"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako"
Ayubu 22:21-22
Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako,
Usiondoke mara mahali pako ulipo;
Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.
#ElimikaWikiendi
Si ndio ile siku amechagua Bwana kwa ajili ya hawa Vijana wake wa Kipaimara.
Maisha yanabadilika sana darasa la Kipaimara tulianza tukiwa na umri wa miaka 15(ff) nakuendelea, leo wanaanza wakiwa na miaka 11ff.
Yote juu ya yote Mungu anatukuzwa ndani ya yote.
Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
~Waefeso 5 :25-26
Umecheleweshwa, umekatishwa tamaa, umekataliwa, umenyimwa fursa lakini kamwe usiache kuamini na usipoteze Matumaini. Hata katika kipindi cha kusubiri, MUNGU anaendelea kufanya kazi. Kile ambacho MUNGU ameahidi, hakika atakitimiza. Furaha yako iko karibu kuliko unavyofikiri.
Mwangaza Wa Siku. ⛅
Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.
‘Isaya 54:15 SUV’
Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Warumi 15 :13