HIGHLIGHTS ๐น
Simba SC scored twice in 90 minutes against Al Masry SC forcing the game into penalties and securing their spot in the semi-finals. ๐
#TotalEnergiesCAFCC | @Football2Gether
Hongera kwa Klabu ya Simba kwa kufuzu kuingia Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Endeleeni kufanya kazi kuipa nchi yetu burudani na kuipeperusha bendera yetu kimataifa.
Ninawatakia kila la kheri.
USIMKATIE MUNGU TAMAA.
Katika magumu yoyote na changamoto zozote unazopitia usimkatie Mungu tamaa.
Hata katika dakika za mwisho, pale ambapo hakuna dalili ya msaada wake, bado usimkatie Mungu tamaa.
Abraham alifika miaka 100, na Sara miaka 90, ilikuwa ni rahisi kukata tamaa๐๐พ
Omba Sala ya BABA YETU ULIYE MBINGUNI, kila siku katika ofisi yako. Ina maana na italeta mabadiliko makubwa.
Unaweza kuigawa sala ya BWANA kwa siku saba za wiki, kama ifuatavyo;
1. Baba Yetu uliye mbinguni; mahusiano ya kibaba, familia, baba na wanae.
2. Jina lako litukuzwe; palipo na jina la Yesu na Yesu yupo hapo. Jina la Yesu lijulikane na lipate heshima mahali alipo.
3. Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama yanavyotimizwa huko mbinguni; Kufanya mapenzi ya Mungu hapa duniani wakati ni Ufalme mwingine unatawala ni kazi kubwa, lazima Ufalme wa Mungu na mfumo wake uje ili tuweze kutimiza Mapenzi yake.
4. Utupe leo riziki zetu; usitusahau ututunze, utulishe na kutupa tumaini wewe kila siku. Biashara, akiba, mshahara usituondolee utegemezi wetu kwa Mungu
5. Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea; Kutengeneza mahusiano kati ya mtu na mtu ofisini. Kipimo chako cha kusamehewa kinatokana na kipimo chako cha kusamehe.
6. Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu; Shetani yupo lakini hayupo kwenye agenda kuu.
7. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu na hata milele; Kwa kuwa Ufalme nguvu na mamlaka ndani ya hii sekta ni wako ee Mungu. Amen.
~Mwl Mwakasege.
Tangu tumboni kwa mama yako upinzani juu ya kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako unaanza. Hautaisha hadi unakufa.
Na ukisimama kwenye haki uwe umeokoka au hujaokoka jua umesimama upande wa Mungu na utakutana na vita za maadui wa Haki.
~Mwl Mwakasege.