#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 14
Anaendelea Mhe. Lissu
Lissu ameulizwa je utakuwa na mashahidi wangapi?
Mashahidi wangu watakuwa kama ifuatavyo
1. Samia Suluhu Hassan atakuwa ni shahidi wangu wa kwanza
Hakimu anasema anasema kuna taarifa inasambazwa muda huu, anasema kuna watu wanasambaza taarifa za hii kesi.😂
Lissu anednelea na kutaja mashahidi wake.
1. Samia suluhu Hasaan apelekwe summons.
2. Philip Isdory Mpango ni msaidizi wa serikali aje atoe ushaidi nilivyowatisha.
3. Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu nimesmtishia serikali aje atoe ushahidi
Hakimu anasema kwa vile sheria hailazimishi kukulazimisha utaje mashahidi wako utaomba Kibali cha mahakama kuu mimi siwezi kuwaandika hao mashahidi wako.
Hao mashahidi unaowataja utawaomba mahakama kuu mimi siwezi kuwaandika hapa.
Hakimu amekataa mashahidi wa Lissu anasema akawaombe mahakama kuu yeye ni mjanja pia hawezi kuingia huo mkenge.
Hakimu anasema hii safari haikuwa ndogo ilikuwa ndefu kwelikweli. Haisikilizi shauri wala kutoa maamuzi.
Hivyo basi mahakama haikuwa inasikiliza shauri kabisa.
Kwa mujibu wa kifungu cha 263 ninakupeleka mahakama kuu kwa tarehe ambayo itakuwa imepangwa kwa tarehe ambayo itasemwa na msajili wa mahakama kuu.
Kwa leo tumehitimisha hapa so tukutane Mahakama Kuu.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 13
Anaendelea Mhe. Lissu
Hiyo sheria inayotumika kuficha mashahidi haijawahi kuwa kwenye website ya Bunge ni sheria ambayo haijulikani kabisa.
Huyu Katuga anasimama anaongea takataka kwamba nisiongee kuhusu mashahidi kufichwa kwasababu sheria yenyewe haiko kokote.
Sheria inasema chochote kinachokuwa published lazima nakala mbili ziwepo maktaba kuuu hii sheria yao haipo kabisa.
Matumizi mabaya ya hicho kifungu iko hivi watu 11 nakaa nao wamehukumiwa kifo hawajawahi kuona shahidi hata mmoja na kwenye hiyo kesi aliendesha Latifa Mansoor, Jaji alimuuliza Shah umetoa ushahidi mara ngapi kwenue kesi hii anasema nimetoa mara 5.
Kama hii ndio haki inabidi tutafute tafsiri nyingine ya neno haki.
Utaratibu huu wa haki gizani unakiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara nyingi sana zinaeleza mambo ya haki hizi.
Sheria hii ya kulinda mashahidi ni mashahidi wa amshitaka na sio upande wa utetezi.
Hakimu anasema ikifika saa 11 na nusu jioni hii utatakiwa kusimama ili tuendeleee na shughuli nyingine.
Lissu anasema sitasimama kwasababu nakubaliana na wewe nitasimama kwasavabu umesema nisimame.
Na ninaomba uandike kuwa ulinisimaisha na sio niliacha kuzungumza kwa kuwa nilimaliza.
Nitasimama na nikifika huko mahakama kuu nitawauliza kama ulikuwa sahihi kuniambia nisimame kuendeleee.
Kwahiyo nitaacha kuzungumza kwasababu umenikatisha wakati bado niko na yakusema.
Mahakama kuu itaniambia ambayo sijasema hapa Kisutu nitayasema wapi? Watanielekeza huko.
Mashahidi nitakaokumbana nao wanakuja gizani lakini wakwangu waje hadharani. Hii haiwezi kuwa haki kabisa kisheria.
Na sasa saa 11 na nusu imefika kwahiyo muda wowote atakatishwa kuendelea na submission yake.
Wanajaza magereza watu wa kunyongwa kwa mashahidi wa gizani. Kama Segerea wako 11, je Isanga Dodoma, Maweni Tanga je wako wangapi?
Mheshimiwa anasema muda unatosha dakika zimeisha
Part 14 itaendelea post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 12,
Anaendelea Mhe. Lissu
Hakuna aliyesema kuwa nilichapisha video, nilisambaza video. Hakuna aliyesema hayo. Kuna shahidi alieleza nilivyokamatwa
Nilikamtwa kule Ruvuma kwa kupigwa mabomu na sio nguvu kiasi kama mashahidi mapolisi walivyokuw wanasema kwenye maelezo yao hapa.
Hakuna waliponiambia kosa langu, walinipiga mabomu na watu walipigwa. Nilipelekwa kwa RPC Ruvuma Michael Chirya ule usiku akaniambia unapekekwa Dar es salaam usiku huu huu.
Nilimwambia kuwa anipe simu niongee na ndugu zangu na kuwapigia Mzee Alute na Dada yangu anileteee Chakula. Akaniletea Chakula ni nikatumia simu ya RPC. Nikawekwa Central shimoni na kujua makosa yangu niliambiwa hapa Dar es salaam kuwa makosa yangu ni uhaini.
Kukamatwa kinyume cha sheria na mashitaka ndio haya nimesema.
Hayo maneno yanayodaiwa kuwa nilisema. Sitaki tusumbuane huko mbele ya safari.
Ninachokisema hapa ni kwamba NI KWELI NILISEMA MANENO HAYO.
Sijawahi kukataa maneno yangu ni maneno ambayo nimeyasema kwenye mikutano ya hadhara mkoa wa Mbeya, mkoa wa Iringa, Songwe, Njombe, Rukwa na Mtwara.
Msimamo wangu kuhusu kuzuia uchaguzi haujawahi kuwa yakificho.
Swala je ni uhaini?
Wajibu hilo swali la msingi?
Msihangaike kwasababu sitabishia hao mashahidi wa video hao sina shida nao.
Mashitaka haya ni mashitaka ya kisiasa hilo linapaswa kueleweka kuwa mshitaka haya ni mashitaka ya kisiasa ili tumalize uchaguzi halafu tumuache.
The political nature of this charge is like this.
Historia ya miaka 22 ya makesi ya uongo dhidi yangu ni ushahidi mwingine kuwa makesi haya ni ya uongo.
Tangu nimekamatwa nimetendewaje huo pia ni ushaidi wa kuwa ni mashitaka ya kisiasa.
Nimetendewa mambo ya hovyo tangu siku ya kwanza kama mtu mwenye hatia ninavyokuwa treated ni kama nina hatia ya mauaji.
Nakaa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa, nachanganywa na wafungwa wa kifo. Why? Kwanini hilo?
Hata hao waliohukumiwa kifo wanaruhusiwa hata kufanya ibada ya Mungu, nimenyimwa kufanya ibada.
Hadi nilipolalamika hapa ndo wakamleta Father George akaja chumbani kunifanyia ibada na amekuja mara mbili tu.
Wafungwa wenzangu wote ambao hawajahukumiwa kifo wanafanya ibada.
Mimi mfungwa ninaekaa na waliofungwa kifo siruhusiwi kufanya ibada. Kwanini wanafanya hivi sasa?
Wafungwa waliohukumiwa kifo wanalindwa na maaskari wawili 24hrs. Tangu ijumaa kuu nilipokamatwa nalindwa na Bwana Jela wako pembeni wawili. Mahali pekee ambako hawanisindikizi ni chooni.
Why tusiseme hii ni political persecution ni nini kingine?
Hii ni kesi za kubambikiza kwa maneno ya Rais wa Tanzania ni kesi zenye lengo la kuumiza watu hii ni kesi mojawapo ya kubambikiza.
Tarehe 18/05 Rais Samia alifunga mafunzo ya maafisa wa polisi kurasini alisema maneno yafuatayo kuhusu kesi za kubambikiza.
Katuga anasema asimseme Rais Samia haya hayahusiki hapa.
Lissu anasema nina kurasa 140 na leo hii ngoma haiishi.
Hakimu anasema ni wajibu wa ku control hizi proceedings.
Lissu anasema mheshimiwa nina kurasa 140 na sasa ni page 70 kwahiyo wewe vumilia tu nisome.
Wajibu wako wewe ni kuandika na sio kunielekeza nini chakufanya.
Lissu anasema mheshimiwa wenzangu wametumia siku zaidi ya siku 100 kwanini mimi siku moja inakuumiza?
Hakimu anasema hii ni committal Court hayo mengine nenda nayo high court.
LISSU anasema mimi naongea tu wewe ukiona nakuchosha utanisimamisha utasema niache kuongea.
Sasa naendelea.
Sasa Rais anasema niongee na Mapolisi mmekuwa na mlolongo mkubwa wa kubambikiwa kesi. Nanyi Polisi jikagueni kama kuna kesi za aina hii mzifute.
Anayefungua kesi sio mapolisi ni DPP hawa ndio wanapaswa kuzifuta kesi kama hizi.
Hii amri ya kuficha mashahidi ya kutengeneza star chamber Court inatokana na kifungu cha 194 cha CPA.
Part 13 itaendelea Post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 11,
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa naomba nizungumzie kesi yenyewe sasa.
Kwa kuanzia baada ya kusikiliza information ilivyosomwa yote baada ya kusoma haya maelezo yote.
Cha kwanza ninachoweza kusema ni kwamba
Hapa hakuna uhaini.
Pili hapa hakuna kosa lolote la jinai.
Hakuna uhaini na hakuna kosa lolote la jinai.
Mashitaka yanasema nimefanya kosa la uhaini.
Kifungu cha 39(2) (d) cha penal code kinatengeneza kosa la aina gani?
Ni kweli mimi ni raia wa Tanzania lakini nia ya kufanya uhaini ni kuzuia uchaguzi, kuvuruga uchaguzi, imesemwa imerudiwa imerudiwa.
Je kuzuia uchaguzi ni kosa la uhaini? Au wanasema wakiyatoa wapi?
Kifungu cha 39 kinasemaa uhaini ni kutishia Bunge, Serikali na Bunge.
Kuzuia Uchaguzi sio uhaini.
Kwa sheria za Tanzania kuhamasisha kuzuia Uchaguzi sio uhaini labda wawe na sheria zao binafsi huko sirini.
Sheria ya Uchaguzi imetengeneza makosa ya Uchaguzi imeandikwa kiswahili.
Hakuna kosa linaloitwa kuzuia uchaguzi.
Hakuna kosa la kuvuruga uchaguzi.
Sio jinai kwa mujibu wa sheria.
Nashangaaa inakuwaje uhaini kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi?
Hebu nyie mawakili wa serikali mseme inakuwaje uhaini?
Mheshimiwa utakumbuka tangu mapema kabisa kwamba hii kesi sio kesi ya kwanza ya uhaini Tanzania ni kesi ya nne.
Kwahiyo tunayo Precedent ya Mahakama ya afrika mashariki na mahakama ya rufani ya Tanzania zote zinaeleza kuhusu mambo ya uhaini.
Tunamuomgozo wa kesi ya uhaini inavotakiwa kuwa na Muongozo wa Mahakama ya rufani on how to frame a charge of treason.
Mwongozo unasema pawe na statement of the offence, particulars and overt act hiyo nia iwe na tendo la wazi.
It must be pleaded, Utekelezaji lazima uwepo na uelekezwe.
Wamekoroga mashitaka hayaeleweki, haijulikani overt act ni ipi? Walichokifanya hapa ni mkorogo maana hakuna charge hapa.
Jambo lingine muhimu kuhusu hii information ni kwamba maelezo Mheshimiwa Lissu alisema alisema alisema.
Swali ni kwamba Je maneno peke yake yanatengeneza uhaini? Maneno matupu yanatengeneza uhaini?
Kwa mujibu wa mahakama ya rufani Khatibu Gandi ilisema maneno matupu hayatengenezi uhaini isipokuwa yanatengeneza kosa la uhaini.
Kuzuia uchaguzi sio kosa la uhaini na sio kosa la jinai.
Hakimu anasema mimi pia leo nitapata relief wewe kuondoka kwenda mahakama kuu kwahiyo naomba naomba ujielekeze pia kwako na wewe utunze muda.
Mhehsimiwa naomba niendeleee nisipotezewe muda tafadhali sana.
Je Tundu Lissu peke yake anatosha kutenda kosa la uhaini?
Hili kosa nimeshtakiwa peke yangu na hakuna mtu mwingine kabisa.
Kwanza sheria inataka nifanye publication kwa watu wengine kuhusu huo uhaini na mipango yake. Sasa mimi hakuna mahali nimefanya publication. Wanasema JAMBO TV ndio walichapisha hayo maneno.
Hakuna aliyesema kuwa Tundu Lissu amemtishia Rais, Bunge au mahakama? Hakuna hata mmoja amesema hivyo. Wote wamesema tutazuia uchaguzi tutafanya vurugu.
Pia maelezo ya mashahidi hakuna aliyesema zaidi ya maneno niliyosema nilitenda kitendo kingine chochote. Hakuna aliyesema hata mmoja.
Part 12, itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 10
Anaendelea Tundu Lissu
Nilishiriki pia katika Bunge maalumu la Katiba la mwaka 2014 na 2015 nikawa mbunge pia.
Nilitumikia nafasi hiyo sikumalizia Tarehe 07/09/2017 nilishambuliwa kwa risasi nyingi na kupelekwa nje kwa matibabu nikafutiwa ubunge wangu na Ndugai marehemu mwenyezi Mungu aiweke roho yake inapostahili.
Pia 2017 nilikuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika na sikumalizia nafasi hiyo kwasababu nilizosema.
Professionally nilipata heshima kuwa Rais wao kwahiyo tunapozungumza kuhusu treason tunauzngunza kuhsu mtu wa aina hiyo.
Mimi nimekuwa mwanaharakati katika maisha yangu yote.
Mwaka 2016 nilipata tuzo ya chuo kikuu huko Marekani (BrichPort University) Maelezo ya tuzo hiyo inasema TUNDU LISSU ni mtetezi wa haki za binadamu na mazingira Tanzania na Afrika. Nilipewa hiyo tuzo.
Ni muhimu kusema mambo haya ilitumjue Tundu Lissu ni nani na yanamaanisha nini?
Yanamaanisha kwamba huyu mtu anbae amechaguliwa na wananchi,
Amepata heshima ya kuwatumikia wanataaluma wenzake,
Heshima ya kutambulika na taasisi za kimataifa.
Haya yote yanasema ukweli mmoja kuwa, MIMI NI MPIGANIA HAKI, DEMOKRASIA NI MTETEZI WA HAKI ndo maana nimetambuliwa hivi.
Mimi sio MHAINI,
Mimi sio mhalifu na sio yote hayo uliyoyasikia hapa.
My contribution recognised nationally na internationally.
Hii kesi ya uhaini ni kesi kweli au ni siasa tu?
Mambo hayo niliyosema yanakusaidia kujibu swali hilo hapo juu.
Lingine uelewe kwangu mimi ni mwendelezo wa mashitaka ambayo nimefunguliwa kwa zaidi ya miaka 23 nimefunguliwa mashitaka kwahiyo huu ni mwendelezo tu.
Kesi yangu ya kwanza katika Mahakama hii katika chumba hiki siku ya Christmas mwaka 2002 mbele ya hakimu Lugulu kwenye chumba hiki hiki kosa lilikuwa uchochezi.
Tulimkosoa Rais Mkapa kutokana na wachimbaji wa wadogowadogo 1996 nikapewa kesi ya Uchochezi nilikaa nayo kwa miaka 6 baada ya miaka 6 kesi hiyo ilifutwa bila maelezo.
Baada ya hapo miaka 10 ya kikwete nilishtakiwa mara tatu, mara moja Tarime, nilikoenda kupinga mauaji nikashitakiwa huko kesi ya criminal trespasses,
2012 nikafunguliwa kesi mbili Arusha mjini, kesi ya kwanza kupinga mauaji ya waandamanaji 2011 tukaenda kupinga nikafunguliwa kesi.
Kesi ya pili Arusha nilienda kupinga mkutano wa Chadema kupinga wanachadema kuuliwa arusha ikafutwa pia na kesi hiyo.
Tulivyoingia Tanzania ya Magufuli kwenye mwaka mmoja wa Magufuli 2016 hadi 2017 kwenye mahakama hii na kwenye chumba hiki nilishatakiwa kwa kesi sita nilikuwa nikipinga mambo ya Magufuli.
Nilipochaguliwa RAIS wa TLS nilitokea hapa Kisutu na kwenda kushinda uchaguzi wa TLS nilikamatwa na mapolisi mara nane.
Kesi zote hizo pia zilifutwa hizo kesi zilifutwa na hakuna aliyekuja kutoa ushahidi hata mmoja.
Ikaja ile habari ya risasi walitaka kuninyamazisha forever.
Tangu mwaka jana hadi leo nimeshakamatwa na Polisi mara 3 nilikamatwa Mbeya, August mwaka jana, mara ya pili 13/09 nikakamatwa pia kulikuwa na mauaji ya Mzee Kibao walikuja nyumbani kunikamata.
Anasimama Katuga anasema haya maelezo ya Lissu hayana umuhimu wowote, asiyaseme na ni kinyume na Sheria.
LISSU Anasema yeye sheria yuko nayo na anasoma Sheria.
Lissu anasema anachokisema wakili wa serikali ni non sense huwa sipendi kusema maneno haya lakini anapaswa kurudi shule huyu asome kifungu cha 53 cha sheria ya ushahidi kwaba good character is relevant to the case.
Hakimu anasema maelezo yote ajielekeze kwenye charge sheet
Lissu anasema mheshimiwa kazi yako wewe ni kuandika na mimi kazi yangu nitasema kama hutaki kuandika usiandike ila mimi nitasema. 🤣🤣🤣🤣
Wapendwa Leo mambo yangekuwa live vingekuwa ni vituko sana vinaendelea hapa ndan Hakimu kapanic, Mawakili wa Serikali wamepanic, Mhe. Lissu anawashona bila ganzi 😂😂😂😂😂
Part 11, itaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendele Mhe. Lissu
Kifungu cha 263(3)(5) kinanipa haki ya kusema na nitakayosema yote uyaandike na uyasome kwangu ni muhimu kwasababu kwa kesi kama hii kubwa kuliko zote Tanzania.
Ambayo adhabu yake ni adhabu ya kifo kwa kesi ya aina hii,
Anasimama Katuga hapa anasema Mhehsimiwa kifungu namna anavyokitafsiri ni tofauti na maana yake. Hapaswi kusema kila kitu, yeye aseme ni kweli au sio kweli?
Tundu Lissu anasema huyu Wakili wa serikali tumemvumilia sana kasema yakwake. Sasa muda huu anisubiri na mimi niseme yakwangu. Anivumilie na awe mtulivu kabisa.
Hakimu anasema ntuhumiwa unapaswa kwenda direct. Lissu anasema hapana siwezi kwenda huko
Kwanza naomba niendelee na nipewe muda.
Jambo la kwanza nataka kusema kuhusu mimi. Masuala ya character ni muhimu sana kwasababu ni maswala relevant to the charge.
Jina langu ni TUNDU ANTIPHAS MUGH'AI LISSU. nimezaliwa Mahambe Ikungi Singida 20/01/1968. Nina miaka 57 ni mtoto wa Saba kati ya watoto 10.
Nilipata elimu ya msingi Mahambe.
Amesimama Katuga anasema mheshimiwa asiende kwa style hiyo asiseme mambo ya amesoma wapi?
Mheshimiwa anasema Lissu asome hati ya mashitaka
Amesoma yote.
Lissu anasema Mhehsimiwa Hakimu unapswa kulinda haki yangu ya kusema. Inakuwaje hawa wameongea yote kuanzia asubuhi hadi sasa hivi wamekaa siku zaidi ya 100 wanaandaaa haya makaratasi. Na wewe ulinde hiyo haki yangu sitakubali kabisa kwenye jambo hilo.
Nimesoma Ilboru, Galanos, nilienda kwa mujibu wa sheria JKT 1989/1990. Baaada ya JKT nilitakiwa kwenda kusoma chuo kikuu 1990 kutokana na mgomo wa wanafunzi kwahiyo nilifanya kazi shule ya sekondari Bondeni arusha.
1991 nilisoma kitivo cha sheria shahada ya kwanza pale UDSM.
Nilimaliza UDSM na kumaliza November 1994 na kuzawadiwa shahada ya sheria ya heshima. Honours degree. Mimi ndie niliyekuwa mwanafunzi bora wa sheria wa mwaka wa 3 pale UDSM.
Nilipograduate nilipata scholarship kwenda kusoma nje kutoka Serikali ya Wingereza, Mwaka 1995 hadi 1996 nilipata distinction na ndoto zangu nilikuwa nataka kurudi UDSM kufundisha sheria ilikuwa ni ndoto yangu siku zote.
Nilipata kazi LEAT ya Dar es salaam mwaka 1998 kama mtafiti wa masuala ya mazingira na haki za binadamu hadi mwaka 1999.
Nilipata kazi world resources institute (Taasisi ya Rasilimali za Dunia)
Nilifanya kazi WRI kwa miaka 3 na 2002 nilirudi Tanzania.
June 2003 nilipata uwakili wa mahakama kuu za Tanzania na chini yake. Nimekuwa Wakili wa nchi hii namba yangu ni 945.
Ni muhimu kuelewa maisha yangu ya ajira kwasababu yana uhusiano na kesi hii maana nimesikia wanasema kuhusu siasa zangu.
Katika maisha yangu yote nimekuwa mwanaharakati wa kisiasa. Na mwanahatakat wa haki za binadamu. Kwenye siasa mimi nilipiga kura kwa mara ya kwanza 1985 nikiwa kidato cha 5.
Kabla sijaenda chuo kikuu nilienda jeshini na majeshi yalikuwa ya CCM. Na mimi nikiwa jeshini nilikataa utaratibu wa majeshi kuwa ni mali ya CCM.
HAKIMU anauliza hiyo ni relevant Lissu anamjibu kuwa hiyo ni Character na ni muhimu sana urekodi.
Nayasema haya ili ujue mimi ni mtu gani yuko mbele yako. Nilianza harakati zangu jeshini sio tu huku mtaani.
Mwaka 1995 nikiwa mwanafunzi wingereza nilirudi nyumbani kuja kugombea ubunge singida kusini miaka ile. Nilikuwa mgombea ubunge kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na baadae nilirudi shule.
Naomba kusema kuhusu Chadema, nilijunga Chadema 2004 July na nilipojiunga niliteuliwa kuwa mkurugenzi wa sheria na haki za binadamu. Na kwasababu nilikuwa wakili uchaguzi wa 2005 nilikuwa wakili wa wagombea wote wa Chadema walioshitakiwa kwenye uchaguzi.
Kwahiyo kwenye haya masuala ya Uchaguzi nina historia ndefu sana.
2010 nilichaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya Chadema. Na nilikuwa mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.
Part 10, itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Nini maana ya kukinukisha?
Neno "kukinukisha" linatokana na kitenzi cha Kiswahili -kinukisha, ambacho asili yake ni kutoka neno "kunuka" (kuwa na harufu).
Kwa kawaida, kukinukisha humaanisha:
1. Kusababisha kitu kitoe harufu mbaya – mfano: Chakula kilichooza kikinukisha nyumba nzima.
2. Kwa maana ya kifigurative, hutumika pia kueleza jambo baya au la fedheha ambalo “limefichuka” na kufanya watu walione kama aibu au skandali – mfano: Kashfa ya ufisadi ilikinukisha serikalini.
Kwa hivyo, matumizi yake yanaweza kuwa ya moja kwa moja (harufu mbaya) au ya kifumbo (fedheha, aibu, au jambo la kuchukiza).
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 6
ASP lugano ndio shahidi anayefuata shahidi wa 20
Ni Askari Polisi Mbinga na Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Mbinga.
Anasema tarehe 08/04 nilipewa maelelezo ya kusimamia mikutano ya hadhara miwili ambayo angeifanya Mbinga.
Mkutano wa Soko kuu pale Mbinga uliokuwa unafanyika Mbinga jioni Saa 10:30 jioni mwenyekiti wa Chadema Taifa alifika na mkutano ukaendelea.
Saa 11:05 jioni nilipewa maelekezo kuwa anapaswa kukakamatwa kwa tuhuma za uhaini.
Afande alimfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi kwa vile aligoma ilitumika nguvu ya kawaida hadi kupelekwa Mbinga na saa moja na nusu usiku aliondoka kuelekea Songea kwa hatua zaidi ni hayo tu.
Shahidi anayefuata ni afisa wa polisi pia.
Anasema aliambiwa aende Mbinga kwenda kumchukua Lissu na kabla sijafika huko, tulirudia njiani baada ya kukutana nae anasafirishwa kuletwa Songea mjini nikiwa na askari wengine.
Niliambiwa nimsafirishe hadi Dar es salaam, Tulitumia land cruiser hadi Dar es salaam tuliondoka saa nne usiku na kufika saa nne asubuhi, nikiwa Mkuu wa msafara nilimkabidhi Tundu Lissu kwa Mafwele.
Anafuata ni Shaidi wa 22 Geoffrey Mtufyi, PF 1548
Nafanya ofisi ya upelelezi arusha, tulipokea taarifa za watu wanaohamasisha kufanya fujo na kupanga njama, tulipokea kutoka kwa msiri wetu na tuliwakamata vijana hao.
Anafuata Shahidi wa 23 ni Mhini Mahamba ni Askari, nafanya kazi Mkoa wa Dar es salaam.
Tarehe 08/04 nilipewa maelekezo kuungana na timu ya upelelezi kuungana na Timu kuchunguza kosa la uhaini. Nilitambulishwa na timu, tulikuwa na timu tatu katika kupeleleza suala hili.
Kama timu tuliona matamko haya ni kinyume cha sheria kwani sio kweli mapolisi wanaingiza kura feki, majaji ni Maccm na pia Rais aliagiza wapinzani kuenguliwa.
Upelelezi wa Mikoa ya Arusha, lindi na Dar es salaam ulionesha wananchi wameanza kujiandaa na maandalizi ya kufanya jinai hizo.
Baada ya kusoma majalada kutoka mikoa hiyo niligundua watuhumiwa hao walichochewa tu na Lissu kama kiongozi wao na nilitoa maelekezo kuwa watuhumiwa hao wahojiwe kama mashahidi.
Ushahidi uliokusanywa ni pamoja na picha mjongeo zilizokusanywa na tulipokamilisha jalada likafungwa.
Shahidi anayefuata ni Askari pia.
Anasema yeye ni ASP anafanya kazi ya ofisi ya ZCO na anafanya upelelezi.
ASP George alinipa maelekezo nifanye uchunguzi kuhusu makosa aliyofanya Lissu, nilifungua jalada mimi.
Niliandika majalada mawili ambayo ni uchochezi na nyingine ni hili la uhaini.
Nikakusanya vielelezo na kuvichukua kwa mtunza vielezo na kuvipeleka kwenye uchunguzi, viligongwa muhuri na tulifuata taratibu za kubadilishana hivyo vilelezo ni hayo tu.
Shaidi anayefuata ni Peter Lucas ni afisa uhamiaji Dar es salaam.
Majukumu yangu ni kutoa passport na hati ya kusafiria.
Nilipokea barua nikiwa ofisini kutoka mkuu wa upelelezi Dar es salaam kuomba kupewa taarifa kuhusu mtuhumiwa Tundu Lissu ambae kama kweli ni raia wa Tanzania au anao uraia wa Tanzania.
Tarehe 09/11/2005 alipewa passport ya Tanzania na ilikuwa inaisha 2015 na mwaka 2016 alipatiwa diplomatic passport ikaisha 2021.
Mwaka 2020 alipewa passport ya kawaida na matumizi yake ingeisha mwaka 2030 na mwaka 2022 alipatiwa passport nyingine baada ya ile ya kwanza kupotea. Kupitia taarifa hizo tumethibitisha kwamba Tundu Lissu ni raia wa Tanzania. Nikakusanya nyaraka hizo na kuwasilisha.
Shahidi anayefuata ni Askari polisi pia msaidizi wa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Arusha.
Nikiwa ofisini kwangu nilipokea taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna vijana wako Moromboo Arusha wanapanga kufanya fujo, nikatoa maeleezo wakakamatwe vijana hao na wakakamatwa.
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 5
Shahidi ASP Juma Batazali yeye ni shaidi wa 14.
Maelezo yake baada ya kuapa huko polisi songea anasema Mimi ni afisa wa polisi ni mrakibu wa polisi. Mkuu wa upelelezi Songea.
Mimi nilimuhoji P2 ambae alisema alikuwa bize na mapokezi ya vipngozi wa Chadema songea na tarehe 04/04 aliona video kwenye simu Mhe. Lissu akitoa maelezo kwanwanachama wa Chadema kuwa watazuia uchaguzi kwa kuhamsisha uasi.
Video hii ilimpa hamasa sana baada ya kumsikiliza Tundu Lissu, amemaliza ushaidi wake.
Anafuata Amani Michael ni Polisi. Shahidi wa 15 Polisi Ilomba ndio mahojiano yalifanyika.
Anasema Nilizaliwa same Kilimanjaro, Nilipangiwa polisi Mbeya na mwaka wa 7 nafanya doria mtandaoni.
Tarehe 04/04 nilipewa maelezo kuwa nifuatilie watu wanaofanya njama za kuandaa fujo kuzuia uchaguzi, nilienda kumkamata P3 baada ya kubaini kuwa anapanga kufanya uasi na vurugu.
Nilimuhoji na kuandika maelezo yake P3 ambae alikubali ni mfuasi wa CHADEMA. alishiriki Mkutano ulioomgozwa na Lissu pale Ruanda Nzovwe Mbeya.
Aliona YouTube pia Mwenyekiti wa CHADEMA Lissu akisema tutahamsisha uasi na kuzuia uchaguzi. Alisikia maneno hayo na alihamasika sana katika mpango huo wa kujiandaa kupiga mawe watu watakaoshiriki uchaguzi huo na baadae akakakamtwa na polisi.
Leo Tarehe 17 nimepewa maelekeoz ya kumuhoji kama shahidi.
Anafuata ASP masalanga ambae ni Shahidi wa 16.
Nafanya kazi Polisi Songea na nilitoa maelekezo ya kuwakamata watuhumiwa wanaopanga kufanya fujo na walikamatwa wote na kufunguliwa kesi za kufanya maandamano bila Kibali. Leo Tar. 25/04 nimeambiwa niwahoji watuhumiwa kama mashahidi
P4 ni mwanachama wa Chadema ambae anasema aliongea na Mwenyekiti wa Vijana Songea ambae anaitwa Chiza
Akamsajili kama mwanachama aliona video ya Lissu na alihamsika sana kuanza taratibu za kuzuia uchaguzi. Aliingizwa kwenye group la SIASA yetu ambalo lilikuwa linajadili mikakati ya kukinukisha.
Baadae tulipata taarifa mwenyekiti kuwa amekamatwa na polisi na baadae nilipatataarifa kutoka essau kuwa yapo maandamano ya amani na alinunua t-shirt ya elfu 20 ya no reforms.
Ndio alipokamatwa na polisi kwa mshitaka ya kufanya njama za kuandamana bila kibali, hayo ndio maelezo yangu.
Anakuja shahidi wa 17 ambae ni P1 huyu ni mwandishi wa habari, anaishi Sinza.
Anasema nimezaliwa Njombe na nimesoma maeneo tofauti tofauti
Nimesoma form 5 na 6 huko mbeya na 2024 niliajiriwa na JAMBO TV kama mpiga picha.
Siku ya Tarehe. 03/04 nilipewa majukumu na baadae nikaambiwa niende ofisi za Chadema kuna kikao huko. Nikawakuta wafanyakazi wenzangu pale ukumbi wa Chadema.
Nilikuta mkutano upo katikati na Lissu alikuwa amekwishaanza kuongea.
Tulikuwa na camera tatu na computer na vifaa vingine.
Nikiwa Dodoma mwenzangu alipigiwa simu kuwa amepigiwa na askari hivyo nikamsindikiza na tukaenda kutakuwa kutoa ushaidi wa ile video. Tukawa ikawa hivyo. Nimemaliza.
Anafuatia Insp. Mwaligau mkazi wa Pugu kinyerezi. Shaidi wa 17
Kazi yangu ni kutunza vielelezo mbalimbali vilivyokamatwa katika maeneo mbalimbali.
Shahidi anayefuata ni Msajili msaidizi wa vyama vya siasa.
Anasema Elimu yangu shada ya uzamili na nafasi hii niliteuliwa. Mnamo tarehe 03/04 kupitia simu yangu niliona Mwenyekiti wa Chadema Lissu akiongea kuhusu msimamo wa Chadema kuhusu uchaguzi
Alisema atahamasisha uasi na watakinukisha vibaya sana, Sisi ofisi ya msajili tulibaini maneno aliyosema Lissu yanakiuka sheria ya Vyama vya siasa kwani chama cha siasa hakipaswi kutumia maneno kama hayo.
Tarehe 04/04 tuliwaandikia Chadema kuwa wanakiuka sheria kuhusu matendo ya Mwenyekiti wao wa Chama.
Bila shaka huyu ni Sisty Nyahoza ndio shahidi anayesema haya.
Chadema walijibu barua ya msajili na katika majibu yao walieleza kuwa hawawezi kutoa maelezo yoyote kwasababu lipo polisi basi na sisi tukaliacha suala hilo.
ASP Lugano ndio shahidi anayefuata shahidi wa 20.
ASP lugano Gwasa ameapa na kutoa ushahidi
Part 6 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Retweete yako.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 2
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Tarehe 03/04 mtumiaji wa mtandao huo wa YouTube yaani akaunti ya JAMBO TV alichapisha maudhui yakiyojulikana TUNDU LISSU uso kwa uso na watia nia chadema.
Katika video hiyo Lissu alisema majaji ni maccm, mapolisi wanaiba kura na vibegi na uchaguzi wa 2024 Rais alitoa maeleekezo kuwa wapinzani wasiende kokote. Yaani walienguliwa na maccm.
Pia alisema mimi nataka kacheo na nyie hamtaki kacheo sasa tunaweza kushinda au kushiriki uchaguzi wa aina hii? Sas amsimamo wetu kama Chama ni No Reforms no Election tunasimamia hapo.
Nilipakua video hiyo kwenye ukurasa wa JAMBO TV na kuiwasilisha.
Maelezo ya shaidi wa tatu PF ... Insp. Andrew Churu nae maelezo yake yanasomwa.
Mimi natokea Dodoma nafanya kazi huko na maelezo haya nimeyatolea Dar es salaam. Niko polisi toka 2000 nafanya kazi ofisi ya DCI makao makuu Dodoma. Tar. 07/04 nilipigiwa simu na DCP kuwa yupo.mfanyakazi wa JAMBO TV yuko Dodoma akanitumia namba ya simu ili nimtafute.
Siku hiyo alikuja shahidi hiyo na camera yake na kutoa ushirikiano ambapo alinipa memory card ambayo ilikuwa na video ya Lissu. Alifungua camera na kunipa kidhibiti hicho na tukaaandikiana uthibitisho wa nyaraka hiyo.
Nilimuhoji kuhusu ufahamu wake wa tukio hilo alipoenda pale Makao makuu ya Chadema na yeye ametokea Jambo TV alirekodi kupitia camera hiyo. Anakiri kuwa walipandisha instgram na mitandao mingine. Na nilielekezwa kuwa nivipeleke Dar es salaam siku hiyo hiyo na kuleta Dar es salaam.
Nikakutana na afande George Dar es salaam kwa ajili ya kumkabidhi vifaa hivyo vyote kwa maandishi.
Shahidi wa 4 ASP Kaaya ni ushahidi unaofuata.
Samwel Elibariki Kaaya mimi ni mtaalamu wa picha ni Askari wa Jeshi la Polisi ninafanya kazi ya kupiga picha za mnato.
Nilipewa vifaa vya kuvifanyia uchunguzi ikiwemo adapter, flash disk, barua na vifaa vingine nikitakiwa kufanya uchunguzi wa video mbalimbali. Zilizokuwepo kwenye memory na flash disk. Nilitahijika kuthibitisha uhalisia wa video hizo kitaalamu. Maudhui yenyewe ni yale mapolisi kuiba kura na vibegi, majaji ni maccm na taarifa kama hizo.
Chanzo cha picha mjongeo hizo ni kipi na zimetoka wapi ndio kazi yangu niliyotakiwa kufanya.
Niliakgua vifaa vyangu kuona usalama wake, Vilikuwa salama na imara kufanya kazi hiyo.
Baada ya uchunguzi wa kitaalamu niligundua picha mjongeo nilizopewa niligundua ni halisi kabisa na nikaandaa taarifa na kusaini taarifa hiyo.
Shahidi wa tano anaitwa " P"huyu ni mzaliwa wa Dar na mwaka umefichwa na ni mtoto wa kwanza. Nilisoma shule .... nilijiunga chuo cha kilimo na niliishia elimu ya certificate. Na 2020 nilijiunga chuo cha DSJ 2021 hadi 2023 na kujiunga na JAMBO TV kama mpiga picha kazi ninayoifanya hadi leo.
Nilihudhuria mkutano wa Chadema. Uliofanyika makao makuu chadema. Ulihudhuriwa na watia nia na mh. Lissu alihutubia. Tulienda wafanyakazi watano wa jambo na tukaenda. Niliona tangazo kupitia mkurugenzi wetu.
Tulikuwepo waaandishi wengi ikiwemo wa Azam na vyombo vingine tulirusha live tukio lile sisi jambo TV.
Masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni kuhusu suala la Uchaguzi na mambo yaliyokuwa yakiongelewa ni uchaguzi na no reforms: No election na kikubwa ni matatizo wanayokutana nayo kama Chama katika chaguzi zao. Mambo hayo yapo kwenye memory kama nilivyokukabidhi yapo humo. Kikao hicho kilifanyika masaa mawili hadi matatu. Na baadae waandishi tuliondoka na wenzetu tukawaachia
Maelezo ya shahidi wa 6 anaitwa P2 nae anaanza baada ya yule aliyepita.
Mimi ni mkazi wa matalawe ni mkazi wa matalawe. Sijao sina mtoto ni mfuasi wa CHADEMA toka 2021 na ni mshabiki wa tundu Lissu nililjpia kadi ila sijapata kadiyangu. Nimekuwa namuunga mkono Lissu na kwa songea mwenyekiti wetu wa BAVICHA ndio kiongozi wetu ambae almaarufu kama mwamba wa Kigoma.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Retweet yako
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 1
Mahakama imeamuru kuwa committal itasomwa yote bila kurushwa live.
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea kusoma kwa sasa.
Maajabu yaliyotokea ni kwamba mawakili wa serikali waliomba maelezo ya mashahidi wa siri yasirushwe live.
Lakini cha ajbu mahakama imesema maelezo ya mashahidi wote yafichwe na yasiwe live.
Kifupi mahakama imetoa uamuzi ambao hata serikali haijaomba. Imefunga kila kitu na kesi kuzimwa.
Katuga anaendelea, amemkumbusha Mtuhumiwa Shitaka lake na kumkabidhi taarifa ya mashitaka.
Anasema Jamhuri itakuwa na mashaidi 30 na vielelezo vya myaraka 9.
Maelezo yataanza kusomwa na Thawabu Isa wakili wa serikali.
Anasimama na kuanza kusema SSP Kangio, atakuwa shahidi wa kwanza. Ameapa kusema ukweli na maelezo yake ni kama ifuayavyo.
Nimeajiriwa 2003 polisi na mikoa mbalimbali ninefanya. Nimekuwa na vyeo tofauti na sasa ni mrakibu wa polisi kanda ya Dar es salaam. Nafanya majukumu ya kusimamia askari katika majukumu ya kiupelelezi.
04/04/2025 nikiwa ofisi afande Kaaya anayefanya Doria mtandaoni nilimtaka anipe picha mjongeo kuhusu maudhui yakiyokuwa yanatoa taarifa yenye uchochexi.
Maudhui hayo ni mapolisi wanakuja na mabegi ya kura feki kwenye vituo. Jambo ambalo ni uongo. Majukumu yetu ni ulinzi na sio kuiba kura.
Pia maelezo yaliyokuwepo ni kuhusu majaji ni MACCM hivyo wanafanya kazi kwa mujibu wa CCM. Na sio kweli kwamba majaji wanafanya kazi kuwaonea wapinzani. Na hivyo taarifa hii ni uongo na yalilenga kuleta chuki.
Pia alisema kuenguliwa kwa wapinzani ni mkakati wa serikali hivyo zilikuwa ni uongo na kutengeneza chuki dhidi ya Rais.
Na msimamo wetu ni wa uasi. Ni kweli ni msimamo wa uasi kwani tunaenda kukinukisha na huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli.
Katika picha mjongeo hiyo mzungumzaji alikuwa ni LISSU. Na aliyokuwa anafanya yalikuwa na nia ya kuitishia serikali ili ayapate yeye na wafuasi wake.
Niliamuru Insp. Kaaya aanze kufanya uchunguzi wa jalada hilo na taarifa hiyo ndio akafungua kesi na kuanza uchunguzi. Na akaanza kujaza PF500
Baada ya kutoa maelekezo kutafuta mjengeo iliyoerekodiwa eneo husika nilitoa taarifa kwa mabosss wangu na kuhusu kile alichosema TUNDU LISSU mtandaoni. Niliripoti kwa afande DCI akasema tuendeleee
Nilimtafuta kiongozi wa JAMBO TV anipe video ile na baadae akasema video anayo P ambae kasafrir. Hivyo nikatoa taarifa kwa maboss kuwa video tutaipata kwa P ambayo yuko Dodoma.
DCP NG'ANZI nilimpa taarifa kuwa tutaipata kwa kijana wa Jambo TV ambae yuko Dodoma.
Haya ni maelezo ya George ambae ni kaimu mkuu wa upepelezi kanda ya Dar es salaam. Yansomwa maelezo yake hapa mahakamani.
Nikaeleza lifunguliwe kosa la uhaini kwasababu aliesema TUNDU lisuu hayo maneno yake, yeye ni Askari ambae ana cheti cha Kujenga taifa kutoka jeshi la JKT hivyo alikuwa na wajibu wa kulinda amani ndani ya Taifa letu. Kusema maneno kama hayo ni kosa kisheria.
Hayo ndio maelezo yangu yote. Yameisha maelezo ya George na anasemaa anayo maelezo ya nyongeza Ya huyo SSP George akasema pia nilikabidhiwa TUNDU LISSU akitokea RUVUMA.
Nilimpokea Lissu na wakati nafanya mahojiano walikuja mawakili wake pia Tulienda kwenye ofisi yenye utulivu na nikamuonya kuwa anatuhumiwa kosa la uhaini. Na kumpa haki zake za msingi.
Huyu George ni msaidizi wa Mafwele. Anasemaa Lissu aligoma kutoa maelezo yoyote.
ASP. John. Ni shaidi wa pili ambae ni mkazi wa Temeke. Amekula kiapo na ushaidi wake ukaanza kuandikwa.
Nimeajiriwa 2005 na nina elimu ya computer na mfanyakazi wa polisi. Nimesoma vyuo ikiwemo Chuo Cha Polisi kurasini.
Nafanya kazi kwa DPP dawati la Doria mtandaoni. Na huwa napeleleza makosa yanayofanywa mitandaoni.
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Retweet yako.