Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2025 kabla ya kuzindua Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Viongozi pamoja na Wananchi mbalimbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2025.
Just arrived in Accra, Ghana 🇬🇭 ahead of the Africa Health Sovereignty Summit.
Appreciate the warm welcome. Looking forward to discussions on reimagining global health governance in face of challenging financial landscape.
More than ever we need strong investment & leadership.
Tulipohamisha Stendi ya Mabasi Ubungo kuipeleka Mbezi Luis, Dar es Salaam kulikuwa na hofu kwa wananchi kuwa watapoteza fursa za kiuchumi. Ninafarijika kuwa leo nimezindua Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) katika eneo ilipokuwepo stendi hiyo, kituo ambacho kinatoa fursa nyingi zaidi, hasa ajira, kuliko zilizokuwepo awali.
Mradi huu wa kimkakati utaimarisha na kukuza biashara na nchi jirani kwa kuwaunganisha wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa bidhaa kutoka ndani na nje ya nchi. Pia, utapunguza gharama za usafirishaji, utaongeza mapato ya serikali na akiba ya fedha za kigeni, utatoa ajira kwa wananchi na ni sehemu ya jitihada za kufanikisha ndoto ya soko la pamoja Afrika.
Nimeona wananchi wamejitokeza kwa wingi kukodi maduka kwenye eneo hili. Hongereni sana. Hata hivyo, nimewatoe hofu kuwa, kituo hiki siyo mshindani wa Soko la Kariakoo, bali ni sehemu ya wafanyabiashara kujifunza, hasa matumizi ya teknolojia katika kuongeza thamani ya bidhaa na kufanya biashara.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshinda kura za maoni za Ubunge wa Arusha Mjini kwa kupata kura 9,056 sawa na asilimia 97.63 ya kura zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo leo August 04,2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema jumla ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo ni 10,186 na waliopiga kura ni 9,276 (91%) ambapo kura zilizoharibika ni 11 na kura halali zilizopigwa ni 9, 265.
Paul Makonda amepata 9,056 (97.63%), Mustafa 83, Gonga 46 , Ali Babu 28, Aminata 26, Mgweno 16 na Kishumbua 10.
#MillardAyoUPDATES
Kazi ya kuifanya nchi yetu kuwa kitovu cha biashara, usafirishaji na uzalishaji wa bidhaa, inahitaji uwekezaji na miundombinu bora. Kazi hiyo tunaendelea kuifanya kwa weledi ambapo, leo mkoani Pwani nimezindua Bandari Kavu ya Kwala, usafirishaji wa mizigo kwa SGR kutoka Kwala kwenda Dodoma na kuweka jiwe la msingi katika Kongani ya Viwanda Kwala. Maendeleo haya ni sehemu ya kazi ya ujenzi wa sura mpya ya nchi yetu.
Kujenga tu haitoshi, ni lazima tunufaike na ujenzi huo. Hivyo, nimeelekeza ndani ya siku 4 zijazo kwa maana ya Agosti 4, 2025, huduma zote za kibandari ziwe zimehamishiwa kituo cha Kwala. Aidha, Wizara ya Uchukuzi ihakikishe usafirishaji mizigo unafanyika kibiashara, na pia waalike sekta binafsi itumie miundombinu ya reli ili kuongeza tija. Kwa upande wa kongani ya viwanda, nimeielekeza mamlaka ya uwekezaji kuvutia wawekezaji zaidi na wahakikishe hawakwamishwi, lakini pia wazingatie ubora wa bidhaa zinazozalishwa.
Wananchi hatuna budi kuchangamkia fursa zinazotokana na miradi hii, pamoja na mingine tunayotekeleza maeneo mbalimbali nchini ili iendelee kuleta utofauti wa kimaisha. Matokeo haya mazuri ni yetu sote kwani ni matunda ya jitihada za pamoja kama taifa.
Tanzania imefanikiwa kufanikisha ukuaji mkubwa katika sekta ya utalii wa ndani kati ya mwaka 2021 na 2024, ikivunja rekodi za awali. Mafanikio haya yanatokana na juhudi thabiti na uongozi makini wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni mbalimbali za kimkakati.
Moja ya juhudi kubwa za Mheshimiwa Rais ni uzinduzi wa filamu maarufu ya Royal Tour mwaka 2022, ambayo ilionyesha uzuri wa vivutio vya asili na kiutamaduni vya Tanzania kwa ulimwengu. Filamu hiyo ilifanikiwa si tu kuvutia watalii wa kimataifa, bali pia kuhamasisha Watanzania wengi kutembelea vivutio vyao vya ndani.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH #MSLAC
Tanzania imefanikiwa kufanikisha ukuaji mkubwa katika sekta ya utalii wa ndani kati ya mwaka 2021 na 2024, ikivunja rekodi za awali. Mafanikio haya yanatokana na juhudi thabiti na uongozi makini wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni mbalimbali za kimkakati.
Moja ya juhudi kubwa za Mheshimiwa Rais ni uzinduzi wa filamu maarufu ya Royal Tour mwaka 2022, ambayo ilionyesha uzuri wa vivutio vya asili na kiutamaduni vya Tanzania kwa ulimwengu. Filamu hiyo ilifanikiwa si tu kuvutia watalii wa kimataifa, bali pia kuhamasisha Watanzania wengi kutembelea vivutio vyao vya ndani.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH
Tanzania Yapiga Hatua Kubwa Katika Sekta ya Utalii (2021-2024)
Tanzania imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika sekta ya utalii kati ya mwaka 2021 na 2024, ikiweka rekodi za kipekee katika ukuaji wa utalii wa ndani na kimataifa. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii, utalii wa ndani umeongezeka kwa asilimia 307.9%, huku utalii wa kimataifa ukiongezeka kwa asilimia 132.1% ndani ya kipindi hicho.
Ukuaji huu wa kasi umetokana na juhudi za makusudi za serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kupitia kampeni kama Royal Tour, Tanzania imefanikiwa kuvutia watalii wa kimataifa huku ikiimarisha ari ya Watanzania kutembelea vivutio vya ndani.
Serikali pia imewekeza katika miundombinu muhimu ya utalii, kuboresha barabara, viwanja vya ndege, na huduma za malazi. Kampeni za kuhamasisha utalii zimeimarishwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, hatua iliyochangia kuongeza mwamko wa wananchi na wageni kuhusu vivutio vya kipekee vya Tanzania.
Matokeo ya ukuaji huu si tu kuimarisha mapato ya taifa kupitia sekta ya utalii, bali pia yamechangia kuongeza ajira na maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi. Tanzania sasa inajitokeza kama mfano wa mafanikio barani Afrika katika kukuza sekta ya utalii kwa njia endelevu.
Mafanikio haya ni ushahidi wa dhamira thabiti ya serikali ya awamu ya sita katika kutumia sekta ya utalii kama chombo cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH
Tanzania Yafanikisha na Kuvuka Malengo Katika Sekta ya Utalii (2021-2024)
Sekta ya utalii nchini Tanzania imefikia na hata kuvuka malengo yaliyowekwa kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024, hatua inayodhihirisha mafanikio makubwa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kupitia juhudi za kimkakati, ikiwemo uzinduzi wa filamu ya Royal Tour, uwekezaji katika miundombinu ya kitalii, na kampeni za uhamasishaji wa utalii wa ndani na kimataifa, Tanzania imefanikiwa kufanikisha ukuaji wa sekta hii kwa viwango vya kihistoria.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii, utalii wa ndani umeongezeka kwa asilimia 307.9%, huku utalii wa kimataifa ukikua kwa asilimia 132.1% ndani ya miaka minne. Ukuaji huu umepita matarajio, na sekta ya utalii imekuwa moja ya vyanzo vikuu vya mapato ya taifa, ikichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Mafanikio haya yameongeza nafasi za ajira, kuimarisha biashara zinazohusiana na utalii, na kuhamasisha Watanzania kufurahia utajiri wa asili na utamaduni wa nchi yao. Tanzania sasa inajivunia nafasi yake kama kiongozi wa utalii barani Afrika na mfano wa jinsi juhudi thabiti za serikali zinavyoweza kuleta mabadiliko makubwa.
#Sisinitanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya #kaziiendelee #kazinaututunasongambele #katibanasheria #mslac #SSH
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), zasaini mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa Uhifadhi wa Maeneo Oevu na Bioanuwai katika Kidakio cha Katuma, mkoani Katavi.