamaa mwingine ni kiburudisho cha nafsi yake ni simu moja maelekezo, yule Mwanaume unayekula nae vumbi leo kesho atakula bata Fivestars na Wanawake wa ndoto zake, ile gari ya ndoto zako kwa mwingine ni usafiri wa watoto shule.
Yule Mwanamke wako wa ndoa alikubali kwako baada ya kuumizwa na Kipenzi cha maisha yake, yule Mwanaume aliyekuoa huenda alikuwa anamkomoa Ex wake, wale wanaokupigia makofi wakati unashinda wapo kwa Mganga wa Kienyeji wanasema mikono inawauma wanataka kukuona chini.
I wish they would have been careful with what they wish for! Mwanamke wanayemtazama kama role Model mtandaoni kila trip Dubai mara New car, yupo hotel amekaa anasubiri wenye chapaa wampelekee moto aote kwakuwa anajisikia baridi, mwili wake una majeraha mengi japo picha zake nzuri machoni mwa wengi.
Nini maana ya maisha? Ni kuishi leo kwakuwa kesho hajapewa ahadi mtu yoyote, Mungu atubariki Wana Wa Hawa, uzao wa Adam! Fahamu mmekutana ukubwani na malezi kutoka familia tofauti, penda sana ila usiamini sana, wanapokuja wakaribishe sebuleni sio chumbani, past paper za Watu wema ndio zimejaa machozi mengi na matokeo ya Wanafki yana alama A.
NDIMI MKULIMA WA ULANGA NA KILOMBERO HUKO MOROGORO.
JANUARI 11, 2024! SHEKILANGO, DAR ES SALAAM.
VISIT MOROGORO🇹🇿
Habari!
Mtu yeyote ambaye anamfahamu huyu mwanamke afike ofisi ya kata ya Kinyerezi, Ilala. Mwanamke huyu amefika tangu Jumamosi na amegoma kula au kunywa chochote na hazungumzi kitu chochote, yupo kimya. Tafadhali sambaza ujumbe ufike mbali.